JamiiForums
✔
23.9K subscribers
40.7K photos
3.6K videos
34.7K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Nchini Thailand, Watu wasiopungua 18 wamepoteza Maisha huku juhudi za uokoaji zikiendelea kuwatafuta wengine 78 waliokuwa kwenye jengo la ghorofa 30 lililoanguka Jijini Bangkok baada ya Matetemeko Mawili ya Ardhi yenye ukubwa wa richa 7.7 na 6.4 kuikumba Myanmar, Machi 29, 2025

Aidha, Misaada ya kibinadamu kutoka China, Urusi, India, Uingereza na mataifa jirani imeanza kuwasili Myanmar kusaidia waathirika wa tetemeko

Soma https://jamii.app/MyanmarUpdates

#JamiiForums #MyanmarEarthquake #NaturalDisasters
👍1
MYANMAR: Maafisa wa Uokoaji wamesimama kwa dakika moja (kimya) karibu na jengo la Sky Villa condominium, moja ya maeneo yaliyoathirika zaidi na tetemeko la Ardhi la Machi 28, 2025, kutoa heshima kwa waathirika

Tetemeko hilo lenye ukubwa wa 7.7 ndilo kubwa zaidi kuwahi kutokea Nchini humo katika zaidi ya Miaka 100, likiangusha pagoda za Kihistoria na majengo ya Kisasa

Kiongozi wa Kijeshi wa Myanmar, Jenerali Mkuu Min Aung Hlaing, amesema idadi ya vifo imefikia 2,719 na huenda ikazidi 3,000. Aidha, Watu wasiopungua 20 wamefariki katika Nchi jirani ya Thailand.

Soma zaidi: jamii.app/EarthQuakeDeathToll

#JamiiForums #MyanmarEarthquake #Governance #NaturalDisasters
👍1
Tahadhari ya kutokea kwa mawimbi makubwa ya bahari 'Tsunami' imetolewa baada ya kutokea kwa tetemeko kubwa la ardhi lenye ukubwa wa Richa 8.8 katika eneo la Bahari ya Pacific Mashariki mwa Mji wa Urusi wa Petropavlovsk-Kamchatsky kwa mujibu wa Shirika la Jiolojia la Marekani (USGS).

Pia, Mamlaka ya Hali ya Hewa Japan imetangaza tahadhari ya Tsumani kwa maeneno mengi ya Pwani ya Mashariki mwa Nchi hiyo ikitoa onyo kwa Wananchi kuepuka maeneno ya Ufukweni kutokana na uwezekano wa mawimbi yenye urefu wa Mita 3.

Aidha, tahadhari pia imetolewa kwa maeneo ya Taiwan, Ufilipino, Visiwa vya Hawaii na Visiwa vya Aleutin vya Alaska kuwa makini na mawimbi hayo.

Soma https://jamii.app/TsunamiTetemekoRussia

#JamiiForums #JamiiAfrica #RussiaEarthquake #NaturalDisasters #ClimateChange
❤2