JamiiForums
✔
23.9K subscribers
40.7K photos
3.61K videos
34.7K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Mdau, hali ya usafiri wa umma kwenye eneo unaloishi ikoje? Tuambia hapa https://jamii.app/TandikaDaladala

#JamiiForums #JFMdau2026 #Uwajibikaji
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR ES SALAAM: Yanga imeingia Hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa ushindi wa Magoli 4-1 dhidi ya CFFA na kufanya matokeo ya jumla katika michezo miwili baina ya timu hizo kuwa magoli 8-1.

Mjadala unaendelea https://jamii.app/YangaButuaCFFA

#JamiiForums #JFSports
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
ITALIA: Mdau aliyejitambulisha kuwa shabiki wa Manchester United ametoa maoni kuwa anaamini ndani ya saa chache zijazo Kocha Michael Carrick anaweza kukutana na barua ya kufukuzwa kazi kutokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo katika michuano yote msimu huu.

United imefungwa magoli 4-1 na Como 1907 inayonolewa na Cesc Fàbregas katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, Oktoba 21, 2026 ikiwa ni mchezo wa saba mfululizo bila ushindi.

Mdau una maoni gani kuhusu mwenendo wa Man United?

Mjadala unaendelea https://jamii.app/ComoYaibondaManU

#JamiiForums #JFSports
PWANI: Mdau wa JamiiForums.com ameandika "Tunaomba Mamlaka za Juu kuingilia suala letu, tumefuatilia kwa ngazi tofauti lakini hatujapata utatuzi mpaka sasa."

Jitihada za kupata mrejesho kutoka Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kuhusu hoja ya Mdau zinaendelea...

Fuatilia zaidi https://jamii.app/TTCLDhuluma

#JamiiForums #Uwajibikaji #JFMdau2026
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Wakili kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (#LHRC), William Maduhu amesema hayo Oktoba 22, 2026 wakati akihojiwa kupitia Kituo cha Redio cha Wasafi FM.

Ikumbukwe, Oktoba 16, 2026, Mahakama Kuu ya Tanzania iliuagiza uongozi wa Gereza la Ukonga kuruhusu Mawakili wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu kuzungumza naye kwa usiri, huku maafisa Magereza wakikaa umbali wa kuona bila kusikia mazungumzo yao, shauri lililofunguliwa na Wakili Maduhu na wenzake.

Zaidi tembelea https://jamii.app/MaduhuLissuUkonga

#JamiiForums #Sheria
Ikumbukwe, Oktoba 7, 2026 kupita JamiiForums.com, Mdau aliandika “Matokeo ya CBE Dodoma Mwaka 2018/19 na 2019/20 hayajawekwa kwenye Mfumo wa NACTVET, aliyehitimu miaka hiyo akirudi chuoni kuendelea na masomo, anaambiwa matokeo yake bado hayapo NACTVET.

Zaidi https://jamii.app/CBETamko
UFARANSA: Rais wa Bunge la Ulaya, Roberta Metsola amesema tuzo hiyo inatambua mchango wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (#ICC) katika kusimamia Haki za Kimataifa. Tuzo ya Sakharov ilianzishwa Mwaka 1988, huku hafla ya mwaka huu ikipangwa kufanyika Desemba 16, 2026, mjini Strasbourg.

Zaidi tembelea https://jamii.app/IccYatwaaSakharov

#JamiiForums #Diplomasia #TuzoYaSakharov2026 #Governance #Accountability
Moja ya Mjadala unaoendelea ndani ya JamiiForums.com

Fuatilia zaidi https://jamii.app/NambaWakopeshaji

#JamiiForums #JFMdau2026
DAR: Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar, leo Oktoba 22, 2026 imetupilia mbali ombi la Said Issa Mohammed na mwenzake, ikisema haioni sababu za msingi za kuzuia shughuli za kisiasa za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kama wafungua maombi walivyokuwa wanaomba.

Itakumbukwa awali, Mei 28, 2026 Mahakama Kuu ilitupilia mbali kesi kama hiyo iliyofunguliwa na Said Issa, Rashid na Maulida Anna Komu (marehemu) ikiwa na madai ya aina hiyo.

Uamuzi ambao umetolewa leo umetokana na maombi kwenye shauri la msingi la kuiomba Mahakama Kuu kuichukulia hatua CHADEMA kwa kudai haitoi mgawanyo wa mali ulio sawa upande wa Zanzibar.Hivyo, CHADEMA itaendelea kufanya shughuli zake wakati shauri la msingi likiendelea.

Zaidi https://jamii.app/CHADEMAKesi

#JamiiForums #Siasa
Please open Telegram to view this post
VIEW IN TELEGRAM