JamiiForums
✔
23.9K subscribers
40.7K photos
3.61K videos
34.7K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MADHARA YA ‘ENERGY DRINKS’

Vinywaji vya kuongeza nguvu ‘Energy Drinks’ vinachangamsha mwili na akili lakini vinaweza kusababisha Shambulio la Moyo, Uraibu na Kisukari

> Inashauriwa kusoma maelekezo kabla ya kutumia

Soma - https://jamii.app/VinywajiVyaNguvu

#FoodSecurity #JFAfya
👍20😢3👎2👏2😁2🔥1😱1
MAUZO YA NAFAKA: UKRAINE NA URUSI ZASAINI MAKUBALIANO

Ni makubaliano ya kuruhusu mauzo ya nafaka kutoka Bandari ya Bahari Nyeusi ya Ukraine yanayolenga kupunguza uhaba wa Chakula duniani

Vita ilisababisha Bandari kufungwa na kukwamisha usafirishaji

Soma https://jamii.app/RussiaUkraineWar

#FoodSecurity
😁11👍5
#TEKNOLOJIA: #Niger imeanza kutengeneza Mvua kwa Teknolojia ya kutumia Ndege kunyunyiza Kemikali kwenye Mawingu ili kupunguza athari za Ukame Nchini humo

Lengo ni kuongeza uzalishaji wa Vyakula baada ya kukabiliwa na vipindi virefu vya Ukame

Soma https://jamii.app/NigerMvua

#FoodSecurity
👍8🥰3
#AFGHANISTAN: Umoja wa Mataifa umebainisha kwamba Raia Milioni 6 wako hatarini kukabiliwa na Njaa, huku milioni 19 wakiwa na upungufu mkubwa wa Chakula

Watoto milioni 3 wana Utapiamlo huku milioni 1 Kati yao wakiwa hatarini kufariki

Soma https://jamii.app/NjaaAfghan

#FoodSecurity
👍5
TANZANIA YASITISHA VIBALI VYA KUSAFIRISHA MAHINDI KWA WAFANYABIASHARA WA #KENYA

Lengo ni kujilinda dhidi ya baa la njaa kwa kulinda Akiba ya Chakula kutokana na Mavuno Duni na Ukame

#Tanzania ndiye msafirishaji mkubwa wa Mahindi Nchini Kenya

Soma - https://jamii.app/MaizeExports

#FoodSecurity
👍19😁2
IGAD: WATU MILIONI 51 AFRIKA MASHARIKI HAWANA UHAKIKA WA CHAKULA

Pia, ripoti hiyo ya Shirikisho la Maendeleo Afrika (IGAD) imeonesha kuwa Watoto milioni 10 wana Utapiamlo

> Zaidi ya Watu 380,000 wako hatarini kufa kwa njaa

Soma https://jamii.app/IGADFood

#FoodSecurity
👍5
#JFDATA: Wakati baadhi ya maeneo Nchini yakikabiliwa na Upungufu wa Chakula, ikiwa ni pamoja na kupanda kwa Bei ya Mazao ya Nafaka, 75.5% ya Ardhi inayofaa Nchini bado haijatumika kwa #Kilimo

Halmashauri 17 katika Mikoa 8 zimetajwa kukabiliwa na upungufu wa #Chakula kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo Ukame, Wanyama Pori, Ndege aina ya Kweleakwelea na Viwavi Jeshi

Soma https://jamii.app/KilimoTZ

#JFUwajibikaji23 #FoodSecurity #FoodSafety
👍6
NBS: TUTAENDELEA KUWA NA MFUMUKO WA BEI STAHIMILIVU HADI MACHI 2023

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), imesema Mfumuko wa Bei za Vyakula utapungua kutoka 9.7% ya Desemba 2022 hadi 8.4% ifikapo Machi 2023. Pia, Mfumuko huo bado ni Himilivu kwa kuwa uko kwenye Tarakimu 1

Je, Bei ya Mchele, Mahindi na Maharage ikoje mtaani kwako?

Soma https://jamii.app/BeiVyakula

#JFGovernance #JFDATA #JFUwajibikaji23 #FoodSecurity
👍5🤔3
RIPOTI: Ripoti mpya iliyotolewa na Taasisi ya Kenya #FoodSecuritySteering imeonesha idadi ya Wananchi walioathirika na Ukame inazidi Watu Milioni 6 kutoka Milioni 4.2 iliyoripotiwa Julai 2022

Zaidi ya Watoto 970,000 wenye Miaka chini ya 5 na akina Mama Wajawazito na Wanaonyonyesha wapatao 142,000 wanahitaji Matibabu ya haraka ili kudhibiti Utapiamlo

Soma https://jamii.app/UkameKE

#Governance #FoodSecurity #ClimateChange
RIPOTI: Mamlaka ya Maendeleo baina ya Serikali za #AfrikaMashariki, (IGAD) imesema eneo kubwa la Pembe ya Afrika linatarajiwa kukumbwa na Mzozo wa Kiuchumi zaidi kutokana na Ukame utakaoendelea kwa msimu wa 6 mfululizo

Nchi za Ethiopia, #Kenya, na Somalia zinatarajiwa kupata Mvua chini ya kiwango, huku baadhi ya maeneo ya #Uganda, Sudan Kusini, #Rwanda, Burundi, #Tanzania, na yakitajwa kukumbwa na tatizo hilo

Soma https://jamii.app/ChacoF63

#Governance #FoodSecurity
👍3
Utafiti mpya wa Shirika la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF) umeonesha dunia inakabiliwa na ongezeko kubwa la Wanawake Wajawazito, Wanaonyonyesha na Wasichana walioathiriwa na Uhaba wa Chakula na #LisheDuni

Watoto Milioni 51 wenye chini ya miaka 2 wanakabiliwa na Udumavu kutokana na #Utapiamlo, Nusu yao hudumaa wakati wa Ujauzito na Miezi 6 ya kwanza

Je, Unachukua hatua gani kuepusha Jamii yako kuathiriwa na #Utapiamlo?

Soma https://jamii.app/UNICEF

#FoodSecurity #Governance
👍1
Siku ya Chakula Duniani huadhimishwa Oktoba 16 kila Mwaka ikiwa ni kumbukumbu ya kuanzishwa kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) Mwaka 1945

Kupitia Siku ya Chakula Duniani, juhudi za pamoja hufanywa kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDG's) ambayo ni pamoja na kumaliza Njaa, kufikia usalama wa Chakula, kuboresha Lishe, na kukuza Kilimo endelevu ifikapo Mwaka 2030

Soma https://jamii.app/WorldFoodDay2023

#JamiiForums #WorldFoodDay2023 #FoodSecurity #HumanRights
👍3
BULGARIA: Wakulima wakubwa na Wadogo wameandamana kwa siku ya pili walishinikiza Serikali kuweka Uongozi unaowajibika pamoja na kuongezwa kwa Fedha za Ruzuku ya Kilimo nchini humo

Kamati ya Mipango ya Wakulima hao imesema Umoja huo hautasitisha Maandamano hayo hadi Waziri wa Kilimo, Kiril Videev atakapojiuzulu huku wakitishia kufunga maeneo muhimu ya kuingia Mjini ikiwemo kumwaga maelfu ya Lita za Maziwa Barabarani

Pia, Wakulima hao wamedai kuwa endapo Serikali ikipuuza matakwa yao ikiwa ni pamoja na kuzuia uagizwaji wa Ngano kutoka Ukraine, kuanzia Wiki ijayo wataingiza Mifugo katikati ya Majiji yote

Soma https://jamii.app/FarmersBLG

#JamiiForums #SocialJustice #Accountability #FoodSecurity #JFSC
👍4
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limesema Mchele, Mafuta ya kupikia ya Alizeti na Maharage ambavyo vimeongezwa Virutubisho vilivyotolewa na Wizara ya Kilimo ya Marekani kwa ushirikiano na Taasisi ya Jumuiya za Kimataifa (Global Communities) kwa baadhi ya Shule za Dodoma, vyote ni salama kwa Walaji

TBS imesema taratibu za uingizwaji wa chakula Nchini zilifuatwa ikiwemo ukaguzi na uchunguzi wa Kimaabara

Meneja Uhusiano na Masoko wa TBS, Gladness Kaseka amesema "Utaratibu wa kuongeza virutubisho kwenye chakula (food fortification) unakubalika kitaalamu na hufanyika kwa lengo la kuboresha hali ya lishe kwa walaji."

Siku chache zilizopita Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alisema Taasisi hiyo ya Marekani inunue vyakula kutoka kwa Wakulima wa Tanzania na Virutubisho viwekwe huku Watanzania wakishuhudia

Soma https://jamii.app/TBSChakula

#Diplomacy #Governance #FoodSecurity #JamiiForums
👍5
Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema kutokana na ukame unaoikumba Nchi ya #Zambia, Serikali ya Nchi hiyo imeingia makubaliano na #Tanzania kununua Tani 650,000 za Mahindi kwaajili ya kusaidia takriban Watu 7,000,000 nchini humo

Amesema Mkataba huo utatekelezwa kwa kipindi cha Miezi 8 na utaiingizia Tanzania Dola Milioni 250 (zaidi ya Tsh. Bilioni 650) na kuwa Mahindi hayo yatatolewa katika maghala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ambapo kituo cha Songwe kitauza Tani 55,000, Makambako Tani 75,000, Sumbawanga Tani 250,000 na Songea Tani 270,000

Soma https://jamii.app/TZZambiaMahindi

#JFDiplomacy #Governance #FoodSecurity #ServiceDelivery #JamiiForums
👍2❤1
RIPOTI: Imeelezwa kuwa kati ya Mwaka 2023 hadi 2024, Watu Milioni 1.9 wameongezeka katika idadi ya Watu wanaokabiliwa na Hali Mbaya ya Upatikanaji wa Chakula duniani kutoka Watu 705,000 walioongezeka mwaka 2022/23

Kwa mujibu wa Ripoti mpya ya Kimataifa ya Migogoro ya Chakula (GRFC), ongezeko hilo limechangiwa zaidi na Mvua za El Niño na hali mbaya ya Usalama inayoendelea katika maeneo ya Gaza na Sudan

Aidha, Nchi 10 zikiwemo 4 za Afrika (DR-Congo, Nigeria, Sudan na Ethipia) kati ya 59 zilizofanyiwa tathmini zimeonesha hadi kufikia Desemba 2023, zilikuwa na Watu Milioni 281.58 ambao hawana uhakika wa kupata Chakula, kati yao Watoto ni Milioni 72.8

Soma https://jamii.app/GRFC2024

#JamiiForums #Governance #HumanRights #FoodSecurity #ChildRights #ClimateChange #JFDATA
👍1
Kwa mujibu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) uagizaji wa chakula kutoka nje ya Afrika unazidi kuongezeka kuanzia mwaka 2023 kwa takriban mara tatu kutoka kutumia Dola Bilioni 35 (Tsh. Trilioni 95.37) hadi kufikia Dola Bilioni 110 (zaidi ya Tsh. Trilioni 299.75) ifikapo mwaka 2025

Pia, makadirio ya Kilimo cha Biashara kwa Wakulima Wadogo na Biashara ya Kilimo ya mwaka 2022, yanaonesha bado Afrika ina pengo la ufadhili wa kilimo la Dola Bilioni 74.5 (zaidi ya Tsh. Trilioni 203.01) kwenye Kilimo cha Kibiashara Kidogo na cha Kati (SMEs) hasa katika eneo la Jangwa la Sahara.

Soma https://jamii.app/ZeroHunger

#JamiiForums #Governance #Accountability #FoodSecurity #JFDATA
👍1
RIPOTI: Nchi za Lesotho, Malawi, #Namibia, Zambia, Zimbabwe, #Angola na Msumbiji zimeripotiwa kukumbwa na hali mbaya ya Upatikanaji wa Chakula, hali inayosababisha takriban Watu Milioni 27 kutokuwa na uhakika wa Chakula

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), takriban Watoto Milioni 21 katika Nchi hizo wameripotiwa kuwa na #Utapiamlo unaosababishwa na ukosefu wa Lishe Bora

WFP imeeleza kuwa ili kukabiliana na hali hiyo inayosababisha Watoto kupata Mlo mmoja au kukosa kabisa, zinahitajika takriban Tsh. Trilioni 1 (Dola Milioni 369) ambapo hadi sasa imepokea Theluthi moja tu ya kiasi hicho kutoka kwa Wafadhili.

Soma https://jamii.app/WFPFoodCrisis

#JamiiForums #Governance #FoodSecurity #Accountability
👍2