AFRIKA KUSINI: Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Umma, imemwondoa Rais #CyrilRamaphosa katika kashfa ya kuficha Tsh. Bilioni 9.3 kwenye mashamba yake ya Phala Phala baada ya kubaini aliwajibika kutangaza maslahi yake katika mashamba hayo na kuripoti Polisi
Februari 9, 2020, Watu 2 waliingia #PhalaPhala na kuiba zaidi ya Tsh. Bilioni 1.3 zilizofichwa kwenye mito ya Sofa. Ramaphosa alidai fedha hizo zilikuwa ni mauzo ya Nyati kutoka katika shamba hilo
Soma https://jamii.app/CyrilCleared
#Governance #Acountability

π13
BRAZIL: Mahakama ya Juu imetoa kibali cha uchunguzi wa Akaunti za Benki na Nyaraka za Kodi za Aliyekuwa Rais, #JairBolsonaro, kutokana na tuhuma zilizoibuliwa kuwa alifanya Ubadhirifu wa Fedha na kuuza Madini na Zawadi alizopokea kwa niaba ya Serikali
Bolsonaro aliondoka Brazil siku mbili kabla ya kumaliza muhula wake, akipuuza kuapishwa kwa mrithi wake Luiz Inacio Lula da Silva aliyeshinda Urais Mwaka 2022. Pia, anachunguzwa kwa kudaiwa kuhamasisha Wafuasi wake kuvamia makazi ya Rais.
Soma https://jamii.app/BrazilPrezo
#JamiiForums #Goernance #Acountability #Democracy

π3
MDAU MASASI: Anadai Uongozi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Masasi - Nachingwea (MANAWASA) unaendesha Taasisi kama Mali binafsi na kufanya vitu vingi kinyume na taratibu za Kazi
Baadhi ya changamoto anazotaja ni kutolipwa stahiki kama vile muda wa ziada na nauli za likizo, kutopatiwa muda wa mafunzo wakiambiwa βmafunzo si haki kwa Watumishiβ, baadhi ya Watumishi kusitishiwa Ajira bila kuzingatia Kanuni za Utumishi na kukosa uhusiano mzuri kati ya Uongozi na Watumishi wa chini
Aidha, anadai baadhi ya Watumishi wapo kwenye adhabu za kinidhamu lakini wamepandishiwa Mishahara.
Soma https://jamii.app/Manawasa
#JFUwajibikaji23 #Governance #JFHuduma #JamiiForums #Acountability

π5
#KENYA: Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Kenya, Githu Muigai amesema Bunge la Nchi hiyo lina idadi kubwa ya Wabunge ambao wanaongeza mzigo wa gharama kwa Walipa Kodi, hivyo ufanyike utaratibu wa kuwapunguza
Pia, Muigai amesema Uwiano wa Theluthi Mbili wa nafasi za Wanawake Bungeni unapaswa kutupiliwa mbali na badala yake kuwe na Uwakilishi wa 50/50
Wakati idadi ya Wabunge wa Kenya ikiwa ni 349, Bunge la Tanzania lina Wabunge 393 kutoka 357 waliokuwepo Mwaka 2010. Ongezeko hilo lilitokana na kuongezwa kwa Majimbo ya Uchaguzi
Soma https://jamii.app/IdadiWabunge
#JamiiForums #Governance #Democracy #Acountability #SocialJustice

π4
#UCHUMI: Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) imesema Ukuaji wa Uchumi wa Bara la Afrika kwa Mwaka 2023 ulishuka hadi kufikia 3.2% kutoka 4.1% ya Mwaka 2022
AfDB imefafanua kuwa hali hiyo imechangiwa na kutokuwa na utulivu wa Kisiasa kwenye baadhi ya Mataifa, Kudorora kwa Uchumi wa China, Athari za UVIKO-19 pamoja na Vita ya Urusi na Ukraine
Hata hivyo, Ukuaji wa jumla wa Pato la Taifa (GDP) kwa Bara la Afrika unatarajiwa kuwa kati ya wastani wa 3.8% Mwaka 2024 na 4.2% Mwaka 2025. Pia, Afrika inatazamiwa kuwa eneo la pili kwa ukuaji wa kasi wa Uchumi ikilifuatia Bara la Asia
Soma https://jamii.app/AfDBForecast
#JamiiForums #AfricanEconomy #Governance #Acountability #AfricanPolitics #EconomyCrisis #JFSC

π4β€1
UCHUMI: RWANDA KUONGOZA KWA KASI YA UKUAJI WA UCHUMI AFRIKA MASHARIKI MWAKA 2024
Ripoti ya Ukuaji wa Uchumi iliyotolewa na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) inaeleza kati ya Nchi 20 zitakazokuwa na Ukuaji wa Kasi ya Uchumi Duniani kote kwa Mwaka 2024, Nchi 11 zitatoka Barani Afrika
Kanda ya Afrika Mashariki imetajwa kuwa itaendelea kuongoza Ukuaji wa #Uchumi katika Kanda zote za Afrika ikiwa na Ukuaji wa kiwango cha 5.1% kwa Mwaka 2024 huku ikitarajiwa kufikia 5.7% Mwaka 2025
Nchi 3 za Afrika Mashariki zimetajwa katika orodha hiyo ambapo zitaongozwa na #Rwanda inayotarajiwa kupata Ukuaji wa 7.2% ikifuatiwa na Tanzania 6.1% na Uganda itakayokuwa na Ukuaji wa Uchumi wa 6%
Soma https://jamii.app/AfDB2024
#JamiiForums #AfricanEconomy #Governance #Acountability #AfricanPolitics #JFSC #JFDATA

π3β€1π1
KENYA; Rais William Ruto amewataka wanaosababisha machafuko kwa kufadhili watu kufanya vurugu nchini humo wajitokeze hadharani na washauri Serikali ifanye nini ili kuondokana na hali iliyopo
Akizungumza baada ya Ibada ya Jumapili, Ruto amesema "Wale wanaofadhili, kuandaa na kufadhili ghasia hizi wajitokeze na kutupa maoni yao ya kipekee kuhusu jinsi ya kuipeleka #Kenya mbele. Wasibaki bila kujulikana, wajitokeze"
Ameongeza "Nataka kuahidi, hali hii itakoma, imetosha sasa. Tutalinda maisha, tutalinda mali, tutawakomesha waporaji, tutawakomesha wauaji, tutakomesha ghasia, tunataka taifa lenye amani na utulivu. Masuala yetu yanatatuliwa kwa njia za Kidemokrasia,β
Kauli za Ruto zinakuja wakati Vijana wa Gen Z wametangaza kufanya Maandamano katika Jiji la Nairobi Julai 23, 2024 wakimtaka Rais kuwaondoa Mawaziri 6 waliorejeshwa katika uteuzi wa Baraza jipya.
Soma https://jamii.app/RutoVsWafadhili
#JamiiForums #Governance #Democracy #Acountability #CivilRights