JamiiForums
βœ”
23.9K subscribers
40.7K photos
3.61K videos
34.7K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Mdau wa JamiiForums.com kutoka Mbezi Luis amelalamikia hali ya Barabara inayopita katika eneo la Mpiji Magohe ambayo imekuwa mbovu kwa muda mrefu licha ya kufikisha kero kwa wahusika ikiwemo Ofisi ya Serikali ya Mtaa

Anadai Barabara hiyo ambayo kama ikijengwa vizuri inaweza kupunguza foleni za maeneo mengi lakini kutokana na ubovu imefanya watu wamekuwa wakitumia muda mwingi Barabarani

Mdau anadai baadhi ya Wanasiasa na Viongozi wamekuwa wakitoa ahadi zisizo na utekelezaji kuhusu ukarabati wa Barabara hiyo na kwa sasa wanaomba Serikali isikie shida zao na kutatua kero hiyo kwa haraka

Soma https://jamii.app/MdauMpiji

#JamiiForums #JFHuduma #SocialJustice #Governance #ServiceDelivery #JFSC
πŸ‘1
BULGARIA: Wakulima wakubwa na Wadogo wameandamana kwa siku ya pili walishinikiza Serikali kuweka Uongozi unaowajibika pamoja na kuongezwa kwa Fedha za Ruzuku ya Kilimo nchini humo

Kamati ya Mipango ya Wakulima hao imesema Umoja huo hautasitisha Maandamano hayo hadi Waziri wa Kilimo, Kiril Videev atakapojiuzulu huku wakitishia kufunga maeneo muhimu ya kuingia Mjini ikiwemo kumwaga maelfu ya Lita za Maziwa Barabarani

Pia, Wakulima hao wamedai kuwa endapo Serikali ikipuuza matakwa yao ikiwa ni pamoja na kuzuia uagizwaji wa Ngano kutoka Ukraine, kuanzia Wiki ijayo wataingiza Mifugo katikati ya Majiji yote

Soma https://jamii.app/FarmersBLG

#JamiiForums #SocialJustice #Accountability #FoodSecurity #JFSC
πŸ‘4
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
#BUNGENI: Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema ni kweli Nchi ina upungufu wa Sukari kutokana na kuwepo kwa Mvua nyingi kwenye maeneo ya Mashamba ya Miwa inayozalisha Sukari, ambapo Maji yamejaa na kusababisha Wakulima kushindwa kutoa Miwa na kupeleka Viwandani

Akijibu swali la Mhandisi Stella Manyanya, Mbunge wa Mbambabay, Waziri Mkuu amesema upungufu huo umeshaanza kufanyiwa kazi na Serikali ikiwemo kuruhusu uagizaji wa Sukari zaidi ya Tani 100,000 ambazo zimeshaanza kuwasili Nchini

Bado Mtaani kumekuwa na malalamiko ya Wananchi kuuziwa Sukari kwa bei kati ya Tsh. 4000 hadi 6000 ikiwa ni zaidi ya Bei Elekezi ya Serikali inayotaka Sukari iuzwe kati ya Tsh. 2,700 hadi 3,200 kwa Kilo 1.

Soma https://jamii.app/BungeniSukari

#JamiiForums #Governance #Accountability #JFHuduma #SugarScarcity #JFSC
πŸ‘8❀1
GHANA: Serikali imesitisha mipango ya Ukusanyaji wa Kodi ya 15% kwenye Huduma ya Umeme kufuatia malalamiko na tishio la Maandamano ya Wananchi juu ya kuongezeka kwa Gharama za Maisha

Kodi hiyo ilitarajiwa kuanza kukusanywa kwa shinikizo kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) linalotaka Serikali kuongeza vyanzo vya Kodi ili kulipa Madeni ya zaidi ya Tsh. Trilioni 7.57 kutoka Shirika hilo

Nchi hiyo imekuwa ikitegemea Umeme unaozalishwa kwa Maji na Mafuta huku ikidaiwa kushindwa kufanya ukarabati wa Mitambo yake, ambapo hivi karibuni ilianza kutumia Gesi

Soma https://jamii.app/UmemeGH

#JamiiForums #Governance #Accountability #JFHuduma #EconomyCrisis #SocialJustice #JFSC
πŸ‘7
#LIBERIA: Waziri wa Ulinzi, Prince Charles Johnson III amejiuzulu baada ya Wake wa Maafisa wa Jeshi kuandamana kwa malalamiko ya Waume zao kutoongezewa Mshahara huku wakiishi Maisha duni katika Kambi za Kijeshi

Wanawake hao waliandamana na kuweka Vizuizi kwenye Barabara zinazoingia katika Jiji la #Monrovia na maeneo mengi ya Nchi wakishinikiza Rais #JosephBoakai kusitisha Sherehe za Kitaifa za Jeshi huku wakimtuhumu Waziri huyo kufuja Fedha za Wanajeshi wanaorejea kutoka Vitani

Pia, wamedai Wanajeshi wamekuwa na hali mbaya kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, Kutokuwepo kwa Umeme wa Uhakika kwenye Makazi yao pamoja na ongezeko la Rushwa miongoni mwa Vikosi vya Jeshi

Soma https://jamii.app/LiberiaCS

#JamiiForums #SocialJustice #Governance #Accountability #JFSC
πŸ‘4❀3😁2
Mdau wa JamiiForums.com amehoji sababu za uwepo wa Magari mengi kila kunapokuwa na misafara ya Viongozi mbalimbali nchini, kitendo anachodai kinaongeza mzigo wa gharama kwa Walipa Kodi pamoja na usumbufu mkubwa kwa Watumiaji Barabara ambao husubirishwa kwenye foleni ili kupisha wingi wa Magari hayo

Changamoto gani huwa unazipata kukiwa na Misafara ya Viongozi katika eneo lako?

Soma https://jamii.app/MisafaraTZA

#JamiiForums #Governance #Accountability #JFSC
πŸ‘3❀2
#UCHUMI: Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) imesema Ukuaji wa Uchumi wa Bara la Afrika kwa Mwaka 2023 ulishuka hadi kufikia 3.2% kutoka 4.1% ya Mwaka 2022

AfDB imefafanua kuwa hali hiyo imechangiwa na kutokuwa na utulivu wa Kisiasa kwenye baadhi ya Mataifa, Kudorora kwa Uchumi wa China, Athari za UVIKO-19 pamoja na Vita ya Urusi na Ukraine

Hata hivyo, Ukuaji wa jumla wa Pato la Taifa (GDP) kwa Bara la Afrika unatarajiwa kuwa kati ya wastani wa 3.8% Mwaka 2024 na 4.2% Mwaka 2025. Pia, Afrika inatazamiwa kuwa eneo la pili kwa ukuaji wa kasi wa Uchumi ikilifuatia Bara la Asia

Soma https://jamii.app/AfDBForecast

#JamiiForums #AfricanEconomy #Governance #Acountability #AfricanPolitics #EconomyCrisis #JFSC
πŸ‘4❀1
UCHUMI: RWANDA KUONGOZA KWA KASI YA UKUAJI WA UCHUMI AFRIKA MASHARIKI MWAKA 2024

Ripoti ya Ukuaji wa Uchumi iliyotolewa na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) inaeleza kati ya Nchi 20 zitakazokuwa na Ukuaji wa Kasi ya Uchumi Duniani kote kwa Mwaka 2024, Nchi 11 zitatoka Barani Afrika

Kanda ya Afrika Mashariki imetajwa kuwa itaendelea kuongoza Ukuaji wa #Uchumi katika Kanda zote za Afrika ikiwa na Ukuaji wa kiwango cha 5.1% kwa Mwaka 2024 huku ikitarajiwa kufikia 5.7% Mwaka 2025

Nchi 3 za Afrika Mashariki zimetajwa katika orodha hiyo ambapo zitaongozwa na #Rwanda inayotarajiwa kupata Ukuaji wa 7.2% ikifuatiwa na Tanzania 6.1% na Uganda itakayokuwa na Ukuaji wa Uchumi wa 6%

Soma https://jamii.app/AfDB2024

#JamiiForums #AfricanEconomy #Governance #Acountability #AfricanPolitics #JFSC #JFDATA
πŸ‘3❀1πŸ‘Ž1
Mdau wa JamiiForums.com kutoka Mitaa ya Tabata Segerea, ameilalamikia Mamlaka ya Majisafi na Uhifadhi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kutokana na kukosekana kwa huduma ya Maji kwa takriban Wiki 3 katika Mitaa hiyo

Mdau anasema hata wanapojaribu kuripoti tatizo hilo kwenye Kurasa za Mitandao ya Kijamii za DAWASA hawajibiwi, na wengine wanaofika katika Ofisi zao zilizopo Tabata-Chama, wanapewa majibu kuwa tatizo linashughulikiwa ndani ya muda mfupi lakini hakuna mabadiliko wanayopata

Soma https://jamii.app/SegereaMaji

#JamiiForums #SocialJustice #Governance #JFHuduma #ServiceDelivery #JFSC
πŸ‘4❀1
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imesema kuwa msukumo mdogo wa Maji uliosababishwa na changamoto za Umeme, umechangia baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar kutopata Maji ikiwemo Kinyerezi na Bonyokwa

Ufafanuzi huo umetolewa baada ya Mdau wa JamiiForums.com kudai maeneo ya Tabata Segerea kuna changamoto ya Maji kwa zaidi ya wiki, hali inayofanya Wakazi kulazimika kununua Maji ya Visima huku malalamiko yao yakiwa hayafanyiwi kazi licha ya kuripoti katika Ofisi na Mitandao ya DAWASA

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa DAWASA, Everlasting Lyaro amesema β€œKinyerezi wanatumia pump ya Segerea, wanaendelea kupata huduma kwa Mgawo lakini Wataalamu wetu wanafuatilia na kinachofanyika kwa sasa ni kuongeza msukumo Bonyokwa.”

Soma https://jamii.app/MajiSegerea

#JamiiForums #SocialJustice #Governance #JFHuduma #ServiceDelivery #JFSC
πŸ‘1
#UCHUMI: Serikali ya Tanzania imetia saini Mkataba wa Tsh. Bilioni 988.098 kutoka Benki ya Dunia (WB), Fedha zitakazotumika kutekeleza Awamu ya 2 ya Mradi wa Miundombinu ya Jiji la Dar es Salaam (DMDP II)

Akizungumza mbele ya Mkurugenzi Mkazi wa WB, Nathan Belete, Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba ametaja maeneo yatakayofanyiwa Uboreshaji wa Miundombinu ni Ilala, Temeke na Kinondoni, Ubungo na Kigamboni

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Fedha, Awamu ya Kwanza ya DMDP iliyokamilika Mwaka 2023, Benki ya Dunia ilitoa Dola Milioni 300 (Tsh. Bilioni 760.5 zilizojenga Kilomita 207 za Barabara, Vituo 4 vya Mabasi, Kilomita 75 za Mfumo wa Maji na Mabwawa 3 ya kuzuia Mafuriko

Soma https://jamii.app/DMDPII

#JamiiForums #Governance #Economy #Accountability #JFSC
πŸ‘2
KENYA: Mahakama Kuu imetoa uamuzi kuhusu Haki za Msingi za Wafungwa katika Maisha ya kawaida na kuamuru Wafungwa wote Nchini humo wanapaswa kupewa Haki kama Binadamu wengine ikiwemo Haki ya kuhudhuria Mazishi

Mahakama imetoa uamuzi huo kupitia Kesi iliyofunguliwa na Mwandishi wa Habari Moses Dola Otieno, ambaye anatumikia Kifungo Jela baada ya kukutwa na hatia ya Kumuua Mke wake

Katika madai yake, Mwandishi huyo aliwashutumu Wakuu wa Magereza kwa kuwakatalia Wafungwa kuhudhuria mazishi ya wapendwa wao akieleza suala hilo liko kinyume na Haki za Binadamu

Soma https://jamii.app/MazishiKE

#JamiiForums #Governance #SocialJustice #JFSC
πŸ‘5
UCHUMI: Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) imesema kuendelea kupanda kwa gharama za maisha hasa mahitaji muhimu kama Chakula, Nishati na bidhaa nyingine kunaweza kuibua hasira za Wananchi na kusababisha vurugu katika baadhi ya Mataifa ya Afrika

#AfDB imezitaja baadhi ya Nchi zinazopaswa kuchukua hatua za haraka kushughulikia masuala hayo ni #Angola, #Ethiopia na #Kenya huku #Nigeria ikiwa tayari imeanza kushuhudia kukosekana kwa utulivu kutokana na gharama kubwa za maisha

Pia, imeelezwa kuendelea kushuka kwa thamani ya Sarafu za Fedha dhidi ya Dola ya Marekani katika Nchi nyingi za Afrika kutaongeza Bei za Vyakula kwa Mwaka 2024, hali inayoweza kuchochea madai ya mabadiliko ya Kiserikali

Soma https://jamii.app/AfDBForecasts

#JamiiForums #Governance #AfricanEconomy #Accountability #EconomyCrisis #SocialJustice #JFSC
πŸ‘8❀1
#UCHUMI: Serikali kupitia Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Elijah Mwandumbya amesema Tanzania ni kati ya Nchi chache zenye viwango vizuri vya kuendelea kukopeshwa kutokana na kuthibitishwa na Taasisi za Kimataifa za Tathmini za Moody's na Fitch

Akizungumza katika Mkutano uliojadili Viwango vya Riba za Mikopo katika Nchi za Afrika uliofanyika Zimbabwe, amesema Madeni ya Nchi nyingi za Afrika yanakua kwa kasi kutokana na kuongezeka kwa viwango vya Kubadilisha Fedha Duniani na Riba, hali inayosababisha kushuka kwa thamani ya fedha za ndani

Aidha, ameongeza kushuka kwa thamani ya Fedha za ndani dhidi ya Dola katika Nchi za Afrika, kumeendelea kusababisha viwango vikubwa vya Riba vinavyoathiri uhudumiaji wa Madeni, huku Nchi nyingine zikishindwa kukusanya mapato ya kutosha

Soma https://jamii.app/Kukopesheka

#JamiiForums #Governance #AfricaEconomy #Accountability #JFSC
πŸ€”2πŸ‘1
LIBERIA: Rais #JosephBoakai ametangaza kuunda Kikosi Kazi kitakachokuwa na jukumu la Kukabiliana na Vitendo vya #Rushwa pamoja na kurejesha Mali za Serikali zilizoibwa kifisadi

Rais Boakai ameagiza Kikosi hicho kumtafuta Afisa wa ngazi yoyote aliyehusika na Rushwa katika Serikali zilizopita na Serikali ya sasa pamoja na kuanza uchunguzi dhidi ya tuhuma zitakazobainika

Aidha, Rais amesema Mali zote za Serikali zilizouzwa na kununuliwa kinyume na utaratibu zirejeshwe haraka. Uamuzi huo unakuja ikiwa ni Siku 44 tangu aingie Madarakani.

Soma https://jamii.app/TaskForceLBR

#JamiiForums #Governance #Accountability #JFSC
❀4πŸ‘3
UCHUMI: Serikali ya Mapinduzi #Zanzibar imetangaza bei elekezi ya Sukari kwa lengo la kupunguza gharama za maisha katika kipindi cha Mfungo wa Mwezi wa Ramadhani

Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Omar Said Shaaban amesema Kilo 1 ya Sukari itauzwa kwa TSh. 2,650 kwa Unguja na TSh. 2,700 kwa kilo kwa upande wa Pemba. Awali, Bei ya Rejareja ya Sukari ilikuwa Tsh. 3,200

Soma https://jamii.app/SukariZNZ

#JamiiForums #Governance #JFHuduma #ServiceDelivery #JFSC
πŸ‘2❀1
#UCHUMI: Serikali ya #Tanzania imesema inatarajia kukusanya na kutumia Tsh. Trilioni 49.34 katika Mwaka 2024/25 ambapo kati ya Fedha hizo, Tsh. Trilioni 6.61 zitakopwa kutoka Soko la Ndani na Tsh. Trilioni 2.98 zitakopwa kutoka katika Soko la Nje

Wizara ya Fedha imeeleza kuwa katika mipango ya Matumizi, Tsh. Trilioni 33.55 zitatumika kwa Matumizi ya Kawaida na Tsh. Trilioni 15.79 zitatumika kwenye Miradi ya Maendeleo ikiwemo Kilimo, Elimu, Barabara, Maji, Umeme, Afya na ukamilishaji wa Bwawa la Nyerere (JNHPP)

Aidha, Serikali inatarajia kutumia Tsh. Bilioni 200 katika maandalizi ya Kombe la Mataifa ya Afrika (#AFCON) 2027, Tsh. Bilioni 900 zitagharamia chaguzi za Mwaka 2024 na 2025 ambapo Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 utatumia Tsh. Bilioni 300 na Uchaguzi Mkuu 2025 utagharimu Tsh. Bilioni 600

Soma https://jamii.app/BajetiTZA

#JamiiForums #Governance #Accountability #Economy #TanzaniaBudget #JFSC #JFDATA
πŸ‘3
NIGERIA: Rais Bola Tinubu amepiga marufuku safari zote za Nje za Viongozi kwa muda wa miezi mitatu kuanzia Aprili 1, 2024, lengo likitajwa kuwa ni mpango wa kubana na kupunguza Matumizi ya Serikali yasiyo na ulazima

Hatua ya Rais inafuatia uwepo wa malalamiko ya Wananchi wanaodai Serikali imekuwa na matumizi makubwa ya Fedha za Walipa Kodi yasiyo na tija, zikiwemo Safari za Mfululizo za Viongozi akiwemo Rais aliyefanya safari 15 kwenda nje ya nchi tangu alipoapishwa Mei 29, 2023

Hii ni mara ya pili kwa Rais Tinubu kuchukua maamuzi ya kudhibiti matumizi ya Serikali ambapo Januari 2024 alitangaza kupunguza kwa 60% idadi ya Watu wanaokuwa kwenye Misafara ya Viongozi akiwemo yeye mwenyewe. Hata hivyo Tinubu hajaweka wazi kama safari zake pia zitasitishwa.

Soma https://jamii.app/TripsBanNGR

#JamiiForums #Governance #Accountability #AfricanEconomy #JFSC
πŸ‘7❀1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
#BUNGENI: Ripoti 21 za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) zinazohusu Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka 2022/2023 zimewasilishwa Bungeni leo baada ya tukio la kukabidhiwa kwa Rais, Machi 28, 2024

Miongoni mwa Ripoti hizo ni pamoja na Ukaguzi wa Taarifa za Fedha za Serikali Kuu, Taarifa za Fedha za Mamlaka za Serikali za Mitaa na Taarifa za Fedha za Miradi ya Maendeleo

Awali akiwasilisha Ripoti hizo kwa Rais Samia, CAG Kichere alisema Ukaguzi umebaini baadhi ya Mashirika ya Umma yakiwemo Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Kampuni ya Mawasiliano Tanzania (TTCL), Shirika la Reli Tanzania (TRC), Kampuni ya Uwekezaji (TANOIL) na Shirika la Posta Tanzania yamepata hasara.

Soma https://jamii.app/CAGReports24

#JamiiForums #Governance #RipotiYaCAG24 #Accountability #JFSC
❀1πŸ‘1