JamiiForums
βœ”
23.9K subscribers
40.7K photos
3.61K videos
34.7K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UMUHIMU WA BUNDI KWA WAKULIMA

Mbali na kuchukuliwa kama uchuro lakini wana msaada mkubwa kwa Wakulima kwa kuwa wanakula Panya, Wadudu na Ndege waharibifu wa Mazao

Bundi hutembelea Makazi ya Watu ili kupata chakula ambacho ni Panya na Mijusi

Soma https://jamii.app/BundiKilimo
#Kilimo
SERIKALI KUTOTOA KIBALI CHA KUAGIZA SUKARI NJE YA NCHI

Waziri wa #Kilimo, Prof. Mkenda amesema Sukari kutoka nje inasababisha Viwanda vya ndani kushindwa kukua

Asema katika bonde la Kilombero kila Mwaka tani 350,000 za Miwa hutupwa

Soma - https://jamii.app/VibaliSukari
#Uchumi #JFLeo
MAWAZIRI WATAKIWA KUJA NA MIKAKATI YA KUTUMIA TEKNOLOJIA KUMSAIDIA MKULIMA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka Waziri wa Kilimo pamoja na wa Uwekezaji kuhakikisha Wakulima wanapata Mbegu bora, pembejeo na kuunganishwa na masoko ya uhakika

Soma https://jamii.app/MkakatiKilimo
#Kilimo
MBEYA: Never Black Mwakalinga, Wakala wa Pembejeo za #Kilimo katika Kijiji cha Mwaya na Holdin ambaye ni Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho, wamehukumiwa Kifungo cha Miaka mitatu kwa kughushi vocha za Pembejeo za Kilimo

Soma https://jamii.app/JelaKwaKughushi

#KemeaRushwa
πŸ‘7😁1
OKTOBA 16: SIKU YA CHAKULA DUNIANI

Siku hii ilianzishwa na Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO), ikilenga kupambana na Njaa na kuboresha Mifumo ya #Kilimo ili kuhakikisha Baa la Njaa linatokomezwa Duniani

Soma https://jamii.app/WFD2022

#HumanRights #WFD2022
πŸ‘6πŸ‘1
MTWARA: WANAFUNZI 1,648 WA KIDATO CHA 2 NA 4 WAMEACHA SHULE 2022

Ni kutokana na sababu mbalimbali kama; Mimba, Kuhama kwa Wazazi kwa ajili ya #Kilimo, Hali ngumu ya Maisha, Wazazi kutengana na Wenyewe kutokuwa na mwamko wa #Elimu

Soma https://jamii.app/KuachaShule

#ServiceDelivery
πŸ€”10πŸ‘Ž6πŸ‘5😒1
#JFDATA: Wakati baadhi ya maeneo Nchini yakikabiliwa na Upungufu wa Chakula, ikiwa ni pamoja na kupanda kwa Bei ya Mazao ya Nafaka, 75.5% ya Ardhi inayofaa Nchini bado haijatumika kwa #Kilimo

Halmashauri 17 katika Mikoa 8 zimetajwa kukabiliwa na upungufu wa #Chakula kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo Ukame, Wanyama Pori, Ndege aina ya Kweleakwelea na Viwavi Jeshi

Soma https://jamii.app/KilimoTZ

#JFUwajibikaji23 #FoodSecurity #FoodSafety
πŸ‘6
Mdau wa JamiiForums.com amesema Shughuli za kibinadamu kama #Kilimo na ukataji wa Miti kwa ajili ya kuni na Mkaa, zimepelekea uharibifu mkubwa wa misitu ambao unaweka hatari kubwa kwa vizazi vijavyo

Ameshauri Wadau wa #Mazingira kuzipa kipaumbele jitihada za Utunzaji wa Misitu, ikiwemo utekelezaji wa njia endelevu za usimamizi wa ardhi, kama vile kilimo shirikishi na upandaji wa miti kwenye ardhi iliyoharibiwa ili kurejesha ikolojia ya #Misitu

Soma https://jamii.app/MisituItunzwe

#EnvironmentalConservation
πŸ‘5
Benki ya Dunia imeipatia Tanzania Mkopo wa Dola za Marekani Milioni 300 (zaidi ya takriban Tsh. 700 Bilioni) kwa ajili ya kuchochea Uzalishaji, kuimarisha Sekta ya #Kilimo na kukabiliana na Mabadiliko ya #TabiaNchi

Miongoni wa mambo yatakayotekelezwa ni pamoja na kuboresha utoaji wa Huduma katika Utafiti, Ugani na Mbegu, Kuendeleza Miundombinu ya Kilimo Vijijini pamoja na kuimarisha usimamizi wa Rasilimali Fedha na Uwekezaji

Soma https://jamii.app/MkopoBilioni700

#ServiceDelivery #ClimateChange #Agriculture
πŸ‘6πŸ‘Ž5
Mdau wa JamiiForums.com anasema kumekuwa na tabia ya Wazazi, Viongozi na Walimu kutishia Watoto kuwa wasiposoma watakuwa Wakulima maisha yao yote. Hii inawajengea dhana kwamba #Kilimo ni kazi ya mtu aliyekataa shule

Huku Kilimo kikizidi kuonekana kuwa ni kazi ya mtu asiyekuwa na #Elimu, utasikia viongozi wakiwaambia vijana wenye Shahada wakajiajiri kwenye kilimo baada ya kushindwa kuwaaajiri

Amehoji, ni kwa namna gani tunategemea vijana wawe na moyo wa kujiajiri kwenye kilimo ikiwa miaka yote wamejengewa dhana hasi kukihusu?

Soma https://jamii.app/KilimoNiKazi

#JFHuduma #ServiceDelivery
πŸ‘2❀1
Katika Nchi nyingi Duniani kote, asilimia kubwa ya Watoto wanaotumikishwa wanafanya kazi katika Sekta ya #Kilimo, Uvuvi, Ufugaji wa Samaki, Misitu na Mifugo

Kwa mujibu wa Shirika la Kazi Duniani (ILO), kilimo ni mojawapo ya Sekta tatu hatari zaidi katika suala la Vifo vinavyohusiana na Kazi, Ajali zisizo mbaya na Magonjwa yanayotokana na kazi

Umasikini ndio sababu kuu ya Ajira kwa Watoto katika Kilimo, pamoja na Upatikanaji mdogo wa Elimu bora, na Teknolojia duni ya Kilimo

Ajira kwa Watoto ni jambo ambalo limeenea zaidi katika Nchi za Ulimwengu wa tatu ambapo Umasikini umekithiri. Kwasababu Wazazi hawana Ujuzi na fursa za kuandalia Familia zao inavyopaswa, Watoto hutafuta kazi ili kusaidia Familia kupata riziki

Soma https://jamii.app/AjiraHatariWatoto

#JamiiForums #JFHakiElimu #HumanRights #ChildRights #ChildProtection
πŸ‘6❀1
#RipotiYaUwajibikaji imebainisha mapungufu katika Usimamizi wa rasilimali za #Kilimo, ikiwemo Mkandarasi kutelekeza Mradi wa Ujenzi wa Maghala 14 ya Halmashauri ya Wilaya ya #Babati, wenye thamani ya Tsh. Bilioni 1.07 ambao ulitarajiwa kukamilika Agosti 30, 2022

Changamoto hiyo imetokana na Menejimenti ya Wizara kushindwa kusimamia Vipengele vya Mkataba vinavyomtaka Mkandarasi kuwepo eneo la Ujenzi au kutoa taarifa ya kutokuwepo kwake na hatua zinazopaswa kuchukuliwa endapo hatatekeleza vipengele hivyo

Soma https://jamii.app/HudumaZaJamii

#HudumaKwaJamii #JFUwajibikaji23 #JFHuduma #RipotiYaUwajibikaji23 #JamiiForums
πŸ‘1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Waziri wa #Kilimo, Hussein Mohammed Bashe, akifafanua kuhusu uhaba wa #Sukari Nchini na hatua ambazo Serikali inachukua kuhusu baadhi ya Wafanyabiashara wanaouza bei tofauti na iliyoelekezwa na Serikali

Soma https://jamii.app/IkuluFeb22

#Governance #JamiiForums
πŸ‘2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Akifafanua kuhusu changamoto ya Sukari Nchini, Waziri wa #Kilimo, Hussein Mohammed Bashe amegusia kuhusu Serikali kufanya Mabadiliko ya #Biashara ya Sukari na kuruhusu ushindani wa Bidhaa hiyo kwa wawekwa wa ndani na nje ya Nchi

Soma https://jamii.app/IkuluFeb22

#Governance #Economy #Accountability #JFHuduma #JamiiForums
πŸ‘7
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Waziri wa #Kilimo, Hussein Mohammed Bashe, amesema baadhi ya Wafanyabiashara wamechangia uhaba wa Sukari Nchini kutokana na kutotimiza maelekezo ya vibali wanavyopewa

Aidha, amedai baadhi ya Wafanyabiashara wanaficha bidhaa hiyo, akiahidi Serikali kuwachukulia hatua wote watakaohusika hadi ngazi ya Kiwanda kinachozalisha kikibainika kushiriki katika Mchezo huo

Soma https://jamii.app/IkuluFeb22

#Governance #Economy #Accountability #JFHuduma #JamiiForums
πŸ‘4πŸ”₯1
Dhima ya Msimu wa 4 wa Shindano la Stories Of Change (SoC 2024) ni "Tanzania Tuitakayo" ikilenga kuhamasisha Wananchi kuibua mawazo bunifu ya kuboresha Sekta mbalimbali Nchini kama #Elimu, #Habari na #Mawasiliano, #Biashara, #Kilimo na #Ufugaji, #Afya, #Teknolojia n.k

Mawazo hayo ni lazima yawe yanayoweza kutekelezeka ndani ya Miaka 5 hadi 25 ijayo

Kumbuka; Mawazo bunifu yanaweza kujikita kwenye Uwanja mmoja tu, sio lazima kugusia yote

Soma https://jamii.app/SoCS4

#JamiiForums #SoC #StoriesOfChange #SoC2024 #Maendeleo #TanzaniaTuitakayo
❀1
#SaveTheDate! Hafla ya utoaji wa Tuzo za Stories of Change Msimu wa 4 inakaribia.

Mwaka huu Washiriki walionesha 'Nguvu ya Kalamu’ zao kwa mawazo, maoni na michango ya kipekee katika kuijenga 'Tanzania Tuitakayo' wakilenga kuboresha #Uchumi, #Elimu, #Afya, #Teknolojia, #Kilimo n.k.

Mbali na zawadi kutolewa kwa Washindi wa Maandiko Bora Usiku wa Septemba 21, 2024, Wazalishaji Bora wa Maudhui kutoka JamiiForums.com watatambuliwa na kutuzwa kwa mchango wao mkubwa katika Majukwaa yetu ya Kidijitali

Zaidi tembelea https://jamii.app/7DaysAwardCeremonySoC

#JamiiForums #SoC2024 #StoriesOfChange #Accountability #Governance #TanzaniaTuitakayo #SoCS4
Hafla ya utoaji wa Tuzo za Shindano la Stories of Change (#SoC) Msimu wa 4 inatarajiwa kufanyika siku Sita kutoka leo ambapo itakuwa Septemba 21, 2024

Mwaka huu 2024, Washiriki wameonesha uwezo wa juu katika kuijenga 'Tanzania Tuitakayo' wakilenga kuboresha #Uchumi, #Elimu, #Afya, #Teknolojia, #Kilimo n.k

Mbali na Washindi wa Maandiko Bora kupewa zawadi, pia baadhi ya Wazalishaji Bora wa Maudhui ndani ya JamiiForums.com watatambuliwa na kutuzwa kwa mchango wao mkubwa katika Majukwaa yetu ya Kidijitali

Zaidi tembelea https://jamii.app/SoC24

#JamiiForums #SoC2024 #StoriesOfChange #Accountability #Governance #TanzaniaTuitakayo #SoCS4
πŸ‘1
#FewHoursToGo! Hafla ya utoaji wa Tuzo za Shindano la Stories of Change (#SoC) Msimu wa 4 inatarajiwa kufanyika kesho, Septemba 21, 2024

Mwaka huu Washiriki wameonesha uwezo wa juu katika kuijenga 'Tanzania Tuitakayo' wakilenga kuboresha #Uchumi, #Elimu, #Afya, #Teknolojia, #Kilimo n.k

Mbali na zawadi kutolewa kwa Washindi wa Maandiko Bora Usiku wa Septemba 21, 2024, Wazalishaji Bora wa Maudhui kutoka JamiiForums.com watatambuliwa na kutuzwa kwa mchango wao mkubwa katika Majukwaa yetu ya Kidijitali

#JamiiForums #SoC2024 #StoriesOfChange #Accountability #Governance #TanzaniaTuitakayo #SoCS4
❀1πŸ‘1
Siku ya Kimataifa ya Wanawake wa Vijijini huadhimishwa Oktoba 15 kila Mwaka ikilenga kutambua jukumu na mchango muhimu wa Wanawake wa Vijijini katika kuimarisha Maendeleo ya #Kilimo, Kuboresha Usalama wa Chakula na Kutokomeza Umasikini Vijijini

Pia, Siku hii inaangazia jukumu la Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wa Wanawake katika kupambana na Umasikini uliokithiri, Njaa na Utapiamlo ambapo kwa mujibu wa takwimu, Wanawake wa Vijijini wanachangia takriban 22% ya idadi ya Watu wote Duniani.

Soma https://jamii.app/VillageWomen

#JamiiForums #SikuYaWanawakeWaVijijini #JFWomen #IDRW2024