JamiiForums
✔
23.9K subscribers
40.7K photos
3.6K videos
34.7K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DAR: Mdau wa JamiiForums ameziomba mamlaka husika kushughulikia ongezeko la Wafanyabiashara kwenye barabara ya mwendokasi ya Gongo la Mboto akidai hali hiyo husababisha foleni hasa mida ya jioni na asubuhi, ameshauri changamoto itatuliwe kabla mambo hayajawa mabaya zaidi.

Kwa taarifa zaidi tembelea https://jamii.app/GongoLaMbotoBarabara

Unaweza kuwasilisha KERO yako kupitia FichuaUovu ndani ya JamiiForums.com📌📌

#JamiiForums #JFMdau2026 #Uwajibikaji #ServiceDelivery
Mdau wa JamiiForums.com amesema utaratibu wa kupanga foleni ili kuongeza salio kwenye Kadi za "N-CARD" zinazotumika kukata tiketi za vivuko Kigamboni unachelewesha Watu katika shughuli zao za kila siku, ameshauri ziwepo mbinu za Kidigitali kufanya mchakato huo badala ya kupanga foleni.

Zaidi https://jamii.app/KeroKivukoni

#JamiiForums #JFMdau2026 #ServiceDelivery
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ametoa kauli hiyo Februari 12, 2026, alipokuwa katika ziara yake Wilaya ya Kinondoni akikagua miundombinu ya Shule ya Sekondari Tarimba Abbas ambayo inajengwa.

Ikumbukwe mara kadhaa Wadau wa JamiiForums.com wameelezea uwepo wa changamoto ya Wanafunzi kukaa chini kutokana na uhaba wa madawati katika baadhi ya shule, ambapo wamekuwa wakitoa wito kwa mamlaka zinazohusika kushughulikia kero hiyo kwa maelezo kuwa inaathiri masomo.

Kwa taarifa zaidi tembelea https://jamii.app/WanafunziDar

#JamiiForums #Accountability #ServiceDelivery
🤬1
NJOMBE: Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa Shirika la Umeme Tanzania (#TANESCO) Wilaya ya Ludewa kushughulikia kero ya umeme kukatika kila mara jioni, tatizo ambalo limeendelea kwa takriban mwezi mzima.

Soma https://jamii.app/UmemeMatikaNjombe

#JamiiForums #Accountability #JFMdau2026 #JFHuduma #ServiceDelivery
MWANZA: Mdau wa JamiiForums.com anaelezea “Nilijiandikisha na kupata Namba ya NIDA Mwaka 2020 na nikaenda kufuatilia kitambulisho Mwaka 2022 ambapo nikaambiwa bado. Nikarudi Disemba 2025 nikaambiwa bado, nilipohoji mbona inachukua muda mrefu kiasi hicho? Nikaambiwa itakuwa kilisahaulika.”

Anaendelea, “Inawezekana vipi taarifa zilizopo kwenye mfumo zisahaulike? Nikaambiwa linashughulikiwa nitapata ujumbe kikiwa tayari, hadi leo Februari 2026 sijapata chochote, hii inarudisha nyuma shughuli za kiuchumi kwani katika maombi ya kazi au huduma za taasisi nyingi zinahitaji Kitambilisho cha NIDA.”

Hivyo, Mdau anaomba Uongozi wa #NIDA Ilemela au wa juu uchunguze sababu za kutokea kwa hali hiyo kama ni uzembe au tatizo ni mfumo wao!

Zaidi tembelea https://jamii.app/NIDAMwanzaMalalamiko

#JamiiForums #JFHuduma #ServiceDelivery #JFMdau2026
❤1👏1
Baada ya Mdau wa JamiiForums.com kudokeza kuwepo kwa uzembe katika Ofisi za #NIDA eneo la Ilemela, Mwanza, Wadau wengine kupitia Mitandao ya Kijamii pia wamejitokeza kueleza changamoto wanazokutana nazo kwenye mchakato huo wa kupata Vitambulisho vya Taifa.

Zaidi tembelea https://jamii.app/NIDAMwanzaMalalamiko

#JamiiForums #JFMdau2026 #Uwajibikaji #ServiceDelivery

Nawe pia unaweza kuwasilisha KERO yako kupitia FichuaUovu ndani ya JamiiForums.com📌📌
Mdau wa JamiiForums.com amehoji kwa nini Wasimamizi wa kwenye milango ya kuingia Vituo vya Mabasi ikiwemo Msamvu Morogoro hawatambui SMS za malipo ya tiketi ya Mtandaoni? Akidai Abiria mwenye tiketi ya karatasi hazuiliwi lakini wenye tiketi za Mtandaoni wanasumbuliwa na kutakiwa kulipa fedha ya kuingia au kutoka Kituoni.

Zaidi tembelea https://jamii.app/WalinziMsamvu

#JamiiForums #JFHuduma #ServiceDelivery #JFMdau2026

Nawe pia unaweza kuwasilisha KERO yako kupitia DM au FichuaUovu ndani ya JamiiForums.com📌📌
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Akizungumza na Waandishi wa Habari, Februari 26, 2026, Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema Mwaka 2026 Serikali inatarajiwa kununua ndege 4 aina ya Bombadier Q400 ili kuboresha huduma za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) ikiwa ni sehemu ya kukamilisha ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ) ambayo iliahidi ndani ya miaka 5 itanunua ndege 8.

Kwa taarifa zaidi tembelea https://jamii.app/MsigwaNdege

#JamiiForums #Uwajibikaji #ServiceDelivery
Mdau wa JamiiForums.com anadai Sera ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa Mtu aliyeondolewa katika ajira binafsi, kumpatia 33% ya mshahara wake kwa miezi sita, kisha kumsimamisha kwa Miezi 18 akitarajiwa apate ajira nyingine, ni sawa na kushikilia fedha za Mtu kwa miezi 24 bila uhakika wowote.

Anaandika “Inaonekana waliopitisha sera hiyo hawatambui ugumu uliopo kupata ajira mpya, kama ni rahisi kiasi hicho kwa nini Wabunge hawako tayari kukaa Bungeni muhula mmoja au miwili tu kisha waende kutafuta ajira? Fao la Kujitoa ni mkombozi wa Vijana wengi katika kupata mitaji.”

Anaongeza “Sera za Mifuko ya Kijamii ziendane na uhalisia wa maisha yetu, NSSF imewasababishia Vijana wengi msongo mkubwa wa mawazo kwa Sera zao hizo, Bunge litafakari hilo kwa maslahi mapana ya Taifa na Fao la Kujitoa lirejeshwe.”

Zaidi https://jamii.app/FaoLaKujitoa

#JamiiForums #Uwajibikaji #ServiceDelivery
❤3
DAR ES SALAAM: Mdau wa JamiiForums.com anadai baadhi ya Maafisa wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo wamemshikilia Kijana aliyeajiriwa kuuza duka kuanzia Mchana wa Machi 5, 2026 na kwenda kumlaza katika ofisi zao zilizopo Kibamba hadi Machi 6, 2026 kisa kuna changamoto ya Leseni ya duka analofanya kazi.

Anahoji “Sheria ipi imetumika kumuweka ndani ya ofisi zao na kumlaza hapo Mfanyabiashara kisa leseni imelipiwa eneo tofauti? Inamaana hata Mamlaka nyingine mfano DAWASA au TANESCO wakikukuta hujalipa bili yao wanakuchukua wanakuweka ndani kwenye ofisi zao? Ofisi ya Manispaa imekuwa Kituo cha Polisi?”

Zaidi tembelea https://jamii.app/UbungoManispaa

#JamiiForums #Uwajibikaji #Mdau2026 #Governance #ServiceDelivery

Nawe pia unaweza kuwasilisha Kero yako kupitia FichuaUovu ndani ya JamiiForums.com📌📌
❤3🤬1
Mdau wa JamiiForums.com anadai Mtandao wa kuomba Vibali vya Kazi (Work Permit) haupatikani zaidi ya wiki sasa na kwamba hali hiyo imekuwa kero watumiaji wengi ambao shughuli zao zimesimama au utendaji umesimama kwa kuwa utatuzi haujapatikana.

Kwa taarifa zaidi soma https://jamii.app/VibaliKazi

#JamiiForums #JFMdau2026 #ServiceDelivery
Baada ya baadhi ya Wadau wa JamiiForums.com kulalamika kutojua hatua ya maombi ya Vitambulisho walivyoomba kwa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (#NIDA), hivyo kulazimika kwenda vituoni mara kwa mara, Mamlaka hiyo imesema imeona maoni na malalamiko hayo na kueleza Wananchi wanaweza kujua hali ya Vitambulisho vyao kwa njia ya Mtandao.

Zaidi https://jamii.app/NIDAKitambulishoMtandaoni

#JamiiForums #Uwajibikaji #DigitalWorld #ServiceDelivery
❤1
Ikumbukwe, Machi 10, Mdau wa JamiiForums.com aliandika “Vibali vya Kazi zaidi ya wiki sasa Mtandao unasumbua haufunguki, nini shida?” Machi 13, 2026, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano (OWM-KAM) ikaomba radhi na kusema kuna tatizo la kiufundi katika Mfumo wa Vibali vya Kazi (OWAIS), lakini Mdau anadai bado changamoto hiyo haijatatuliwa.

Zaidi soma https://jamii.app/MfumoVibaliKazi

#JamiiForums #JFMdau2026 #ServiceDelivery
ARUSHA: Taarifa ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kujibu hoja ya Mdau kuhusu taa za kuongozea magari za eneo la Sakina Triple A kutowaka kwa muda wa miezi minne imeeleza “Kwa sasa tunaendelea na taratibu za manunuzi kwa ajili ya kufunga taa mpya za kisasa zenye ufanisi mkubwa. Tunaomba radhi kwa usumbufu uliotokea.”

Fuatilia zaidi https://jamii.app/TANROADSTaa

#JamiiForums #Uwajibikaji #ServiceDelivery #JFMdau2026
Mdau ameshauri kuwa kampuni zinazounga huduma ya "Home Internet" nchini ziwajibishwe pale ambapo wanashindwa kutatua changamoto za Wateja na kuboresha huduma za utoaji Intaneti kwa Wateja.

Umeshakutana na changamoto hii? Una maoni gani?

Mjadala huu unaendelea hapa https://jamii.app/HudumaIntanetiMbovu

#JamiiForums #ServiceDelivery #JFMdau2026 #DigitalRights
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kike na Uzazi kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Jofrey Marandu anaeleza kwa kina nini cha kufanya pale mjamzito anapopata kifafa cha mimba, dalili zake, pamoja na umuhimu wa kupata huduma ya haraka ya kitabibu.

Elimu hiyo imechapishwa na Hospitali ya Taifa Muhimbili kupitia Akaunti yao ndani ya JamiiForums.com

Zaidi tembelea https://jamii.app/KifafaChaMimba

#JamiiForums #ServiceDelivery #PublicHealth
Mdau ametoa wito kwa mamlaka husika kutatua changamoto ya muda mrefu ya ukosefu wa chumba cha kuhifadhia maiti (Mochwari) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi.

Zaidi https://jamii.app/GariLaStaff

#JamiiForums #ServiceDelivery #JFMdau2026 #Uwajibikaji
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
KUMBUKIZI: Masanja Kadogosa, ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Bariadi Vijijini aliyasema hayo Februari 26, 2024, alipokuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), akizungumza na Waandishi wa Habari kabla ya kuanza kwa safari ya majaribio ya treni ya umeme ya abiria kutoka Dar es Salaam kuelekea mjini Morogoro.

Zaidi tembelea https://jamii.app/sgrumeme

#JamiiForums #Uwajibikaji #ServiceDelivery
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Kupitia Kikao cha Ushauri Wilaya ya Mpanda (DCC) cha Septemba 4, 2026, Mwananchi alihoji sababu ya umeme kukatika mara kwa mara katika Manispaa ya Mpanda licha ya Katavi kuunganishwa na Gridi ya Taifa, ufafanuzi umetolewa na Afisa Huduma kwa Wateja wa TANESCO Mkoa, Mary Ngole.

Ikumbukwe, mara kadhaa Wadau wa JamiiForums.com wamewasilisha hoja zao wakidai kuna changamoto ya umeme kukatika mara kwa mara hali inayosababisha kero na hasara katika shughuli zao za kila siku.

Zaidi https://jamii.app/KataviTANESCO

#JamiiForums #Uwajbikaji #JFMdau2026 #ServiceDelivery
❤1
Mdau, imewahi kukutokea ukaona nauli haiendani na hadhi ya usafiri uliopanda? Nini kifanyike?

Zaidi https://jamii.app/LATRAVIPMabasi

#JamiiForums #Uwajibikaji #JFMdau2026 #ServiceDelivery #JFHuduma