Dini Ni Nasaha
795 subscribers
11K photos
540 videos
497 files
17K links
Helping to connect you to the senior salafi scholars, dedicated to educating and spreading as-Salafiyah with Wisdom
Download Telegram
💥*HALI TULIYO NAYO LEO: JAMBO NI HILO HILO; LAKINI LAU LITASEMWA NA YULE WASIYEMPENDA KATIKA MASALAFI BASI HAWATOKUBALI NA WATAMSHAMBULIA, LAKINI LAU LINGESEMWA NA SHEKHE KIPENZI BASI WANGELIPOKEA. HII SIYO MANHAJ YA SALAF KATU!*

_Amesema al-Hafidh ibn Rajab rahimahullah:_

*«Kwa hivyo, Maimamu wa Salaf ambao wamekubaliwa kwa pamoja kuhusu ilmu na fadhla yao walikuwa wakiikubali haki kutoka kwa yeyote aliyeileta kwao, hata kama alikuwa mdogo. Na walikuwa wakiwausia wenzao na wafuasi wao kuikubali haki pale inapodhihirika katika kauli isiyokuwa yao.»*
[الفرق بين النصيحة والتعيير-مجموع رسائله (٤٠٦/٢)].

(*فلهذا كان أئمة السلف المجمع على علمهم وفضلهم يقبلون الحق ممن أورده عليهم وإن كان صغيراً ويوصون أصحابهم وأتباعهم بقبول الحق إذا ظهر في غير قولهم.*)

*═══ ❁✿❁ ════*
*Salafi Da'wah East Africa (Salafi Da'wah Afrika Mashariki)*
⬆️_*Tuamke enyi ndugu vipenzi, sisi ni Masalafi sio Mahizbi, haya ni mambo ya Mahizbi na Watu wa Bid'ah ambao ni Watu wa Ushabiki na Ta'assub za Kijahiliyyah, Allah Atuondoshee haya. Allahul-Mustaa'n*_
_*Angalieni tofauti kati ya Salaf (Wema Waliotangulia), na sisi! Sisi, tunapomwona ndugu yetu ana shida, hata ikiwa tunaweza kutambua hali yake na kuona kwamba anahitaji msaada, tunataka mpaka aje mwenyewe kutuomba. Na unakuta yeye anajizuia kuomba maskini. Tunamwambia: “Una shida? Unahitaji kitu? Niambie...” Yaani, mpaka atuombe ndipo tunamsaidia?!*_

_*Na tukimsaidia: tunamsema au tunamdharau au kumfedhehesha na kumdogesha au kumdhalilisha au kumkandamiza au kumtajia kwamba tumemsaidia hiki na kile, au kumtangazia kwa watu..nk*_
_*Na hizi si tabia njema wala za Kiislamu wallah.*_
_*Allah Atuongoze sisi.*_
بسم الله الرحمن الرحيم.
الحمد لله رب العالمين، وصلى الله وسلم على نبينا محمد، وعلى آله وصحبه أجمعين، أما بعد:

Kwa idhini ya Allah, In shaa Allah, kesho tutachapisha makala ambayo tunawaomba ndugu zetu wote waipitie kwa umakini, wazisome hoja zilizomo ndani yake, wazitafakari na wazizingatie ipasavyo.

Haswa, dalili mbalimbali tulizozitaja, pamoja na kauli za Salaf na wanazuoni wetu wa Kisalafi, ili tuweze kuelewa vizuri yaliyowasilishwa na kuyapima kwa mizani ya haki na dalili.

Tunamuomba Allah atuongoze sote katika haqi, atuwezeshe kuifuata na atujalie kusimama imara juu yake mpaka tutakapokutana Naye.

*SDEA – Salafi Da'wah East Africa*
*MPYA📝*

📒 *Huu si Usalafi Wala si Njia ya Ulamaa Wa Kisalafi Wala si Majibu Ya Kielimu - SDEA 25.10.2026*


*DOWNLOAD, FUNGUA NA SOMA PDF*⬇️

*LINK 1:*
https://drive.google.com/file/d/11jEgWpuokNWbd4w4u67aQp7OVNZ5VL_r/view?usp=drivesdk


*LINK 2:*
https://ia903105.us.archive.org/28/items/huu-si-usalafi-sdea-25.10.2026-rev/HUU%20SI%20USALAFI%20-%20SDEA%2025.10.2026%20%281%29.pdf


Tunawaomba ndugu zetu wote waipitie kwa umakini, wazisome hoja zilizomo ndani yake, wazitafakari na wazizingatie ipasavyo. Haswa, dalili mbalimbali tulizozitaja, pamoja na kauli za Salaf na wanazuoni wetu wa Kisalafi, ili tuweze kuelewa vizuri yaliyowasilishwa na kuyapima kwa mizani ya haki na dalili na uadilifu.

Tunamuomba Allah atuongoze sote katika haqi, atuwezeshe kuifuata na atujalie kusimama imara juu yake mpaka tutakapokutana Naye.

*═══ ❁✿❁ ════*
*Salafi Da'wah East Africa (Salafi Da'wah Afrika Mashariki)*
بسم الله الرحمن الرحيم الحمد لله و صلى الله وسلم على نبينا محمد وعلى آله وصحبه أجمعين، وبعد؛

Inshaallah, kesho tutajibu baadhi ya shubuhati ambazo wamezileta baadhi ya ndugu zetu masalafi Allah atuongoze sisi na wao, baada ya kuenezwa hii Makala.

Pamoja na kwamba maswali tuliyouliza kwenye makala, hata MOJA halijajibiwa, hata moja. Lakini la ba's. Sisi tutajibu baadhi ya yale ambayo wametuhumu/wameleta ishkaal kwayo Bi idhni-llaah.

Kama vile dhulma ambazo wamewafanyia ndugu zao waliokosoa, ikiwemo kudai kwamba siyo Masalafi, bila kutaja hoja ya Msingi wala dalili: *"SIO MASALAFIY...."*

Na atakayeuliza dalili ya hilo ataambiwaje; *"NA WEWE UNAWATETEA? NA WEWE SIO SALAFI?!"* Vitisho na mabavu, irhab fikri na atifi (Ugaidi wa kifikra na kimihemko)

Kwa hiyo, hayo na mengine, Inshaallah, tutayazungumzia kesho, Bi idhni-llaah.

Lakini tunawasihi nyinyi ndugu zetu msome hiyo makala Baarak Allahu Feekum. Ikiwa kuna kosa, sisi milango yetu abadan hatujaifunga, tufikishieni. Kuna email/barua pepe tumeiweka hapo; tutumieni, mtuambie kosa liko wapi kwa dalili. Kama lipo, Wallahi, tutalirekebisha hapo hapo na kutarajaa', wallah wabillah.

Haswa msisite kufaidika na ufafanuzi mzuri kutoka kwa Ulamaa Wakubwa wa Kisalafi tuliounukuu humo, hao pia sio Masalafi?

Na kama kwenye makala kuna baatil, wewe usikubali baatil, ikosoe, dini si mali binafsi ya mtu, Alhamdulillah.
Na kama kuna kitu kilichosemwa ambacho ni haki, basi ni wajibu kwako kuichukua haki hiyo.

الحق ضالة المؤمن، أينما وجده أخذه.

"Haki ni kitu kitafutwa cha Muumini; popote anapoipata, huichukua."

Jazakum Allahu Khayran wa Baarak Allahu Feekum

*SDEA – Salafi Da'wah East Africa*
*MUENDELEZO:*


Na tunaomba ndugu zetu Baarak Allahu Feekum waulize maswali, au ni haramu na makosa kuuliza maswali ya msingi pale mtu anapopewa hukmu juu ya mtu mwingine? Haitakiwi kuuliza?

Kwa mfano, ukiambiwa kwamba fulani anayeswali na kufunga na hafanyi shirk bali anapinga shirk na anatetea Tawhid, ukaambiwa *"HUYU SI MUISLAMU!"* au *"HUYU MSHIRIKINA!"* Huruhusiwi kuuliza: Kwa nini si Muislamu? Kwa nini au vipi Mshirikina?

Bila shaka, anatakiwa kuthibitisha madai yake kwa dalili kwamba huyu si Muislamu. Amefanya kitenguzi gani katika vitenguzi vya Uislamu mpaka akahukumiwa kuwa si Muislamu au Mshirikina?

Haya, sasa tunaomba muwaulize wale wanaosema kwamba Salafi Da‘wah East Africa [SDEA] si Masalafi:

1. Ni lini walipotoka katika Usalafi?


2. Ni jambo gani lililowatoa katika Usalafi?


3. Tufahamisheni, bid‘ah yao ni ipi na iko wapi?


4. Je, ni Makhawarij? Je, ni Mahizbi? Ni watu wa Twariqa za Kisufi: Maqadiriyyah au Naqshabandiyyah au Shadhiliyyah, ni wepi? Ni hizbiyyah gani waliyonayo? Ni Hizbu Tahreer? Ansar Sunnah? IKhwani au Sururi? Ni Mahalabi au wafuasi wa Muhammad al Imam au Hajoori au Muhammad bin Hadi? Ni watu wa Siasa? Tubainishieni tena kwa ushahidi (dalili)


5. Je, wanashirikiana na watu wa bid'ah?


6. Je, kuna sehemu yoyote ambayo wamekhalifu Sunnah? Au wamekhalifu Asl katika Usool za Sunnah?


7. Je, wamefanya makosa yoyote yanayomtoa mtu katika Manhaj ya Ahlus-Sunnah?


8. Na kama ambavyo tumetuma baadhi ya maneno ya Shaykh Rabīʿ na wengine katika wanazuoni, yanayoonyesha kwamba inajuzu kukuosolewa mtu hata awe ni imamu mkubwa, na mwanachuoni wa Sunnah. Lakini haifai kumkosoa taalib ilm wa kwetu, na ukimkosoa wewe unakuwa si Salafi?Hizi qawāʿid zimetolewa wapi?


9. Je Ustadh akitarajaa haya makosa, na tunamdhania kheri biidhinillah, Allah Ampe Tawfiq; nanyi mtatarajaa' pia? Kwa hiyo huo wenu ni ushabiki au ni msimamo wa Kielimu na Kidini?


Au hairuhusiwi kuuliza; tuwe kama Masufi wanavyosema kwenye vitabu vyao:

«كُنْ بَيْنَ يَدَيِ الشَّيْخِ كَالْمَيِّتِ بَيْنَ يَدَيِ الْغَاسِلِ»
“Kuwa mbele ya sheikh wako kama maiti ilivyo mbele ya mtu anayei­osha?”


Allah Awabarik nyote.


*SDEA – Salafi Da'wah East Africa*
💥*MWAMBIENI MWENYE KUWATAHADHARISHA MASALAFI WENZIE NA KUAGIZA WATENGWE; AFRIKA MASHARIKI AU KWINGINEKO: ZIKO WAPI HOJA NA DALILI ZAKO ZA WAZI KAMA JUA??!*


_Katika aliyosema al-Imam Rabii' al-Madkhali (Rahimahullah):_

*....Basi mcheni Allah na muwe na upendo na umoja baina yenu, na msikubali maneno ya yeyote isipokuwa kwa hoja na dalili. Na yeyote anayekubali maneno ya kumtwaa'ni mtu au kuwatuhumu Masalafi bila dalili, basi anaweza kujumuishwa na Watu wa bid’ah....*

*....Hivyo basi, mcheni Allah, shikamaneni, na shikamaneni na Kitabu cha Allah na Sunnah ya Mtume wake ﷺ, wala msikubali tuhuma yoyote kutoka kwa mtu yeyote—haijalishi ni nani—isipokuwa kwa dalili zilizo wazi kama Jua....!*

*.....Ama tuhuma, kejeli na mashambulizi ya batili, basi hayo hufanywa na watu wa matamanio na bid’ah (Ahlul-Ahwaa). Hivyo mcheni Allah na jiepusheni na njia zao na mbinu zao. Shikamaneni na pendaneni, na muwe kama mwili mmoja: unapoumwa kiungo kimoja, mwili wote huathirika kwa homa na maumivu....*

*.... Nasisitiza jambo hili juu yenu—nasisitiza sana—kwamba mshikamane na muwe na mapenzi, na mupuuze na kutupa mbali sana maneno ya watu ikiwa hayana dalili, haijalishi ni nani..!*

Rejea: https://youtu.be/k2e227qNejs?si=iELHIgqb5y4w0e1B

*════ ❁✿❁ ════*
*Salafi Da'wah East Africa* *(Salafi Da'wah Afrika Mashariki)*

https://whatsapp.com/channel/0029VabMSx07tkj3R6Dou41f
Kwanza, waoneni baadhi ya wale ambao wametahadharisha kwamba sisi [SDEA] siyo Masalafi. Hawa hapa kwenye channel yao. Na hizi ni miongoni mwa posts zetu ambazo wao walikuwa wakishare kwenye channel yao.

Sasa, mbona tanaqudh na kujigonga? Yaani, jana tulikuwa Masalafi, leo tumekuwa siyo Masalafi, siyo? Kwa nini? Kwa dalili na msingi gani? Au ni hawaa (matamanio yaki binafsi)? Kwa sababu tumesema kwamba huyu ustadhi wa Kisalafi, Allah ampe tawfiqi, maneno aliyoyasema amekosea!! Kwani Masalafi (Ahlus-Sunnah) hawakosoani au kurekebishana au kuraddiana kielimu?

Na mwingine yeyote anayetahadharisha huko pembeni kuwa eti sisi sio Masalafi basi muulizeni yale maswali ya jana, awapeni ushahidi wa madai hayo makubwa Baarak Allahu Feekum.

Ama atakayetoka hadharani na kusema hivyo, pia tutakuwa na waqfa na maneno yake hayo Bi idhni-llaah, hakuna aliye juu ya Sheria, Allah Awabarik.

Huwezi kumtusi mzazi wa binti eti ni dayuthi, hii sio haqi hii ni dhulma. Huwezi kumcheka mtu na kumfanyia maskhara / istihzai kwa sababu amekosea herufi na jambo la kilugha. Mbona hata wanachuoni wetu wanakosea katika mambo hayo? Ni ubinadamu ati. Kwa hiyo, na wao (wanachuoni) wafanyiwe hivyo hivyo, wakejeliwe? Huku si ni kuwafungulia mlango Watu wa Bid'ah wawatusi Ahlu Sunnah?? Bal hizi sio njia za kielimu katika kuraddi wala hatuoni Ulamaa wetu wakifanya hivyo.

Kwa hiyo: Ustadhi akisema maneno yenye makosa, ukasema; amekosea, wewe hapo hapo unakuwa umetoka katika Usalafi?

Allah Anasema;
{وَإِذَا قُلْتُمْ فَاعْدِلُوا} سورة الأنعام (الآية 152)

*"Na msemapo basi semeni kwa uadilifu"*

Hebu acheni hizi dhulma, enyi ndugu, kuna Qiyama. Hii siyo dini ya Allah, wala hii sio njia ya Ahlu Sunnah.
Na pia, nasaha zetu zimewaelekea watu wengine katika ndugu zetu Masalafi.
Tumeona katika mitandao ya kijamii kwamba baadhi ya ndugu zetu Allah awape wao na sisi hidaya na tawfiq wamesema yule mwanamke ni *"KAHABA WA KIKHURAFI."* Subhanallah!

Enyi ndugu zetu Allah Awabarik, mtu akishakuwa mtu wa bida'h, je, inakuwa inaruhusiwa kumfanyia na kumwambia vyovyote tu? Hata kafiri hairuhusiwi kumfanyia hivyo (kumdhulumu na kuvuka mipaka) vipi Muislamu?

Tumewanukulia maneno ya Ulamaa ambao ni maarufu kwa kuwaraddi Watu wa Bid'ah kama vile Shaykh Rabii' rahimahullah akikataza mambo hayo, au naye anakuwa si Salafi!!? Kuwa salafi ni mpaka uwatusi watu na uwe na mdomo mchafu, maneno machafu!!?

Haijuzu kupinga munkar kwa munkar na wote tunajua hili, na makundi yenye misimamo mikali kama Makhawarij na Mahaddadi na Ansar Sunnah nk wamepotea pia kwenye mlango huu, uongo?

Je, mtu kumwita Muislamu ni kahaba bila mashahidi wanne (4) walioshuhudia kitendo hicho kichafu: si ni QADHF hii? Si huyu aliyesema ingekuwa kwenye Sharia ya Kiislamu anatakiwa kupigwa bakora themanini (80) pamoja na hukumu nyingine zilizokuja katika Qur’ani na Sunnah kuhusu mtu aliyefanya kitendo hiki cha kumzulia Muislamu Uchafu??

Sasa, sisi tunapokosoa kwq dalili na kusema kwamba: hawa ni ndugu zetu Masalafi ndio lakini wanakosea na wanaitukanisha Sunnah hivi na haya ni makosa, tunaambiwa kwamba sisi siyo Masalafi??

Haya basi tuonyesheni Usalafi huu wa matusi na kuwatuhumu watu bila kujali kutoka kwa Ulamaa Wakubwa Wakisalafi, nani kasema na amefanya hivi: Bin Baz? Al Albani? Muqbil bin Hadi, Rabii' al Madkhali, Saleh Al Fawzan, Ibn Uthaymeen?? Tumche Allah, kuna hesabu, au mtu akiwa salafi yeye hata kuhesabiwa hahesabiwi?? Yuko huru kufanya na kusema atakavyo??

Lau kama mtu ataitakidi hivyo basi atakuwa na itikadi ya Murjia ambao wao wanakwambia; "Imani ya mlevi ni sawa sawa na Imani ya AbuBakr na Umar (Allah Awaridhie)." Maasi na maovu haidhuru !!

Tumeweka dalili katika Makala yetu jinsi Mtume alivyokasirika alipoona vitendo vinavyoweza kuwafukuza watu akisema:

إن منكم منفرين

"Hakika miongoni mwenu wapo wenye kuwafukuza watu (kwa maneno au vitendo vyao)."

Haya bid'ah yetu ni nini??

Bali, tumenukuu kutoka kwa Mtume (swalallahu alayhi wasallam). Maneno ya Mtume swalallahu alayh wasallam kwamba usimtukane mtu wala kumuaibisha hata kama yeye amekutukana na kukuaibisha. Tumeweka mambo haya kwa dalili, na tumenukuu maneno ya Ulamaa wakubwa kuhusu mambo haya, wazi kabisa.

Sasa, ni wapi tulipokosea sisi? Hebu tukuosoeni kielimu basi Baarak Allahu Feekum.

Bali, tumegundua kwamba hatuna kosa isipokuwa kusema kwamba ustadhi waki Salafi amekosea. Tumesema kwamba ustadhi ni Salafi, lakini amekosea. Hili ndilo tuliloona kwamba ndiyo dhambi yetu.

Na eti, hiyo ni dhambi na kosa kubwa kiasi cha kututoa katika Usalafi!! Mcheni Allah

Sasa, ndiyo maana tunataka uthibitisho. Mtuthibitishie kwamba kusema kuwa ustadhi amekosea ni kosa. Bali, ni kosa kubwa kiasi cha kumtoa mtu katika Usalafi na kumfanya kuwa mpotevu.


Tunasubiri Baarak Allahu Feekum.
Hebu tazameni maneno kama haya. Huu ndio usalafi? Ulamaa wetu waki Salafi wanatumia maneno haya na njia/usloob hizi duni za kejeli? Unapoona kwamba makosa yamefanyika na ustadhi ambaye anasikilizwa na watu wengi, kisha unaona kwamba makosa hayo yamepokelewa vizuri, yaani watu wameyafurahia, halafu wakayaeneza kama hivi, basi inafaa makosa kama haya yasahihishwe ili mtu asije akafahamu na kudhani kwamba Masalafi wanaamini hivi na kwamba huu ndio Usalafi wao na hivi ndivyo wanavyofundishwa na ulamaa wao.

Hili ndilo lengo linalotakiwa: kwamba ile Sunnah ya Mtume (swalallahu alayhi wasallam) na Manhaj Salaf tunayozungumzia ilindwe.

Ama kuhusu mtu, sisi tunasema kwamba yeye ni Salafi lakini amekosea. Wala hatujasema kwamba yeye siyo Salafi.

Je, maneno haya yanakubalika? Hebu kuweni waadilifu. Je, maneno haya ni sawa? Je, Sunnah imetufundisha hivi? Wapi?!


Baarak Allahu Feekum
1. Makhawārīj tunawakosoa kwa kuasi watawala, kuwakufurisha Waislamu kwa sababu ya maasi na kumwaga damu zao, nk; wao hutushutumu kwa kuridhia makosa ya watawala na kuridhia maasi. Na hawa ndugu zetu nao wanatushutumu kuwa eti "tunamtetea huyo mtu wa bid'ah.."


2. Tumekosoa kitendo cha mwanamke huyo zaidi ya sehemu moja. Je, hamjasoma ile makala?


3. Ahlus-Sunnah hawaondoi munkari kwa munkari. Kukosoa makosa hakuhalalishi kufanya makosa mengine.


4. Tunawakosoa ndugu zetu Salafiyūn kwa kuwatakia kheri na kuwanasihi, kama tunavyowaraddi watu wa bid'ah kwa dalili na maneno ya Ulamaa. Katika kadhia hii tumejikita zaidi kwa ndugu zetu Masalafi kwa sababu; wao ndio familia yetu na wengine ni jamii ya nje, nyumbani kwako kukiwa na ufisadi na huko nje kukiwa na ufisadi pia; utajikita zaidi kurekebisha nyumbani kwako.


5. Radd haimaanishi matusi, kejeli, kushambulia wazazi wa watu au kudhihaki usomaji wa ibara. Hii si njia ya Ulamaa wala malezi sahihi kwa vijana wetu.


6. Makosa ya hadharani yanaponasibishwa na Salafiyyah, tutayakosoa kwa njia nzuri bila kuvuka mipaka, bi idhni-llāh.
Na leo usiku tutatuma sehemu ya mwisho ya majibu yetu juu ya shubuhāt na ishkalaat walizozileta baadhi ya ikhwa in shaa Allah.

Na tutakuwa tumefunga ukurasa huu.
Mpaka pale itakapohitajika tena kuufungua.

Na tutaendelea na programs zetu za kila siku na kupeana faida biidhinillah.

Allah Awabarik nyote na Awahifadhi.
Sehemu ya Mwisho ya Majibu ya Shubuhāt na Ishkalaat

*[A]*
*HISTORIA HAIFUTIKI: MAJIBU YA TUHUMA ZA UHIZBI NA UKHURAFI DHIDI YA SALAFI DA‘WAH EAST AFRICA.*

1. Hivi, ndugu zetu mumeshawahi kuona sisi tukiposti na kuwaenezea mfano: Muhammad Bacho, au Barahayani, au mwingine yeyote katika Mahizbi? Je, mumewahi kuona tukimuenezea yeyote katika Mahizbi wa Afrika Mashariki au nje?


2. Akina Muhammad al-Imam, akina Muhammad bin Hadi, al-Hajuri, Halabi nk. Watu ambao unakuta tulishawatahadharisha—kama kawaida, kwa kutumia maneno ya Wanachuoni.


3. Ni nani aliyesimama mwanzoni katika fitnah zilizopita khasa fitna ya Muhammad bin Hadi huku Afrika Mashariki na kubainisha mambo mpaka wakapigwa vita? Ni nani? Historia haifutiki, na rekodi hizo tunazo (Na tunajua mpaka leo kuna ambao wanamtetea Ibn Hadi, na baadhi mnajua hili).


4. Alhamdulillah, hatujawahi kuchanganya Haq na Baatil, wala kuwafanyia watu ghishi (kama wanavyofanya baadhi—na tutawabainisha In shaa Allah).


5. Alhamdulillah, na hiyo ni fadhla ya Allah na tunaomba Allah Atupe Thabat mpaka Mamaat.


6. Kipindi cha kudhihiri kwa fitnah ya bin Hadi:

Hao Salafi Da‘wah East Africa walipigwa vita kwa sababu wao walitangaza maneno ya Wanachuoni Wakubwa kama Sheikh Rabīʿ, Sheikh ʿUbayd na wanazuoni na masheikh wengine kuhusu Muhammad bin Hadi. Walieneza maneno ya Kibar wakiwatahadharisha Masalafi juu ya Fitna ya bin Hadi.

Kwa sababu hiyo, wakapigwa vita. Sikiliza dhambi yao, waliambiwa hivi: *“Kwa nini munawatangulia masheikh zetu?”*


7. Subhanallah! Yaani sisi katika miji yetu tuna masheikh ambao mpaka maneno na maelekezo ya Ulamaa Wakubwa duniani kwa Masalafi wote duniani hayaruhusiwi kuenezwa mpaka wao (hao masheikh wa kwetu) wayapitishe!!? Hili ni jambo hatari. Yaani sisi tuna Usalafi wa kivyetu huku kwetu?


8. Rekodi tunazo na historia haifutiki, na baadhi yenu mnayajua haya vizuri.


9. Sasa, kuna wanaodanganyana na kudanganya wengine. Wanawadanganya ndugu hasa wageni, ili wasisome yale tunayoeneza. Pamoja na kwamba sisi tunanukuu maneno ya wanazuoni na tunaweka mambo wazi kwa ushahidi, wanadanganya kwamba huenda sisi ni Mahizbi au Makhurafi. Vichekesho hivi! Allahul-Musta‘an.


10. Hebu tuonyesheni Uhizbi na Ukhurafi wetu uko wapi! Tunawapa challenge: tuonyesheni kwa ushahidi, mmoja tu wala si kumi!


11. Sisi tunakuwa Mahizbi pale tu tunaposema kwamba Ustaadhi fulani, kipenzi sana, amekosea kwa ushahidi huu na huu? Hapo ndipo tunapoanza kuhusishwa na Hizbiyyah, kana kwamba kumkosoa sheikh kipenzi kwa ushahidi si tu ni kosa lisiloruhusiwa, bali ni tiketi ya kumtoa mtu kwenye Usalafi?


12. Hii ipo kwenye Asl gani katika Usul za Ahlu Sunnah? Usul Sunnah ya Imam Ahmad? Sharh Sunnah ya al-Barbahari? Sharh I‘tiqad ya al-Laalakaai? Taqriiraat za Imam Rabii‘ au Ubayd al-Jabiri (Allah Awarehemu wote), au wapi?


13. Je, mumewahi kuona katika platforms/majukwaa yetu kwenye social media tukimuenezea yeyote miongoni mwa masheikh wa bid‘ah? Au Mahizbi? Hata mmoja, hata mara moja, umewahi kuona jambo hili?


14. Platforms/majukwaa yetu, Alhamdulillah, yote yako wazi kwa umma; WhatsApp, Telegram, nk. Mtu anaweza kuingia, akasearch na kuangalia mambo tunayoyaposti. Sisi tunaposti kutoka kwa Ahlul-Ilmi wa Kisalafi wanaofahamika duniani, tunatafsiri maneno yao na kueneza fatwa zao pamoja na kauli zao. Hii ndiyo kazi ambayo tumekuwa tukiifanya kwa miaka sasa.


15. Sasa, kwa nini kuwadanganya watu wengine kuhusu sisi na kuanza kutuhusisha kwa uwongo na watu wa Bid‘ah na Mahizbi? Wapi ushahidi? Hebu tajeni mmoja tu!


16. Wallahi, tunawapa challenge hawa watu: Waonyeshe mfano mmoja tu wa sisi kushirikiana na watu wa bid‘ah katika machapisho yetu, kuwaenezea maneno yao au kufanya mfano wa mambo hayo. Watafute, waangalie na walete ushahidi ikiwa watapata! نتحداهم


17. Lakini cha ajabu ni kwamba wapo baadhi ya ndugu zetu hawakubali ustadh fulani akosolewe, na sisi hatusemi kwamba si Masalafi. Sisi tunasema wazi kwamba ni Masalafi, lakini wamekosea. Na makosa hukosolewa kwa adabu zake, bila kujali ni nani, kama wanavyobainisha Ulamaa. Tena, haswa ikiwa kosa limeenezwa hadharani na linatafsiriwa kuwa eti hiyo ndiyo dini na ndiyo Sunnah (Salafiyyah), bali ni wajibu kukosolewa kosa kama hili atakama kutoka Salafi. Na hatujawahi kumsingizia mtu, Alhamdulillah.


18. Bali mara ngapi tunawanasihi ndugu zetu kwa private (kwa siri), watu hawajui. Subhanallah! Mpaka tumeshawahi kutumia baadhi ya Mashaykh wakubwa duniani: “Tafadhali ya Shaykh; mnasihi huyu ndugu yetu labda atasikia maneno yako....” Na majibu yakawa ujeuri? Ndiyo, yametokea haya, Baarakallahu feekum, na ushahidi tunao.


19. Kisha angalieni upendeleo wa kishabiki na ta‘assub hii, na huu ni mfano tu: Mmnajua kuwa wapo miongoni mwa walinganizi wa Kisalafi kwetu ambao wameshirikiana na watu wa bid‘ah zaidi ya mara moja, Masufi kwenye misikiti yao. Tena walikaribishwa kwa kutolewa muqaddimah na shekhe wa Kisufi, hawa hawa watu wa bid‘ah.


20. Kila mtu analijua jambo hilo, lakini hatujawahi kuwaona wakishambuliwa popote pale kwa sababu hiyo, katu.


21. Sasa, huu ndio uadilifu ambao mmejifunza wapi, ndugu zetu? Kuwashambulia watu kwa makosa ambayo hawana huku wale ambao wamefanya makosa ya wazi, tena ya mikhalafa ya Kimanhaj na Suluk, hamuwakosoi wala kurekebisha makosa yao ili yasidhaniwe kuwa ni katika Dini ya Allah. Badala yake, mnawakasirikia wale wanaowakosoa na kuwapiga vita?!


22. Je, hii ndiyo dini ya Allah? Je, hii ndiyo Usalafi (Salafiyyah)?


23. Je, sisi tupo kwenye Hizb na chama? Yule tunayemhesabu kuwa ni kipenzi chetu, tunakubali maneno yake hata yakiwa ya makosa. Lakini yule ambaye hatumhesabu kuwa ni kipenzi chetu, hata akituambia kwamba jambo fulani ni kosa lililo wazi kabisa, hatukubali maneno yake hata kama ni kweli. Badala yake, tunamfanyia uadui na kumpiga vita?


24. Mwishowe, mnafikia hatua ya kusema kwamba: *“Hao watakuwa Mahizbi tu....”*


25. Subhanallah! Mtu anakuaje Hizbi bila dalili wala hujja?


26. Kwa hiyo, mcheni Allah, enyi ndugu zetu. Fahamuni kwamba maneno mnayoyazungumza yanaandikwa na mtakwenda kukutana nayo mbele ya Allah na kuulizwa. Msidhani kwamba mnapambana na watu dhaifu tu. Mwenye nguvu zote ni Allah.


27. Ittaqullah juu ya ndugu zenu Masalafi, juu ya hii dini, na juu ya hawa shabab, malezi na tarbiyyah mnayowapa, hata tusipokosoa sisi ipo siku watu watajua kuwa haya ni makosa, na Alhamdulillah watu wanazidi kuamka.


28. Na Allah ni Mkali katika kuadhibu, wala haridhii dhulma. Kwa hiyo, msiwadhulumu watu, na kumbukeni dhulma haidumu.


29. Mcheni Allah! Hakika dhulma ni dhulumaat (viza) Siku ya Qiyama. Na yeyote akikosea ajirekebishe kwa manufaa yake mwenyewe na kuwahurumia shabab.


Jazakum Allahu Khayran wa Baarak Allahu Feekum.
*[B]*
*KWA NINI MNATUKASIRIKIA KWA KUKOSOA MANENO YA AIBU?*

1. Lau si ubishi wa baadhi ya ndugu zetu, wala tusingekuwa tuna haja ya kuzungumza mengi; ishara tu ingetosha na mtu akakiri kwamba haya maneno ni ya kimakosa na ya kimtaani, si ya kielimu.


2. Lakini imebidi tufanye tafsiil ya kina na kunukuu dalili na ubainifu kutoka kwa Ulamaa, nk.


3. Na kuuliza maswali mengi ambayo hayana majibu mpaka sasa


4. Kuna watu wengi mtandaoni wanasema wanataka kumuoa huyu binti wa Kisufi!! Kisha, hata haijalishi kuwa huyo bint ana mume, mnataka kumuoa tu hivyo hivyo? Subhanallah.


5. Mnaona sasa, ndugu zetu? Ni maneno ya aibu yanatuaibisha na kutushushia heshima, achilia mbali kumshambulia mpaka baba yake kuwa ni dayuthi.


6. Kweli mnawakasirikia ndugu zenu kwa sababu ya maneno haya?


Allahul Mustaa'n
*[C]* *JE, SALAFIYYAH YA MTU NI LAZIMA ITHIBITISHWE NA USTADHI FULANI?*



1. Ukienda kwenye maelezo ya Channel yetu utakuta tumejibainisha, Alhamdulillah.


2. Hawa [SDEA] ni ndugu zenu wa Kisalafi, wala si masheikh ati, na kazi yao ni kuwaunganisha watu na Ulamaa al-Kibaar na Mashayikh wakubwa wa Salafiyyah duniani, kwa sababu kuna uhitaji wa jambo hili katika miji yetu. Na hii ndio hamu yao kubwa, si kuwaunganisha watu na wao binafsi, la, na Ulamaa waki Salafi Al Hamdulillah. Na ni jambo linalomfurahisha kila mpenda haki na kila Salafi Baarak Allahu Feekum.


3. Baadhi ya Mashayikh hao wanawafahamu ndugu hawa na kuwa ni Masalafi, na wameshirikiana nao wakiratibu mihadhara, kalimat na duruus kupitia mawasiliano ya moja kwa moja kwa simu, yaani Telelinks na wao, na nyinyi si ni mashahidi wa hili? Al Hamdulillah


4. Sasa, ikiwa baadhi ya Mashayikh wakubwa wa Salafiyyah duniani wanawafahamu na kushirikiana nao, je, hilo halitoshi kuwatambulisha kuwa ni Masalafi mpaka ustadhi fulani kwetu awasifu na awakubali?


5. Kwa miaka yote ambayo ndugu hawa wamekuwa wakieneza maneno, fatwa na maelekezo na tawjihaat za Ulamaa, hawajawahi kushirikiana na watu wa bid'ah au masheikh waliopinda wala kueneza maneno yao Al Hamdulillah.


6. Pamoja na hayo yote, baadhi ya watu bado wanadai kwamba haya yote hayatoshi kuwa hawa ni Masalafi mpaka ustadhi fulani na fulani athibitishe. Subhanallah!!


7. Pia, tuleteeni maneno ya ustadhi yeyote wa Kisalafi yanayobainisha kwamba ndugu hawa si Masalafi, ili tuweze kumuuliza kwa nini amewahukumu hivyo na kwa dalili zipi.


8. Kwa hiyo, jamani, mcheni Allah na fahamuni kwamba maneno yetu yanaandikwa na tutahesabiwa kwayo. Mtume ﷺ ametahadharisha dhidi ya kumzulia Muumini jambo ambalo halipo kwake, na akaeleza kuwa mwenye kufanya hivyo Allah Atamfungia kwenye Raghdatul Khabal (pahala panapokusanyika usaha wa watu wa Motoni), na Allah Atuepeushe na hayo.


9. Tuwape faida watu wetu na tuwahurumie na tufurahi ikiwa kuna mwingine pia anafanya kazi hiyo. Si ndio Da'wah ya haki inaenea zaidi hivyo? Wala tusitake kuwakandamiza bila sababu ya kisheria.


10. Kwenye kosa tukosoeni kwa dalili, tunayakaribisha hayo. Baarakallah feekum.


Na huu ndio mwisho wa ubainifu na majibu yetu.

Tumefunga jambo hili leo, na In shaa Allah, kesho tutaendelea na ratiba zetu za kupeana faida na kukumbushana, kama tunavyofanya kila siku.

Tunamuomba Allah atuhifadhi sote, aweke mapenzi katika nyoyo zetu, ainusuru Da'wah ya Kisalafi, na awanusuru madua't wa kisalafi katika miji yetu, amuongoze yeyote miongoni mwetu anayekosea, atubariki katika juhudi zetu wote, atulipe kila kheri na atusamehe madhambi yetu na kasoro zetu.

Amiin.

*SDEA – Salafi Da'wah East Africa*