JamiiForums
✔
23.9K subscribers
40.7K photos
3.6K videos
34.7K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Mtaalamu wa Mawasiliano na Vyombo vya Habari wa EAC, Lilian Kiarie akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2025 amesema Teknolojia imeimarisha Uandishi wa kiraia huku Watu wa kawaida wakipewa uwezo wa kuripoti matukio kwa wakati halisi, jambo ambalo limepanua Demokrasia ya upatikanaji wa habari

Ametoa wito kwa Waandishi wa Habari kuendelea kushikilia misingi ya ukweli, uadilifu na uwazi, pamoja na Serikali na wadau kulinda Uhuru wa Kujieleza na kukuza ubunifu, ili kuhakikisha Uandishi wa habari unabaki kuwa nguzo ya Demokrasia hata katika enzi za Akili Mnemba

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayOne

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia #AIandMedia #HakikiTaarifa #FactsChecking
Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Media Foundation, Dastan Kamanzi akizungumza katika Siku ya Kwanza ya Maadhimisho ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani ameyataja mambo matatu muhimu wanayohitaji Waandishi wa Habari ili kuboresha kazi zao

Amesema “Waandishi wanahitaji mambo matatu muhimu ili kuboresha kazi zao, kwanza ni Shauku inayohusisha kubadilika na kukua. Pili, ni Utayari unaohusisha Uwekezaji wa maarifa na Uwekezaji wa muda, tatu wanahitaji kudhamiria na kujikita kwenye Majukumu yao”

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayOne

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia #AIandMedia #HakikiTaarifa #FactsChecking
❤1
ARUSHA: Akizungumzia kuhusu kuwawezesha Wanawake kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 katika masuala ya Uhakiki wa Taarifa, Mkurugenzi Mtendaji wa #JamiiAfrica, Maxence Melo amesema Taasisi hiyo imekuwa ikitoa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wadau wa Habari Wanawake na programu hizo zimekuwa zikiendelea

Amesema “Tulikuwa na Mradi maalumu pamoja na WiLDAF kuhusu kuwajengea uwezo Wanawake, pia kama kuna mapendekezo mengine yoyote kutoka kwa Wadau tupo tayari kuyapokea na ikiwezekana kushirikiana nao.”

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia #VisitJamiiCheck #FactsCheck #HakikiTaarifa #FactsChecking #MisDis04
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Wakili Onesmo Olengurumwa, amesema Waandishi wa Habari wanao wajibu wa kusaidia umma kubaini Taarifa za ukweli na uongo, na wanaweza kutumia Teknolojia ya Akili Mnemba (AI) kuongeza tija licha ya kuwa nayo inachangia kuzalishwa kwa Taarifa za uongo

Ameyasema hayo Mei 2, 2025 katika mafunzo ya Siku moja ya Wanahabari 150, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, ambayo inaadhimishwa Mei 3, ambapo Kaulimbiu ya Mwaka 2025 ni “Uhabarishaji kwenye Dunia Mpya: Mchango wa Akili Mnemba/Unde kwenye Uhuru wa Vyombo vya Habari.”

Aidha, ametoa kongole kwa #JamiiAfrica ambayo imekuwa ikishughulikia kubaini Taarifa sahihi na zisizo sahihi kupitia Jukwaa la #JamiiCheck

Soma https://jamii.app/WPFD2025

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia #VisitJamiiCheck #FactsCheck #HakikiTaarifa #FactsChecking #MisDis04
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa ametoa wito kwa Wanahabari kuwa na kawaida ya kuhakiki Taarifa kabla ya kusambaza kama ambavyo imekuwa ikifanywa na JamiiCheck.com

Msigwa amezungumza hayo wakati akichangia mada katika Mkutano wa Wadau kujadili Mchango wa Sekta ya Habari kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City, leo Julai 9, 2025

Amesema “Nimeona Watu wa JamiiForums wana kitu kinaitwa JamiiCheck, wanachofanya ndio kilekile tulichojifunza shuleni kwamba unachotaka kukichapisha jiridhishe kuwa ni sahihi?”

Soma https://jamii.app/MsigwaOnJamiiCheck

#JamiiCheck #HakikiTaarifa #FactsCheck #FactsChecking #VisitJamiiCheck
❤2
Shiriki katika Mjadala wa "Mchakato wa Kuhakiki Taarifa Kwenye Vyombo vya Habari, Unaendana na Kasi ya Kuenea kwa Taarifa Potoshi" kupitia Instagram Live ya JamiiForums.

Usikose kujiunga nasi Machi 30, 2026, kuanzia Saa 12:00 Jioni hadi Saa 2:00 Usiku

#MisinformationAndDisinformation #HakikiTaarifa #FactsChecking #JamiiCheck
❤1
Katika mjadala huu wa “Mchakato wa Uhakiki wa Taarifa kwenye Vyombo vya Habari unaendana na kasi ya kuenea kwa Taarifa Potofu?”, tutachambua kwa kina namna Vyombo vya Habari vinatumia teknolojia pamoja na rasilimali zilizopo kukabiliana na Taarifa Potoshi.

Usikose kujiunga nasi Machi 30, 2026, kuanzia Saa 12:00 Jioni hadi Saa 2:00 Usiku kupitia Instagram Live ya JamiiForums.

#MisinformationAndDisinformation #HakikiTaarifa #FactsChecking #JamiiCheck
Jiunge nasi Machi 30, 2026 kupitia Instagram Live ya JamiiForums, katika mjadala wa: “Mchakato wa Uhakiki wa Taarifa kwenye Vyombo vya Habari, unaendana na kasi ya kuenea kwa taarifa potofu?” kuanzia Saa 12:00 Jioni hadi Saa 2:00 Usiku.

Kushiriki mjadala: https://jamii.app/MarekaniMedia

#MisinformationAndDisinformation #HakikiTaarifa #FactsChecking #JamiiCheck
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Usikose kujiunga nasi Machi 30, 2026, kuanzia Saa 12:00 Jioni hadi Saa 2:00 Usiku kupitia Instagram Live ya JamiiForums katika mjadala wa “Mchakato wa Uhakiki wa Taarifa kwenye Vyombo vya Habari unaendana na kasi ya kuenea kwa Taarifa Potofu?”

#MisinformationAndDisinformation #HakikiTaarifa #FactsChecking #JamiiCheck
Kujua hili na mengine mengi, usiache kujiunga nasi katika Mjadala wa “Mchakato wa Uhakiki wa Taarifa kwenye Vyombo vya Habari unaendana na kasi ya kuenea kwa taarifa potofu?” Jumatatu ya Machi 30, 2026, kuanzia Saa 12:00 Jioni hadi Saa 2:00 Usiku kupitia Instagram Live ya JamiiForums.

#MisinformationAndDisinformation #HakikiTaarifa #FactsChecking #JamiiCheck
Jiunge nasi leo Machi 30, 2026 kupitia Instagram Live ya JamiiForums kuanzia saa 12 jioni hadi saa 2 usiku katika mjadala wa “Mchakato wa Uhakiki wa Taarifa kwenye Vyombo vya Habari unaendana na kasi ya kuenea kwa Taarifa Potofu?” ambapo tutajadili nafasi ya teknolojia, changamoto pamoja na mbinu zinazotumiwa na vyombo vya habari katika kupambana na taarifa potoshi.

#JamiiForums #MisinformationAndDisinformation #HakikiTaarifa #HakikiKablaYaKupost
#FactsChecking #JamiiCheck
TUPO LIVE KUPITIA JAMIICHECK!!! 🔥📌🔨

Jiunge nasi leo Machi 30, 2026 kupitia Instagram Live ya JamiiCheck kuanzia saa 12 jioni hadi saa 2 usiku katika mjadala wa “Mchakato wa Uhakiki wa Taarifa kwenye Vyombo vya Habari unaendana na kasi ya kuenea kwa Taarifa Potofu?” ambapo tutajadili nafasi ya teknolojia, changamoto pamoja na mbinu zinazotumiwa na vyombo vya habari katika kupambana na taarifa potoshi.

Kushiriki Bofya instagram.com/JamiiCheck

#JamiiForums #MisinformationAndDisinformation #HakikiTaarifa #HakikiKablaYaKupost
#FactsChecking #JamiiCheck
❤2
Akishiriki katika Mjadala kuhusu Mchakato wa kuhakiki taarifa kwenye vyombo vya habari kuendana na kasi ya kuenea kwa taarifa potoshi, Mpoki Thompson, Mhariri Mkuu wa Mwananchi ameeleza namna Mchakato wa Kuhakiki taarifa katika Dunia ya sasa ya Kidigitali hauendani na mazingira ya ‘Media’ zetu.

Ameongeza kwamba "Uhakiki wa Taarifa unatakiwa kufanyika kabla ya Habari au taarifa yenyewe kwenda kwa umma, kwa sasa mara nyingi imekuwa tofauti na ndio maana watu wengi wamekuwa wakijutia kwani taarifa zinaenda kwa umma kisha baadaye ndiyo zinahakikiwa"

Mjadala https://jamii.app/MjadalaUhakiki

#JamiiForums #MisinformationAndDisinformation #HakikiTaarifa #HakikiKablaYaKupost
#FactsChecking #JamiiCheck
Akizungumza katika mjadala kuhusu Mchakato wa kuhakiki taarifa kwenye vyombo vya habari kuendana na kasi ya kuenea kwa taarifa potoshi, Nuzulack Dausen, Mtendaji Mkuu wa Nukta Africa, amesema kuwa kuna baadhi ya vyombo vya habari hufanya makusudi kupotosha taarifa kwa nia ya kupata fedha na sababu zingine.

Ameongeza kuwa sababu za kiuchumi zinaweza kuchangia taarifa potofu kwa kukosa watu sahihi wa kufanya uhakiki kwa kutokuwa na uwezo wa kuajiri au kulipa timu ya kufanya majukumu tofauti.

Mjadala https://jamii.app/MjadalaUhakiki

#JamiiForums #MisinformationAndDisinformation #HakikiTaarifa #HakikiKablaYaKupost
#FactsChecking #JamiiCheck
Akichangia mada ya kuhusu Mchakato wa kuhakiki taarifa kwenye vyombo vya habari kuendana na kasi ya kuenea kwa taarifa potoshi, Mtendaji Mkuu wa Nukta Africa, Nuzulack Dausen amesema kuwa “Kuna taarifa unaweza kuiona ni ndogo lakini ikienda upande fulani ni kubwa na ina umuhimu mkubwa kwa Mtu au Watu wengine na kumuharibia maisha".

Mjadala https://jamii.app/MjadalaUhakiki

#JamiiForums #MisinformationAndDisinformation #HakikiTaarifa #HakikiKablaYaKupost
#FactsChecking #JamiiCheck
Akichangia mada ya kuhusu Mchakato wa kuhakiki taarifa kwenye vyombo vya habari kuendana na kasi ya kuenea kwa taarifa potoshi Afisa kutoka JamiiCheck, Edward Chaina amesema “Idara ya JamiiCheck inahusika na mambo ya Uhakiki wa taarifa ikiwemo kuwajengea uwezo Wananchi, Wanahabari, Wanafunzi na watu wa makundi mbalimbali kuhusu elimu katika kutambua taarifa potoshi.”

Mjadala https://jamii.app/MjadalaUhakiki

#JamiiForums #MisinformationAndDisinformation #HakikiTaarifa #HakikiKablaYaKupost #FactsChecking #JamiiCheck
Akizungumza katika mjadala kuhusu Mchakato wa kuhakiki taarifa kwenye vyombo vya habari kuendana na kasi ya kuenea kwa taarifa potoshi, Edward Chaina, Afisa wa JamiiCheck, ameeleza namna matukio makubwa na misimu huchangia kusambaa kwa taarifa potofu kwa kiasi kikubwa.

Ameongeza kuwa "Wapotoshaji wengi wanacheza na hisia za Watu, hivyo wanachokifanya mara nyingi wanalenga hisia ili kumfanya mlengwa afanye kile ambacho wanakitaka au wanachokidhamiria"

Mjadala https://jamii.app/MjadalaUhakiki

#JamiiForums #MisinformationAndDisinformation #HakikiTaarifa #HakikiKablaYaKupost
#FactsChecking #JamiiCheck
Akichangia katika mjadala kuhusu Mchakato wa kuhakiki taarifa kwenye vyombo vya habari unaendana na kasi ya kuenea kwa taarifa potoshi, Mdau wa Jamiicheck ameeleza kuchukizwa kuona Mamlaka zikikanusha taarifa za kweli zilizotolewa na vyombo vya habari.

Mjadala https://jamii.app/MjadalaUhakiki

#JamiiForums #MisinformationAndDisinformation #HakikiTaarifa #HakikiKablaYaKupost
#FactsChecking #JamiiCheck
Akichangia mjadala kuhusu Mchakato wa kuhakiki taarifa kwenye vyombo vya habari unaendana na kasi ya kuenea kwa taarifa potoshi, Mpoki Thompson, Mhariri Mkuu wa Mwananchi ameeleza uzingatiaji wa uhitaji wa uwekezaji katika mifumo ya uhakiki taarifa sahihi.

Mjadala https://jamii.app/MjadalaUhakiki

#JamiiForums #MisinformationAndDisinformation #HakikiTaarifa #HakikiKablaYaKupost
#FactsChecking #JamiiCheck
Akizungumza katika mjadala kuhusu Mchakato wa kuhakiki taarifa kwenye vyombo vya habari kuemdana na kasi ya kuenea kwa taarifa potoshi, Nuzulack Dausen, Mtendaji Mkuu wa Nukta Africa, ametoa wito kwa Mamlaka husika za serikali kuwekeza katika kutoa elimu ili kuwepo na mwamko wa watu kutambua jinsi gani watabaini taarifa kwani siyo kila sehemu kunatakiwa kutumia Sheria,

Mjadala https://jamii.app/MjadalaUhakiki

#JamiiForums #MisinformationAndDisinformation #HakikiTaarifa #HakikiKablaYaKupost
#FactsChecking #JamiiCheck