Tanzania Tech
2.04K subscribers
191 photos
2 videos
1 file
2.77K links
Tovuti ya Habari na Mafunzo Mbalimbali ya Teknolojia Tanzania.
Download Telegram
Samsung Yasitisha Kutoa Support kwa Simu za Galaxy S8
https://www.tanzaniatech.one/2021/05/samsung-yasitisha-support-kwa-galaxy-s8/

Kama wewe ni mmoja wa watumiaji wa simu za Samsung Galaxy S8 na S8 Plus (https://www.tanzaniatech.one/2017/03/sifa-za-samsung-galaxy-s8-na-s8-plus/), basi ni vyema kufahamu kuwa kampuni ya Samsung hapo jana imeitoa simu hiyo kwenye list ya simu ambazo zinapewa support na kampuni hiyo. Kuanzia sasa simu hizo za Samsung Galaxy S8 na S8 Plus zitakuwa hazipati masasisho update yoyote ya ulinzi kama ilivyokuwa kwa miaka minne iliyopita. Hii ina maana kuwa simu hii sasa haipo kwenye list ya simu za kununua kwa sasa. Kama wewe ni msomaji wa Tanzania tech utakuwa unajua kuhusu makala ya kwanini usinunue simu yenye umri zaidi ya miaka minne (https://www.tanzaniatech.one/2021/02/kwa-nini-usinunue-simu-yenye-umri-zaidi-ya-miaka-4/). Kama hujasoma makala hiyo basi nakushauri ukasome makala hiyo sasa. Kwa sasa kama unataka kujua kama simu yako ipo kwenye list ya simu ambazo Samsung wana support, unaweza kubofya link hapo chini kuona kama simu yako inapatikana kwenye list ya simu hizo. Tembela Tovuti Hapa (https://url.tanzaniatech.one/TdW) Samsung Galaxy S8 ilizinduliwa mwaka 2017 na Kioo cha inch 5.8 chenye teknolojia ya Infinity Super AMOLED curved display ambacho kina resolution ya 2960 kwa 1440. Tetesi : Jiandae na Simu Mpya ya Galaxy S21 Mapema (2021) Kwa upande wa Processor Galaxy S8 inakuja na processor ya Qualcomm Snapdragon 835 au Exynos 8895, pamoja na RAM ya GB 4 na uhifadhi wa ndani kati ya GB 64 au GB 128.
Code za Siri za Android Kwaajili ya Simu za Samsung
https://www.tanzaniatech.one/2021/05/code-za-siri-za-samsung/

Simu za Android ni moja ya simu ambazo zina mambo mengi sana pengine kuliko simu janja za mfumo wowote ule, kwa kutumia code za siri unaweza kufungua sehemu nyingine muhimu kwenye simu yako ya Android. Kwa kuanza leo tunakuletea Code za siri za simu za Android za Samsung, Code hizi zinaweza kukusaidia kufungua menu za siri ambazo zinaweza kukusaidia kufanya mambo mbalimbali kwa urahisi na haraka. Basi bila kupotesa muda twende tukangalie code hizo, kumbuka code hizi zinaweza zisifanye kazi zote ila lazima kuna ambazo zitafanya kazi kwenye simu yako ya Samsung. Code za Siri za Simu za Samsung (Android) Kuangalia IMEI Namba – *#06# Kuangalia Mfumo wa Simu – *#1234# Kuangalia Matatizo ya Simu na Menu Kuu – #*#4636#*#* Ku-reset simu – *#*#7780#*#* Kuonyesha Code za Simu – *2767*4387264636# Majaribio ya GPS – *#*#1472365#*#* Kuangalia SW na HW – *#12580*369# Address ya Bluetooth – *#232337# Kuangalia ADC – *#0228# Uchaguzi wa RF Band – *#2263# Majaribio ya Bluetooth – *#232331# Majaribio ya WLAN – *#232339# Majaribio ya Vibration – *#0842# Kuangalia WLAN Mac Address –  *#232338# Majaribio ya Sauti – *#0673# Majaribio ya Pamoja – *#0*# Majaribio ya USB – *#872564# Mpangilio wa GCF – *#4238378# Majaribio ya Clock – *#0782# Majaribio Audio Loging – *#0283# Majaribio ya LBS – *#3214789650# Mpangilio mkuu wa GPS – *#1575# Majaribio ya Proximity Sensor – *#0588# Mfumo wa kamera – *#34971539# Majaribio ya Light Sensor – *#0589# WLAN Engineering Mode – *#526# Debug Dump Menu – *#746# NAND Flash S/N – *#03# Kuangalia Mfumo – *#44336# Mpangilio wa mfumo wa System Dump – *#9900# Mpangilio wa SD Card – *#273283*255*663282*# Mpangilio wa utumiaji wa data – *#3282*727336*# Mpangilio wa mfumo wa TSP / TSK  – *#2663# Menyu ya Camera Firmware – *#7412365# and *#*#34971539#*#* Mpangilio wa WLAN Engineering – *#528# Majaribio ya Melody – *#0289# Menyu ya OTA – *#8736364# Kumbukumbu za Majaribio – *#07# Mpangilio wa HSDPA/HSUPA – *#301279# Menyu ya Majaribio ya Haraka – *#7353# Mpangilio wa Lock – *#7465625# Mpangilio wa majibu ya automatic – *#272886# Updating…… Washa Tochi ya Smartphone kwa Kutingisha SimuNa hizo ndio baadhi ya code za siri ambazo unaweza kuzitumia kuweza kufungua menyu ya siri kwenye simu yako ya android ya aina ya Samsung. Kumbuka sio kila kodi zitakuwa zinafanya kazi kwenye simu yako. Pia kumbuka menyu hizi zimewekwa siri kwa sababu ya kuwa ni muhimu na zinauwezo wa kuharibu au kuonyesha data za siri zinazoweza kusababisha mtu au wewe mwenyewe kuaribu simu yako, Hivyo ni muhimu sana kuwa makini kwani hatuta husika pale utakapo haribu simu yako. Kama wewe ni mtumiaji wa simu nyingine kama Tecno na nyingine kama hizo endelea kutembelea Tanzania Tech tutakuletea code za siri za simu hizo hivi karibuni.