Upandaji wa Miti si tu ni juhudi za kuhifadhi Mazingira, pia ni hatua ya kumlinda Mwanamke dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi
Wanawake, hasa wa Vijijini, wanategemea sana rasilimali kama maji, kuni, na mazao ya kilimo kwa maisha yao ya kila siku. Mabadiliko ya tabianchi yanapoathiri moja kwa moja upatikanaji wa rasilimali hizi, huongeza mzigo wa Majukumu
Kwa kupanda miti, tunarejesha uoto wa asili, kuboresha vyanzo vya maji, na kupunguza kasi ya mabadiliko ya tabianchi, hivyo kuwasaidia Wanawake kuishi maisha bora na endelevu.
Soma https://jamii.app/SeraTabianchi
#JamiiForums #ClimateIsssues #ClimateChange #WanawakeNaTabianchi #JFWomen

👍1
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limesema njaa inaendelea kuongezeka, ambapo Watu Milioni 343 katika Nchi 74 wanakabiliwa na uhaba mkubwa Chakula, kiwango ambacho ni ongezeko la 10% ikilinganishwa na Mwaka 2023
Idadi hiyo inajumuisha Watu Milioni 1.9 walio katika hatihati ya kutumbukia kwenye baa la njaa, huku kiwango kikubwa cha njaa kikiripotiwa #Gaza, Sudan, Sudan Kusini, #Haiti na #Mali
Katika nchi za Afrika zilizo Kusini mwa jangwa la Sahara, zaidi ya Watu Milioni 170 wanakabiliwa na njaa. Mizozo Nchini Sudan, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na ukanda wa Sahel, ikichanganywa na majanga ya tabianchi yanayochochewa na El Niño, vimefanya janga la njaa kuwa kubwa zaidi.
Soma https://jamii.app/WFPNjaa2024
#PublicHealth #JamiiForums #HakiZaBinadamu #ClimateChange #FoodCrisis

❤1
UGANDA: Watu 15 wamepoteza Maisha huku wengine 100 hawajulikani walipo kutokana na Mvua kubwa iliyosababisha mafuriko na Maporomoko ya udongo Novemba 28, 2024
Mvua hiyo imesababisha uharibifu wa Makazi na Miundombinu kama Madaraja na Barabara katika Vijiji kadhaa Mashariki mwa Uganda, wilayani Bulambuli
Soma https://jamii.app/MaporomokoUgandaVifo15
#JamiiForums #JFMatukio #ClimateChange #Governance

👍3
MWANZA: Mwonekano wa baadhi ya Mitaa ya Furahisha – Kirumba baada ya mvua iliyonyesha leo Desemba 2, 2024, ambapo Maji yameathiri maeneo mbalimbali ikiwemo kufunika Barabara
Soma https://jamii.app/MwanzaDes2
#ClimateChange #JFMatukio #JamiiForums
Soma https://jamii.app/MwanzaDes2
#ClimateChange #JFMatukio #JamiiForums
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
MOROGORO: Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu imeanza kusafisha maeneo ya Mto Ngerengere, Mazimbu Manispaa ya Morogoro ili kuweka mazingira safi, kuruhusu maji kupita kwa urahisi na kupunguza athari wakati wa mafuriko
Afisa wa Maji Bonde la Wami Ruvu Kidakio cha Ngerengere, Mhandisi Nangu Makula amesema zoezi hilo litaenda umbali wa Mita 900 (Mazimbu hadi Kihonda)
Ikumbukwe Desemba 8, 2024, Mdau wa JamiiForums.com alitoa wito kwa taka zitolewe katika mto huo kwa kuwa zimechangia maji kuingia mtaani, akatolea mfano wanaokuwa hatarini zaidi ni Wanafunzi wa Shule za Msingi, Sekondari na wale wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Kampasi ya Mahlangu
Soma https://jamii.app/MtoNgerengereUsafi
#Accountability #ServiceDelivery #JamiiForums #ClimateChange

This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema msimu huu wa Masika unatarajiwa kuwa na ongezeko la Mvua katika Mwezi Aprili 2025
Akizungumza na Torchmedia, Mchambuzi wa Hali ya Hewa kutoka TMA, Joyce Makwata amesema mifumo ya hali ya hewa inaonyesha uwepo wa ongezeko la mvua na kuwa Wananchi waendelee kufuatilia taarifa za hali ya hewa na kuchukua tahadhari, ili kuepukana na athari za mvua zinazoweza kujitokeza
Aidha, amesema maeneo mengi yaliyo karibu na misitu au miti mingi yanatarajiwa kupata mvua nyingi tofauti na maeneo mengine
Soma https://jamii.app/TMAMvua
#JamiiForums #ClimateChange

👍2❤1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
MYANMAR: Matetemeko Mawili ya Ardhi yenye ukubwa wa richa 7.7 na 6.4 yameikumba Myanmar ambapo majengo mbalimbali ukiwemo Msikiti yameporomoka na kusababisha vifo vya watu 3 na mamia ya majeruhi huku takriban watu 81 wakiripotiwa kupotea
Athari za Matetemeko hayo zimeshuhudiwa hadi Thailand-Bangkok ambapo Mamlaka zimeripoti hali ya dharura huku shughuli za Uokoaji zikiendelea
Soma https://jamii.app/TetemekoMyanmar
#Earthquake #ClimateChange #Governance #JamiiForums

😢1
Aprili 11, 2025, Maeneo ya Kaskazini mwa Nchi ya China yalikumbwa na dhoruba iliyosababisha upepo mkali wenye kasi ya Kilomita 150 kwa Saa, ambapo Miti takriban 300 ilianguka na Magari kuharibika
Kutokana na athari hizo Mamlaka zilitoa tahadhari kwa Watu wenye uzito wa chini ya Kilogramu 50 kutotoka nje kwa kuhofia kubebwa na upepo
Eeeheee Mdau, dhoruba ikitokea Kilo zako zitakubeba au tutakupoteza? 😂😂😂
Mjadala https://jamii.app/UpepoChina
#JamiiForums #ChinaStorm #ClimateChange

MWANZA: Mdau aliyejitambulisha kuwa ni Mkazi wa Kitongoji cha Nyaruhama, Kijiji cha Nyangomango, Kata ya Usagara Wilayani Misungwi anadai kuna changamoto ya uharibifu wa mazingira eneo hilo unaochangiwa na utaratibu mbovu wa uchimbaji moramu
Anadai mashimo hayo wakati wa mvua yanajaa maji, pia kuna utamaduni wa kulipua mawe kwa baruti maeneo haya bila kufuata utaratibu hali ambayo ni hatari pia kwa Wananchi
Anatoa wito kwa Mamlaka za ngazi za juu kufuatilia changamoto hiyo ambayo anadai inaendana na mazingira ya uwepo wa Rushwa
Soma https://jamii.app/UsagaraArdhi
#JamiiForums #ClimateChange #Accountability #Uwajibikaji #JFMdau2025

PWANI: Mdau wa JamiiForums.com anahoji ni kwa nini Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) halichukui hatua au kukagua uharibifu wa mazingira unaofanywa na Kiwanda cha Pombe kilichopo Misugusugu Kibaha ikiwa Wananchi wameshalalamika mara kadhaa kwa Mamlaka hiyo?
Anadai maji hayo machafu yamekuwa na athari kwa viumbe wanaoishi au kutumia mabwawa madogo yaliyopo jirani
Soma https://jamii.app/MazingiraKibaha
#JamiiForums #ClimateChange #Accountability
Anadai maji hayo machafu yamekuwa na athari kwa viumbe wanaoishi au kutumia mabwawa madogo yaliyopo jirani
Soma https://jamii.app/MazingiraKibaha
#JamiiForums #ClimateChange #Accountability
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema mifumo ya Hali ya Hewa haioneshi uwepo wa mvua hivi karibuni hapa nchini badala yake kutakuwa na ukavu na ubaridi ambapo Wananchi wametakiwa kuchukua tahadhari za kujilinda na baridi
Meneja wa Utabiri wa TMA, Dkt. Mafuru Kantamla amesema mvua zilizonyesha hivi karibuni Ukanda wa Pwani zimetokana na ongezeko la Joto katika Bahari ya Hindi hususan katika Mwambao wa Pwani lakini hazitakuwa na mwendelezo kwa kuwa joto la Bahari limeanza kupungua kwa kasi
Soma https://jamii.app/HaliYaHewaJuni
Video Credits: Torch Media
#ClimateChange #JamiiForums #JamiiAfrica

❤2👍1
Tahadhari ya kutokea kwa mawimbi makubwa ya bahari 'Tsunami' imetolewa baada ya kutokea kwa tetemeko kubwa la ardhi lenye ukubwa wa Richa 8.8 katika eneo la Bahari ya Pacific Mashariki mwa Mji wa Urusi wa Petropavlovsk-Kamchatsky kwa mujibu wa Shirika la Jiolojia la Marekani (USGS).
Pia, Mamlaka ya Hali ya Hewa Japan imetangaza tahadhari ya Tsumani kwa maeneno mengi ya Pwani ya Mashariki mwa Nchi hiyo ikitoa onyo kwa Wananchi kuepuka maeneno ya Ufukweni kutokana na uwezekano wa mawimbi yenye urefu wa Mita 3.
Aidha, tahadhari pia imetolewa kwa maeneo ya Taiwan, Ufilipino, Visiwa vya Hawaii na Visiwa vya Aleutin vya Alaska kuwa makini na mawimbi hayo.
Soma https://jamii.app/TsunamiTetemekoRussia
#JamiiForums #JamiiAfrica #RussiaEarthquake #NaturalDisasters #ClimateChange

❤2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
PAKISTAN: Zaidi ya Watu 300 wameripotiwa kupoteza Maisha Kaskazini Magharibi mwa Pakistan kufuatia mvua kubwa na mafuriko yaliyodumu kwa siku mbili, kwa mujibu wa taarifa za maofisa wa eneo hilo Mvua hizo zimeambatana na maporomoko ya ardhi, radi, mafuriko ya ghafla na kufanya msimu wa monsoon kuwa mbaya zaidi Mwaka huu (2025).
Shughuli za uokoaji na kufungua barabara zilizozibwa zimeendelea, huku Serikali ikitoa fedha za dharura. Taarifa ya Wataalam wa Hali ya Hewa imeeleza kuwa hali inatarajiwa kuwa mbaya zaidi kwani mvua zinatarajiwa kuendelea hadi Agosti 21, 2025.
Soma zaidi https://jamii.app/PakistanVifo
#JamiiAfrica #JamiiForums #ClimateChange

AFGHANISTAN: Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa na Vyombo vya Habari vya Reuters na Al Jazeera ni kuwa zaidi ya Watu 800 wameripotiwa kupoteza maisha na wengine zaidi ya 2,500 kujeruhiwa kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lenye ukubwa wa Ritcher 6.0 lililotokea Mashariki mwa Afghanistan usiku wa kuamkia Septemba 1, 2025.
Idadi ya vifo imeendelea kuongezeka kutoka taarifa za awali zilizotolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali, huku jitihada za uokoaji zikiendelea. Maeneo yaliyoathirika zaidi ni Kunar na Nangahar. Tukio hilo limefuatia tetemeko lililotokea Oktoba 2023 Magharibi mwa Afghanistan na kuua takribani Watu 2,400.
Mashirika ya misaada yameonya kuhusu ukubwa wa janga hilo na kueleza kuwa zaidi ya nusu ya Wananchi wanahitaji msaada wa haraka. Umoja wa Mataifa umetangaza kuandaa msaada kwa walioathirika, huku China ikiahidi kutoa msaada wa dharura kulingana na uwezo wake.
Soma zaidi https://jamii.app/Tetemeko

Baadhi ya mambo yanayotishia biashara ya Kaboni Mkoani Katabi ni; mipaka ya vijiji karibu na misitu imekuwa ikisogezwa taratibu, shughuli za kibinaadamu ikiwemo kilimo zimeongezeka na kupunguza sehemu ya misitu…
Kifungu cha 4 cha Sheria ya Misitu Na. 14 ya Mwaka 2002, vijiji vina mamlaka ya kusimamia misitu yao kupitia Kamati za Maliasili. Ofisa Mazingira wa Wilaya ya Tanganyika, Joseph Bisura anasema “Rasilimali za kufanya doria ni ndogo, pia bado kuna Wananchi hawajaelewa kikamilifu umuhimu wa kulinda misitu.”
Zaidi https://jamii.app/BiasharaYaKaboni
#JamiiForums #ClimateChange #Governance
Kifungu cha 4 cha Sheria ya Misitu Na. 14 ya Mwaka 2002, vijiji vina mamlaka ya kusimamia misitu yao kupitia Kamati za Maliasili. Ofisa Mazingira wa Wilaya ya Tanganyika, Joseph Bisura anasema “Rasilimali za kufanya doria ni ndogo, pia bado kuna Wananchi hawajaelewa kikamilifu umuhimu wa kulinda misitu.”
Zaidi https://jamii.app/BiasharaYaKaboni
#JamiiForums #ClimateChange #Governance
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
PWANI: Mdau anadai kuna ugawaji wa vibali vya uchimbaji mchanga kiolela katika Kata ya Vianzi, hususan eneo maarufu kwa Mzee Lyimo, ambapo Wanachimba mchanga na kusababaisha mashimo makubwa ambayo yamekuwa tishio kwa Watoto na Wakazi wa eneo hilo.
Anaongeza kuwa wameshafuatilia kwa mamlaka bila kupata suluhisho, badala yake mashimo yanazidi kuongezeka na wanachonga barabara kuelekea maeneo hayo ili wachimbe zaidi. Hatua zichukuliwe haraka kuokoa mazingira yetu.
Mdau, hali ikoje huko kwenu?
Shiriki mjadala https://jamii.app/VibaliVyaMchanga
#JamiiForums #Uwajibikaji #JFMdau2026 #ClimateChange

Meneja wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Kanda ya Morogoro-Rufiji, Arnold Mapinduzi anasema kwa mujibu wa Kifungu cha 81 cha Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya Mwaka 2004 ni lazima miradi yote ifanyiwe Tathmini ya Athari za Mazingira (EIA) kabla ya mradi kuanza,
Anaongeza kuwa hajapokea malalamiko kuhusiana na miradi ya TAZAMA na TANESCO ambayo ni sehemu ya inayodaiwa kuwa na uchafu.
Zaidi https://jamii.app/MiradiMikubwa
#JamiiForums #Uwajibikaji #ClimateChange
Anaongeza kuwa hajapokea malalamiko kuhusiana na miradi ya TAZAMA na TANESCO ambayo ni sehemu ya inayodaiwa kuwa na uchafu.
Zaidi https://jamii.app/MiradiMikubwa
#JamiiForums #Uwajibikaji #ClimateChange
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
VENEZUELA: Rais wa Mpito wa Venezuela, Delcy Rodríguez kupitia mahojiano na shirika la utangazaji la taifa la Venezuela, amesema anaratibu mikakati na Umoja wa Mataifa (UN) ili kutuma waokoaji, pia ametoa wito kwa sekta binafsi kusaidia kwa kutoa mitambo ili kufanikisha juhudi za uokoaji
Aidha, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio amesema kuwa Marekani tayari imetuma vikosi vya uokoaji nchini Venezuela na itapeleka vifaa kwenye uwanja mkuu wa ndege wa nchi hiyo, ambao amesema "umeharibiwa vibaya."
Zaidi https://jamii.app/VenezuelaVifo
#JamiiAfrica #JamiiForums #ClimateChange
Aidha, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio amesema kuwa Marekani tayari imetuma vikosi vya uokoaji nchini Venezuela na itapeleka vifaa kwenye uwanja mkuu wa ndege wa nchi hiyo, ambao amesema "umeharibiwa vibaya."
Zaidi https://jamii.app/VenezuelaVifo
#JamiiAfrica #JamiiForums #ClimateChange
Moja ya mijadala inayoendelea ndani ya JamiiForums.com kuhusu hoja za Wadau wanaodai kelele za mitambo ya viwanda vilivyo katika makazi ya Watu kuwa kero katika maeneo mbalimbali nchini
Umewahi kupata changamoto ya aina hii, ulichukua hatua gani?
Zaidi https://jamii.app/KeleleZaViwanda
#JamiiForums #JFMdau2026 #Uwajibikaji #ClimateChange

MBEYA: Kilimo cha tumbaku, mahitaji makubwa ya Nishati ya kuni na mkaa na shughuli za uchimbaji madini zinazoendelea katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, vimechochea uharibifu wa mazingira na kuongeza kasi ya upotevu wa misitu, hali inayotishia uendelevu wa rasilimali za misitu.
Mdau, hali ya uharibifu wa mazingira ikoje katika eneo unaloishi?
Zaidi https://jamii.app/MazingiraChunya
#JamiiForums #JFMatukio #ClimateChange