JamiiForums
✔
23.9K subscribers
40.7K photos
3.61K videos
34.7K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
LONDON: Meneja wa Klabu ya Manchester City, #PepGuardiola, amesema Uwekezaji unaofanywa na Saudi Arabia katika Soka unaanza kubadili Soko la Usajili na kuleta Changamoto mpya na ngumu katika Soka la Ulaya

Kauli hiyo inafuatia Winga raia wa Algeria na Ufaransa, #RiyadMahrez kujiunga na Al-Ahli ikiwa ni mwendelezo wa Mastaa wakubwa wa Soka kuanza kutimkia katika Ligi ya Saudi Pro iliyowachukua mastaa kama #CristianoRonaldo, Karim Benzema, N'Golo Kante na Jordan Henderson

Soma https://jamii.app/SaudiPro

#JamiiForums #JFSports #SaudiProLeague
👍5❤2
ENGLAND: Mchezaji #KevinDeBruyne amepata majeraha ya Paja wakati #ManchesterCity ikishinda Magoli 3-0 dhidi ya #Burnley katika mchezo wa kwanza wa #PremierLeague 2023/24
-
Kocha wa City, #PepGuardiola amesema Bruyne amepata maumivu kwenye Misuli ya Paja na Madaktari watamfanyia vipimo kujua ukubwa wa tatizo, hivyo atakuwa nje ya uwanja kwa wiki kadhaa

Soma https://jamii.app/DeBruyneOut

#JFSports #JamiiForums
👍9
GUARDIOLA AANGUA KICHEKO ALIPOULIZWA KUHUSU KIWANGO CHA MAN. UNITED

Kocha wa #ManchesterCity, #PepGuardiola ametoa kicheko hicho wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu kiwango cha Wapinzani wao wa Jadi, #ManchesterUnited jinsi walivyoanza Msimu wa 2023-24

Baada ya kucheka, Guardiola akasema “Hawakuanza kama walivyotarajia, ni kama ilivyo kwa #Chelsea lakini siku zote wao ni Man. United na wale ni Chelsea. Muda si mrefu watapata mwendo mzuri”

United imepoteza mechi tatu kati ya tano za #PremierLeague

Soma https://jamii.app/GiardiolaUtd

#JFSports #JamiiForums
😁5❤1👍1
MAKOCHA WA KLABU WALIOTUMIA FEDHA NYINGI KUSAJILI

Orodha hii inaangalia Makocha waliotumia fedha nyingi kusajili Ngazi ya Klabu pamoja na Idadi ya Mataji waliyofanikiwa kubeba ikiwemo Ngao ya Jamii na Spanish Supercopa

#PepGuardiola wa #ManchesterCity anaongoza kuwa Kocha aliyetumia kiasi kikubwa cha fedha katika maisha ya ukocha. Ametumia Pauni Bilioni 1.75 kwa klabu zote alizotumikia ambazo inajumuisha akiwa #FCBarcelona, #BayernMunich na alipo sasa

Soma https://jamii.app/FransferFee

#JFSports #JamiiForums
❤5👍1
ENGLAND: Kocha #PepGuardiola anatarajiwa kuondoka ndani ya Klabu ya #ManchesterCity, mwishoni mwa msimu ujao wa 2024/25 mara baada ya mkataba wake kumalizika

Guardiola (52) aliyejiunga na Man City Mwaka 2016, amesaliwa na Miezi 12 katika mkataba wake na vyanzo vya Habari kutoka ndani ya klabu vinaeleza hataongeza mkataba mwingine

Kocha huyo ambaye amebeba makombe 15 likiwemo la #ChampionsLeague, pia amebeba mataji 6 ya #PremierLeague ikiwemo kuweka rekodi ya kuwa kocha wa kwanza kubeba ubingwa huo mara nne mfululizo

Soma https://jamii.app/GuariolaWithCity

#Sports #JamiiForums
👍5
ENGLAND: Kocha wa #ManchesterCity, #PepGuardiola amemjia juu Kocha wa #Arsenal, Mikel Arteta akimwambia ametangaza Vita dhidi ya pande hizo mbili, ikiwa ni mwendelezo wa kurushiana maneno baina ya pande hizo, baada ya matokeo ya sare ya Magoli 2-2 walipokutana Wikiendi iliyopita

Guardiola amesema “Wakati mwingine anapotaka kuizungumzia timu yetu awe muwazi sio kwa mafumbo, anaposema anajua kilichotokea Miaka Minne aliyokuwa hapa anamaanisha nini au ni kuhusu hukumu ya Makosa 115? Yawezekana anajua kilichotokea. Si wanataka Vita? Sasa tupo kwenye Vita.”

Pep ametoa kauli hizo baada ya Arteta kunukuliwa akisema walifanikiwa kuzima ‘Soka la Giza’ katika mechi dhidi ya City na kuwa anajua vitu vingi kwa muda aliokuwa mchezaji na kisha Kocha Msaidizi wa Guardiola

Soma https://jamii.app/PepArteta

#JFSports #JamiiForums #JFEPL24
🔥4👍3
ENGLAND: Licha ya kuwa mwanzoni mwa msimu ilielezwa kuwa Kocha #PepGuardiola ataondoka #ManchesterCity mwishoni mwa msimu wa 2024/25, inadaiwa kuna uwezekano wa Kocha huyo kusaini mkataba mpya wa Mwaka Mmoja kuendelea kuinoa timu hiyo

Guardiola (53) anayeelekea mwishoni mwa mkataba wake ambao unamalizika mwishoni mwa msimu huu, alitua City Mwaka 2016 na tangu wakati huo ameshinda mataji 18 yakiwemo ya Premier League (6), Champions League (1), FA Cups (2) na Club World Cup (1)

Soma https://jamii.app/GuardiolaContract

#JFSports #JamiiForums
👍2
ENGLAND: Mambo si mambo kwa Kocha #PepGuardiola, Timu yake ya #ManchesterCity ikiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Etihad imekubali kipigo cha magoli 4-0 kutoka kwa #TottenhamHotspur

Mchezo huo wa Ligi Kuu ya England "Premier League" unaifanya City kupoteza michezo mitano iliyopita, mingine ni dhidi ya Spurs (2-1), Bournemouth (2-1), Sporting (4-1), Brighton (2-1)

City pia inazidi kujiweka mbali na mbio za ubingwa, inashika nafasi ya pili kwa kuzidiwa pointi 5 na Liverpool ambayo ipo nyuma kwa mchezo mmoja.

#JFSports #JamiiForums #JFEPL24
❤2👍1
MICHEZO: Kocha wa #ManchesterCity, #PepGuardiola amesema anaamini #JoseMourinho ambaye kwa sasa ni Kocha wa Fenerbahçe anaitakia mabaya City na ikiwezekana ishushwe daraja

Awali, Guardiola alinukuliwa akisema yeye alibeba mataji sita ya Premier League tofauti na Mourinho aliyebeba matatu, kauli ambayo iliaminika kumkera Mourinho

Mourinho akajibu “Nataka kushinda, lakini ushindi uwe wa haki na safi, kama siwezi kushinda kwa haki bora nisishinde, ameshinda makombe sita, mimi matatu lakini sina kesi 115.”

Soma https://jamii.app/PepAndJose

#JFSports #JamiiForums
FA CUP: Kocha #PepGuardiola anaelekea kuukamilisha msimu wa 2025/26 vizuri licha ya kuwa alianza kwa kusuasua awali, hiyo ni baada ya kubeba taji la pili msimu huu, timu yake ya #ManchesterCity imeshinda goli 1-0 dhidi ya #Chelsea na kubeba Kombe la FA.

Antoine Semenyo ndiye amefunga goli pekee katika dakika ya 71 na kuifanya City kubeba taji la pili baada ya Carabao Cup.

Hivyo, Man City inakuwa imebeba taji la FA kwa mara ya nane, pia ikiwa imecheza fainali yake ya nne mfululizo katika kombe hilo, ikishinda mara mbili.

Zaidi https://jamii.app/CityBingwaFA2026

#JamiiForums #JFSports #JFAFCup2026