MICHEZO: ANTONIO CONTE NA KLABU YA INTER MILAN WAKUBALIANA KUSITISHA MKATABA
- Klabu ya #InterMilan itamlipa Antonio Conte kiasi cha Shilingi za Kitanzania Bilioni 19.8 kama fidia
- #Conte anaondoka #Inter akiwa amewapa ubingwa wa kwanza wa Ligi Kuu ya Italia
#JamiiForums

CAMEROON: KIPA ALIYEONDOLEWA KAMBINI ASTAAFU KUICHEZEA TIMU YA TAIFA
Andre Onana (26) anayeichezea #InterMilan aliondolewa Kambini wakati #Cameroon ikishiriki Kombe la Dunia 2022 baada ya kutofautiana na kocha wake, Rigobert Song
Soma https://jamii.app/Onana
#JFSports

😁11👍7
UEFA: CHELSEA VS REAL MADRID, MAN CITY VS BAYERN MUNICH
Droo ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imepangwa, #RealMadrid ni dhidi ya #Chelsea wakati #ManchesterCity itavaana na #BayernMunich
Mechi nyingine #Benfica dhidi ya #InterMilan, #ACMilan ikivaana na #Napoli
Mechi za raundi ya kwanza zitachezwa Aprili 11 na 12, 2023, marudio ni Aprili 18 na 19, 2023

😁7❤2👍2
UEFA: MAN CITY YAIZUIA REAL MADRID KUFURUKUTA
-
#RealMadrid imeshindwa kuutumia vizuri Uwanja wa #SantiagoBernabéu baada ya kulazimishwa sare ya goli 1-1 katika mechi ya kwanza ya Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya
-
Timu mwenyeji ilitangulia kupata goli kupitia kwa #ViníciusJúnior kisha #ManchesterCity ikasawazisha kupitia kwa #KevinDeBruyne
-
Timu hizo zitarudiana Mei 17, 2023 wakati Nusu Fainali nyingine itazikutanisha #ACMilan dhidi ya #InterMilan (Mei 10, 2023)
-
#JFSports #JamiiForums

❤4👍2
MAN CITY YATWAA UBINGWA WA FA KWA KUIPIGA 2-1 MAN U
#ManchesterCity imefanikiwa kubeba kombe la pili msimu wa 2022/23 kwa kuifunga #ManchesterUnited magoli 2-1 katika Fainali ya #FACup iliyopigwa kwenye Uwanja wa #Wembley
Magoli ya City yamewekwa wavuni na #İlkayGündoğan huku #BrunoFernandes akiifungia United
City imesaliwa na mchezo mmoja wa Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya #InterMilan, ikishinda itaweka rekodi kama ya United ya Mwaka 1999 ya kubeba Mataji makubwa matatu likiwemo la #PremierLeague

👍3❤1
MAN. UNITED, INTER MILAN ZAAFIKIANA USAJILI WA ONANA
Inaelezwa makubaliano yaliyofikiwa ni kumuuza Kipa huyo wa #InterMilan, #AndreOnana kwa Pauni Milioni 43 (Tsh. Bilioni 137) ili kuchukua mikoba ya David De Gea ambaye ameondoka United baada ya kudumu kwa miaka 12
Onana pia ameshakubaliana mahitaji yake binafsi na #ManchesterUnited, akitarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitano
United inatarajiwa kumtangaza raia huyo wa #Cameroon, leo Julai 17, 2023 ambapo pia uongozi unashughulikia suala la visa ili akajiunge na wenzake waliopo ziarani Nchini Marekani
Soma https://jamii.app/OnanaToUnited

❤4👍3
#TETESI: Mshambuliaji #RomeluLukaku Raia wa Ubelgiji anatarajiwa kutua AS Roma kwa mkopo wa Tsh. Bilioni 16 kuungana na #JoseMourinho aliyewahi kuwa Kocha wake miaka kadhaa iliyopita
#Chelsea imekubali ofa ya Tsh. Bilioni 15 badala ya Tsh. Bilioni 25 iliyotaka awali ili kumruhusu Lukaku (30) kwenda kwa mkopo ambapo pia atalazimika kupunguza mshahara wake anaolipwa kwa sasa Tsh. Bilioni 1 kwa wiki
Awali, #InterMilan ilitaka kumsajili baadaye ikajitoa katika mchakato, #Juventus nayo ilionesha nia lakini mashabiki wa timu hiyo waliandamana wakidai hawamtaki. Aidha, Lukaku alikataa ofa ya kuhamia #AlHilal ya #SaudiArabia
Soma https://jamii.app/LukakuRoma

👏5👍2
#MICHEZO: Straika wa zamani wa Brazil, Ronaldo Nazario De Lima ambaye pia amewahi kuchezea Klabu za #Barcelona, #RealMadrid, #InterMilan, #ACMilan ametaja kikosi chake bora cha muda wote wakiwemo #LionelMessi na #CristianoRonaldo
Kikosi hiko ni; 1. Gianluigi Buffon 2. Cafu 3. Roberto Carlos 4. Fabio Cannavaro 5. Paolo Maldini 6. Zinedine Zidane 7. Pele 8. Diego Maradona 9. Ronaldo de Lima 10. Lionel Messi na 11. Cristiano Ronaldo
Unadhani nani mwingine alistahili kuingia kwenye kikosi hiki au kuwekwa benchi?
Soma https://jamii.app/C9Team

👍8
Mabingwa wa Ligi Kuu ya Ufaransa ‘Ligue 1’, Paris Saint-Germain (#PSG) wameonesha huu ni mwaka wao, kwa kubeba taji la #UEFAChampionsLeague (Ligi ya Mabingwa Ulaya), pia kushusha kipigo Kizito kwa #InterMilan ya Italia, Magoli 5-0
PSG inayonolewa na Kocha Luis Enrique, imebeba taji hilo kwa magoli ya Achraf Hakimi (12), Désiré Doué (20, 63), Khvicha Kvaratskhelia (73) na Senny Mayulu (86)
Huo unakuwa ubingwa wa kwanza kwa timu ya Ufaransa katika michuano hiyo
Soma https://jamii.app/UEFAFinal25

🔥1
MICHEZO: Uongozi wa Klabu ya #Fenerbahçe ya Uturuki umemfuta kazi kocha José Mourinho, ambaye amedumu klabuni hapo kwa msimu mmoja pekee.
Mourinho ni miongoni mwa makocha wakubwa Dunia ambaye amewahi kufundisha #Chelsea, #ManchesterUnited, #RealMadrid, #InterMilan, #TottenhamHotspur, #ASRoma na alikuwa maarufu kwa mbinu zake za mifumo ya ulinzi pamoja na kubeba makombe mbalimbali.
Sababu ya kufukuzwa kwake ni kushindwa kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya, kushindwa kutwaa taji lolote msimu uliopita na kushindwa kushindana na Galatasaray ambao ni wapinzani wakubwa wa Fenerbahçe.
Zaidi Soma https://jamii.app/MourinhoLigi
#JFSports #JamiiForums #JamiiAfrica