ENGLAND: Kocha wa #ManchesterCity, #PepGuardiola amemjia juu Kocha wa #Arsenal, Mikel Arteta akimwambia ametangaza Vita dhidi ya pande hizo mbili, ikiwa ni mwendelezo wa kurushiana maneno baina ya pande hizo, baada ya matokeo ya sare ya Magoli 2-2 walipokutana Wikiendi iliyopita
Guardiola amesema “Wakati mwingine anapotaka kuizungumzia timu yetu awe muwazi sio kwa mafumbo, anaposema anajua kilichotokea Miaka Minne aliyokuwa hapa anamaanisha nini au ni kuhusu hukumu ya Makosa 115? Yawezekana anajua kilichotokea. Si wanataka Vita? Sasa tupo kwenye Vita.”
Pep ametoa kauli hizo baada ya Arteta kunukuliwa akisema walifanikiwa kuzima ‘Soka la Giza’ katika mechi dhidi ya City na kuwa anajua vitu vingi kwa muda aliokuwa mchezaji na kisha Kocha Msaidizi wa Guardiola
Soma https://jamii.app/PepArteta
#JFSports #JamiiForums #JFEPL24

🔥4👍3
MICHEZO: Ligi Kuu ya England “Premier League” inaendelea leo Jumamosi Oktoba 5, 2024, vigogo kadhaa wapo uwanjani, wakiwemo #Liverpool, #Arsenal na #ManchesterCity
#JFSports #JFEPL24 #JamiiForums
#JFSports #JFEPL24 #JamiiForums
👍2
MICHEZO: Mbio za kuwania Ubingwa wa Ligi Kuu England “#PremierLeague” zinazidi kuwa ngumu kwa #Chelsea na #Arsenal baada ya timu hizo kutoka sare ya goli 1-1 kwenye Uwanja wa Stanford Bridge
Arsenal ndio ilianza kufunga katika dakika ya 60 kupita kwa Gabriel Martinelli, Chelsea ikasawazisha katika dakika ya 70, mfungaji akiwa ni Pedro Neto
Baada ya matokeo hayo, Chelsea imebaki nafasi ya 3, Arsenal ikiwa nafasi ya 4 huku timu zote zikiwa na pointi 19 na zimecheza mechi 11 kila moja
#JFSports #JamiiForums #JFEPL2024

❤1
Goli lililofungwa na Martin Ødegaard dakika ya 2 lilikuwa na baraka ya kuifanya #Arsenal kushusha mvua ya Magoli 5-1 dhidi ya #ManchesterCity katika Ligi Kuu ya England "#PremierLeague" kwenye Uwanja wa Emirates
Magoli mengine yamewekwa wavuni na Thomas Partey, Lewis Skelly, Kai Havertz na Ethan Nwari, huku City ikipata goli lake kupitia kwa Erling Haaland. Ikumbukwe mchezo uliopita baina ya timu hizo ulimalizika kwa sare ya 2-2
Arsenal imefikisha pointi 50, nyuma ya #Liverpool inayoongoza Ligi, ikiwa na alama 56 huku City imebaki nafasi ya 4 ikiwa na pointi 41
Soma https://jamii.app/ArsenalWin5
#JamiiForums #JFEPL25 #JFSports

UHISPANIA: Kipa wa #FCBarcelona, Wojciech Szczesny amesema anasubiri mwongozo wa Mkewe na Familia yake kabla ya kusaini Mkataba mpya wa kuendelea kubaki Klabuni hapo au kuondoka
Kipa huyo wa zamani wa Arsenal, alisajiliwa Oktoba 2024 ikiwa ni Mwezi mmoja tangu atangaze kustaafu akitokea Juventus, alipewa nafasi hiyo baada ya kipa chaguo la kwanza Marc-Andre ter Stegen kuumia goti
Szczesny na Luczenko walifunga Ndoa Mwaka 2016 baada ya kuwa kwenye uhusiano kwa Miaka mitatu, walikutana wakati akiwa anaichezea #Arsenal
Soma https://jamii.app/SzczesnyTransfer
#JamiiForums #JFSports #Michezo

ENGLAND: Timu ya #ManchesterUnited imeanza vibaya msimu wa 2025/26 kwa kukubali kichapo cha Goli 1-0 kutoka kwa Arsenal kwenye Uwanja wa Old Trafford ikiwa ni mchezo wa kwanza kwa timu hizo katika Premier League.
Goli pekee limewekwa wavuni na beki Riccardo Calafiori akimalizia mpira wa kona dakika ya 13.
Mechi ijayo ya United ni dhidi ya Fulham (Agosti 24, 2025), #Arsenal itavaa Leeds United (Agosti 23, 2025).
#JamiiForums #JamiiAfrica #JFSports #JFEPL2025

MICHEZO: Wikiendi inaelekea kumalizika, haya ni baadhi ya matokeo katika Ligi na Michuano mbalimbali Duniani.
Ngazi ya klabu, timu kutoka Jiji la Manchester hazijapata ushindi, moja imepigwa nyingine imepata sare, #Arsenal, #Chelsea, #BayernMunich zote zimepata ushindi mnono.
Tembelea JamiiForums.com kushiriki kwenye mijadala mbalimbali inayohusu Soka.
#JFSports #JamiiForums #JFEPL2025 #JamiiAfrica #CHAN2024 #JFBundesliga2025

MICHEZO: Timu ya #LiverpoolFC imeitandika Arsenal Goli 1-0 katika mwendelezo wa Ligi Kuu ya England (#EPL) kwenye Uwanja wa Anfield, leo Agosti 31, 2025. Goli pekee likifungwa na Dominik Szoboszlai raia wa Hungary katika dakika ya 83.
Hivyo, Liverpool imefikisha alama 9 baada ya kushinda mechi 3 mfululizo iliwemo dhidi ya Bournemouth na Newcastle United huku #Arsenal ikisaliwa na alama 6 baada ya kupata ushindi katika mechi mbili dhidi ya Manchester United na Leeds United ambao ni wageni wa ligi msimu huu.
Zaidi https://jamii.app/AnfieldTasa
#JFSports #JamiiForums #JamiiAfrica #JFEPL2025

❤3
MICHEZO: Wikiendi hii, mashabiki wa soka wanatarajia burudani ya hali ya juu! #Arsenal inakutana na #ManchesterUnited katika #EPL. Simba SC inapambana kufufua matumaini yao ya kupata angalau pointi kwa mara ya kwanza dhidi ya Espérance ya Tunisia katika Hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.
Timu yako itatoboa? Weka utabiri wako hapa...
Zaidi tembelea https://jamii.app/MechiKaliLeo
#JFSports #JamiiForums #Bundesliga #LaLiga #CAFCL2026

ENGLAND: Timu ya #ManchesterUnited imeendelea kuwa na matokeo mazuri chini ya Kocha Michael Carrick baada ya kuifunga #Arsenal Magoli 3-2 ikiwa ni wiki moja tangu ilipoifunga #ManchesterCity Magoli 2-0 katika #PremierLeague.
Matokeo ya mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Emirates yanapunguza nguvu ya Arsenal (pointi 50) katika mbio za kuwania ubingwa ambapo inaongoza ligi kwa tofauti ya alama 4 dhidi ya Man City (46) na Aston Villa (46) wakati Man United imepanda hadi nafasi ya nne ikiwa na alama 38.
Huo ni mchezo wa kwanza kwa Arsenal kupoteza msimu huu katika Premier League ikiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Emirates.
Zaidi tembelea https://jamii.app/MechiKaliLeo
#JamiiForums #JFSports #JFEPL

Je, unategemea nini kutoka kwenye timu yako Wikiendi hii?😎
Ligi mbalimbali Duniani zitaendelea, katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, #YangaSC na #SimbaSC zitakuwa kibaruani katika ardhi ya nyumbani.
Upande wa #EPL, vigogo #ManchesterUnited na #Arsenal nao watakuwa kazini, wakisaka alama muhimu kwenye mbio za msimamo wa ligi.
Zaidi https://jamii.app/MechiKaliWikiendi
#JFSports #JamiiForums #Bundesliga #LaLiga #CAFCL2026
Ligi mbalimbali Duniani zitaendelea, katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, #YangaSC na #SimbaSC zitakuwa kibaruani katika ardhi ya nyumbani.
Upande wa #EPL, vigogo #ManchesterUnited na #Arsenal nao watakuwa kazini, wakisaka alama muhimu kwenye mbio za msimamo wa ligi.
Zaidi https://jamii.app/MechiKaliWikiendi
#JFSports #JamiiForums #Bundesliga #LaLiga #CAFCL2026
❤1
Timu yako Itabagaza au Itabaragazwa?😃
Mashabiki wa Soka wanatarajia mitanange mikali wikiendi hii, kinara wa Premier League, #Arsenal, inakutana na #Sunderland, upande wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga SC ipo ugenini kucheza dhidi ya FAR Rabat ya Morocco katika Kundi B kutafuta nafasi ya kufuzu Robo Fainali.
Zaidi tembelea https://jamii.app/MechiKubwa
#JamiiForums #JFSports #Bundesliga #LaLiga #CAFCL2026

ENGLAND: Timu ya #Arsenal imeendelea kasi ya kuutaka ubingwa wa Premier League 2025/26 kwa kushinda Magoli 3-0 dhidi ya Sunderland, hivyo kufikisha pointi 56 na kuendelea kutanua wigo wake wa kubaki nafasi ya kwanza katika msimamo wa Ligi.
Aston Villa ambayo ipo nafasi ya tatu ikiwa na alama 47 imelazimishwa sare ya 1-1 dhidi ya Bournemouth, upande wa Chelsea imefikisha pointi 43 ipo nafasi ya tano, imeshinda Magoli 3-1 dhidi ya Wolves
Zaidi tembelea https://jamii.app/ArsenalBingwa
#JamiiForums #JFSports #JFEPL2026

ENGLAND: Ushindi wa Magoli 2-1 dhidi ya #Chelsea unaifanya #Arsenal kuongoza msimamo wa #PremierLeague kwa tofauti ya pointi 5 dhidi ya Manchester City inayoshika nafasi ya pili, huku Chelsea ikibaki nafasi ya 6 kwa kuwa na alama 45.
Upande wa matokeo ya timu hizo kukutana ana kwa ana, Arsenal imeifunga Chelsea mechi ya tatu mfululizo, pia inakuwa imeshinda mechi 9 kati ya 13 zilizopita huku Chelsea ikiwa imeshinda mara moja na sare ni 3.
Zaidi https://jamii.app/MichezoJF
#JamiiForums #JFSports #JFEPL2026 #LondonDerby

ENGLAND: Ndoto za #Arsenal kubeba mataji manne msimu huu wa 2025/26 zimeyeyuka baada ya kupoteza Kombe la EFL (Carabao Cup) kwa kufungwa Magoli 2-0 na #ManchesterCity inayonolewa na Kocha Pep Guardiola katika Fainali iliyopigwa kwenye Uwanja wa Wembley, Machi 22, 2026.
Magoli yote yameweka wavuni na Nico O'Reilly dakika ya 60 na 64, hivyo kuifanya Arsenal inayonolewa na Mikel Arteta kubaki kwenye mataji matatu msimu huu ambayo ni Premier League, Ligi ya Mabingwa Ulaya na Kombe la FA.
Timu zilizotwaa Carabao Cup mara nyingi:
1. Liverpool - 10
2. Man City - 9
3. Man United - 5
4. Aston Villa - 5
5. Tottenham - 4
6. Nottingham - 4
7. Leicester City - 3
8. Arsenal - 2
9. Norwich City - 2
10. Birmingham – 2
Zaidi https://jamii.app/EFLCupFinal
#JamiiForums #JFSports #EFL2026

❤2
PREMIER LEAGUE: Timu ya #ManchesterCity imeshinda Magoli 3-0 dhidi ya #Chelsea, matokeo yanayoifanya kufikisha alama 64 katika mechi 31, ikiwa nafasi ya pili nyuma ya Arsenal yenye alama 70 katika michezo 32.
Mchezo ujao wa City itaivaa #Arsenal mnamo Aprili 19, 2026, ambapo mshindi wa hapo atakuwa na nafasi mzuri katika mbio za ubingwa msimu huu wa 2025/2026.
Baada ya matokeo hayo, Chelsea imebaki nafasi ya 6 ikiwa na alama 48 katika mechi 32.
Zaidi https://jamii.app/ChelseaVsManCityEPL

PREMIER LEAGUE: Licha ya kuongoza msimamo wa Ligi Kuu ya England, #Arsenal imeendelea kuwa na presha ya kuutafuta ubingwa baada ya kufungwa magoli 2-1 dhidi ya #ManchesterCity, ambapo sasa tofauti ya pointi baina ya timu hizo ni 3, huku City ikiwa na mchezo mmoja mkononi.
Matokeo hayo kwenye Uwanja wa Etihad yanaifanya City ambayo ipo nafasi ya pili kuwa na pointi 67 katika michezo 32, Arsenal bado inaongoza kwa kuwa na alama 70 katika michezo 33.
Mechi ijayo ya Arsenal ni dhidi ya Newcastle United (Aprili 25, 2026), City itaivaa Burnley (Aprili 22, 2026).
Zaidi https://jamii.app/ManCityVsArsenal

ENGLAND: Timu ya #Arsenal imefanikiwa kuingia Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuiondoa #AtleticoMadrid kwa jumla ya magoli 2-1 baada ya ushindi wa goli 1-0 katika mchezo wa pili uliopigwa kwenye Uwanja wa Emirates.
Timu hiyo ya London sasa inasubiri mshindi wa mchezo wa Bayern Munich dhidi ya Paris Saint-Germain FC kwa ajili ya Fainali inayotarajiwa kupigwa Mei 30, 2026.
Arsenal ambayo haijawahi kutwaa taji hilo ilifika Fainali mara ya mwisho Msimu wa 2005/6 ikiwa chini ya Kocha Arsene Wenger na kupoteza dhidi ya FC Barcelona kwa magoli 2-1 ambapo straika wa Barca, Samuel Eto’o akipata Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mechi.
Zaidi https://jamii.app/AtleticoVsArsenalUCL
#JamiiForums #JFSports #JFUEFA2026

HUNGARY: Kwa mara nyingine #Arsenal imepoteza taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya (#UEFAChampionsLeague) kwa kukubali kichapo cha penati 4-3 baada ya matokeo ya goli 1-1 katika dakika 120 kutoka kwa Paris Saint-Germain (#PSG) katika Fainali iliyopigwa kwenye Uwanja wa Puskas Arena, Mei 30, 2026.
Arsenal haijawahi kushinda taji hilo, hivyo inakuwa imepoteza fainali yake ya pili baada ya ile ya Mwaka 2006 dhidi ya Barcelona, pia imekwama kuweka rekodi ya kutwaa kwa pamoja UEFA pamoja na Premier League ambalo wamebeba Msimu wa huu 2025/26.
Upande wa PSG inabeba taji hilo mara ya pili na inafanya hivyo mara mbili mfululizo, kabla ya hapo ilifika Fainali Mwaka 2020 ikapoteza dhidi ya Bayern Munich.
Zaidi https://jamii.app/PSGBingwaUefa
#JamiiForums #JFSports #JFUCL2026 #UCL2026

Timu ya #Arsenal imeichakaza #ManchesterCity kwa magoli 3-0 katika mchezo wa Ngao ya Jamii kwenye Uwanja wa Principality, Cardiff, magoli yakifungwa na Riccardo Calafiori dakika ya 1, Kai Havertz (28) na Martin Ødegaard (48).
Ushindi huo ni mwendelezo mzuri wa matokeo kwa Arsenal ambayo ilitwaa ubingwa wa Premier League Msimu wa 2025/26.
Zaidi https://jamii.app/ArsenalMancity