JamiiForums
✔
23.9K subscribers
40.7K photos
3.61K videos
34.7K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MYANMAR YAFUNGA HUDUMA YA INTANETI

- Jeshi la #Myanmar limeamuru leo kufungwa kwa huduma za Intaneti nchini humo

- Aidha, Serikali imevifungia Vyombo vyote vya Habari isipokuwa vichache vinavyomilikiwa na Jeshi

Soma https://jamii.app/NoInternetMyanmar

#InternetShutdown #InternetShutdowns
#DEMOKRASIA: Pakistan imezuia Huduma ya #Internet kwa Simu za Mkononi wakati zoezi la kupiga kura lilipoanza leo Februari 8, 2024 katika Uchaguzi Mkuu, huku Wizara ya Mambo ya Ndani ikisema uamuzi huo ni kutokana na hali mbaya ya Usalama Nchini humo

Siku moja kabla ya Uchaguzi, (Februari 7, 2024) mabomu Mawili yalilipuka na kuuwa Watu takriban 28 karibu na Ofisi za Wagombea, hivyo kuongeza hofu kwamba vituo vya kupigia kura vinaweza kulengwa na kushambuliwa

Kabla ya Uchaguzi, Wakosoaji walitoa tahadhari kuwa kuzuia Intaneti kunaweza kudhoofisha juhudi za Chama cha Waziri Mkuu wa zamani, #ImranKhan cha #Pakistan Tehreek-e-Insaf (#PTI) kinachotegemea sana Mitandao ya Kijamii kueneza Jumbe na Siasa zake

Soma https://jamii.app/PakistanElections

#JamiiForums #PakistanElections #KeepItOn #InternetShutDowns #Democracy #Governance
👍1