JamiiForums
✔
23.9K subscribers
40.7K photos
3.6K videos
34.7K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
ETHIOPIA: #TIGRAY YAKOSA HUDUMA YA INTANETI KWA SIKU ZAIDI YA 300

Huduma hiyo imekosekana tangu kuanza kwa mzozo Novemba 2020

Kukosekana kwa Intaneti kumesababisha Matukio ya Ukiukwaji wa #HakiZaBinadamu kushindwa kurekodiwa

Soma - https://jamii.app/TigrayInternetOff

#InternetAccess
ETHIOPIA: Mamlaka zimerejesha huduma za Kimtandao baada ya kufungia Mitandao ya #Facebook, #Telegram, #TikTok na #YouTube tokea Februari 9, 2023 kufuatia mvutano kati ya Serikali na Kanisa la #Orthodox

Kwa Miezi 5 wale tu waliokuwa wanatumia VPN ndio walioweza kuingia kwenye majukwaa ya Mitandao ya Kijamii, hivyo kuzidisha matumizi ya vifurushi vya #Internet

Soma https://jamii.app/MitandaoEthiopia

#JamiiForums #DigitalRights #InternetAccess #HakiZaKidigitali #Governance #JFDigitali
👍2❤1🤔1
#DIGITALRIGHTS: Agosti 10, 2023 Tanzania ilizindua Mkongo wa Baharini wa Intaneti #2Africa, wenye urefu wa Kilomita 45,000 unaounganisha Mabara ya Ulaya, (kupitia Misri), Asia, (kupitia Saudi Arabia) na Afrika, hivyo kufanya nchi kuwa na Mikongo Mitatu ya Bahari inayofanya kazi, mingine ikiwa ni #EASSy na #SEACOM

Akizungumza katika uzinduzi, Rais Samia amesema Mkongo huo utaongeza Ushindani kwa watoa Huduma za Intaneti ambapo utaongeza Ubora wa Huduma za Mtandao na hata kupunguza gharama, hivyo kuboresha Sekta ya Digitali Nchini

Soma https://jamii.app/MkongoWaBaharini

#JamiiForums #DigitalWorld #HakiZaKidigitali #InternetAccess
👍11
Kwa mujibu wa Mtandao wa cable.co.uk Watumiaji wa #Intaneti katika Nchi nyingi za Afrika wanakabiliwa na gharama kubwa za Mtandao, Miundombinu isiyo thabiti pamoja na huduma isiyo nzuri ikiwemo Kasi ndogo ya Intaneti

Licha ya takwimu za ufikiaji wa Huduma za Intaneti kuonesha Watumiaji wa Intaneti Barani Afrika walifikia Milioni 570 hadi Desemba 2022, bado ni 43.1% tu ya Watu wanapata huduma hiyo Afrika wakati wastani wa Kimataifa ni angalau iwe 66.2%.

#JamiiForums #FIFAfrica23 #InternetFreedomAfrica #DigitalRights #HakiZaKidijitali #InternetAccess #JFDATA
👍4❤2