JamiiForums
βœ”
23.9K subscribers
40.7K photos
3.61K videos
34.7K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
EPL: MAN. CITY, MAN. UTD ZAAMBULIA KICHAPO, ARSENAL YASHINDA

#ManchesterUnited ikiwa nyumbani Old Trafford imepoteza mchezo wa nne kwenye Ligi Kuu ya #England baada ya kufungwa goli 1-0 kutoka kwa Crystal Palace

#ManchesterCity nayo ikiwa ugenini kwa Wolverhampton imeambulia kichapo cha goli 2-1, ikiwa ni mchezo wa kwanza kwa Man. City kupoteza katika msimu huu wa Ligi Kuu England

#Arsenal imeshinda goli 4-0 dhidi ya Bournemouth na kufanya timu hiyo kukwea hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi. Arsenal, Liverpool na Tottenham zinasalia kuwa timu ambazo hazijapoteza mchezo kwenye Ligi hiyo

Baada ya kichapo, Man. Utd ipo nafasi ya 10 ikiwa na pointi 9 kwenye msimamo wa #EPL huku Man. City ikiendelea kushika usukani wa Ligi ikiwa na pointi 18

#JamiiForums #JFSports
πŸ‘6
ARSENAL 1-0 MAN. CITY: MWANAFUNZI AMFUNDISHA MWALIMU SOKA

Ushindi wa goli 1-0 likifungwa na Gabriel Martinelli limeifanya #Arsenal kupata furaha kwa mara ya kwanza kuifunga #ManchesterCity katika #PremierLeague tangu ilipofanya hivyo Desemba 21, 2015

Ushindi huo unaifanya Arsenal kushika nafasi ya pili nyuma ya #Tottenham licha ya kuwa timu zote zina pointi 20 wakati Man City ambayo imepoteza mechi mbili mfululizo za #EPL ipo nafasi ya tatu ikiwa na alama 18

Kabla ya mchezo wa Leo Oktoba 18, 2023, Man. City haikuwa imepoteza mchezo katika mechi 15 zilizopita dhidi ya Arsenal katika EPL

#JFSports #JamiiForums
πŸ‘8😁3❀1
MANCHESTER DERBY: MAN. UNITED YAPIGWA 3-0 KAMA IMESIMAMA

Magoli mawili ya Mshambuliaji #ErlingHaaland na moja la #PhilFoden yameifanya #ManchesterUnited itoke kinyonge kwenye Uwanja wake wa nyumbani wa Old Trafford kwa kufungwa 3-0

Mchezo huo wa #PremierLeague umenifanya Man. City ifikishe pointi 24 ikiwa nafasi ya 3 kwenye msimamo wakati United imebaki na alama 15 katika nafasi ya 8, timu zote zikiwa zimecheza mechi 10

#JFSports #EPL #JamiiForums
πŸ‘4😁4❀1πŸ‘1😒1
MAN. UTD YASHINDA 1-0, ARSENAL YAMBAMIZA MTU 3-1

Goli la Beki wa Kati #VictorLindelof limeiwezesha #ManchesterUnited kupata ushindi dhidi ya #Luton kwenye Uwanja wa Old Trafford ikiwa ni ushindi wa pili mfululizo kwa timu hiyo katika #PremierLeague

Matokeo hayo yameipeleka Man. United katika nafasi ya 6 kutoka ya 8 kwa kufikisha pointi 21

Mchezo mwingine, #Arsenal imepanda kutoka nafasi ya 4 hadi ya pili baada ya kuichapa #Burnley magoli 3-1

#JFSports #EPL #JamiiForums
πŸ‘5
#Everton imekatwa pointi 10 katika Ligi Kuu ya England (#PremierLeague) kwa kosa la kukiuka Kanuni ya Fedha (Faida na Uendelevu), hali ambayo ilitokea katika Msimu wa 2021/22

Baada ya kutangazwa kwa adhabu hiyo, uongozi wa Klabu ya Everton umesema utakata rufaa kwa kuwa adhabu hiyo imewashtua na imekuwa kali licha ya kudai waliwasilisha vielelezo wakati wa mchakato wa kesi hiyo ya ukiukwaji wa Kanuni

Kutokana na adhabu hiyo Everton ambayo ilikuwa na pointi 14 ikishika nafasi ya 14 katika Ligi imeshushwa hadi nafasi ya 19 ikiwa na pointi 4

Soma https://jamii.app/EvertonDeductedPoints

#JFSports #EPL #JamiiForums
❀2πŸ‘1
MICHEZO: #ManchesterCity imeendelea kushika usukani wa #PremierLeague kwa kufikisha pointi 29 licha ya kulazimishwa sare ya goli 1-1 katika mchezo dhidi ya #Liverpool yenye alama 28 kwenye Uwanja wa Etihad

Erling Haaland ameifungia City huku Alexander-Arnold akiisawazishia Liverpool

Baada ya filimbi ya mwisho Kocha wa City, Pep Guardiola na mshambuliaji wa Liverpool, Darwin Nunez walionekana kurushiana maneno huku chanzo kikiwa hakijajulikana

Soma https://jamii.app/CityLiver

#JFSports #EPL #JamiiForums
ENGLAND: Ikicheza mechi ya kwanza tangu ilipokatwa pointi 10 kutokana na kukiuka kanuni za Fedha katika #PremierLeague, Everton imeendelea kuwa na wakati mbaya kwa kuchapika magoli 3-0 kutoka kwa #ManchesterUnited

Waliopeleka furaha Man. United ni #AlejandroGarnacho, #MarcusRashford na #AnthonyMartial

United imefikisha pointi 24 ikiwa nafasi ya 6 katika #EPL huku #Everton ikibaki nafasi ya 19 kwa kuwa na alama 4

Soma https://jamii.app/EvertonManU

#JFSports #JamiiForums
πŸ‘5
MAN. UNITED IMECHEZEA KICHAPO KINGINE TENA EPL

Ikicheza mchezo wake wa 18 katika #PremierLeague msimu huu wa 2023/24, #ManchesterUnited imepoteza kwa magoli 2-0 dhidi ya #WestHamUnited, ikiwa ni mchezo wa 8 kupoteza katika Ligi hiyo

United ambayo imeshinda mchezo mmoja kati ya mitano iliyopita katika #EPL, inazidiwa pointi 11 na vinara wa Ligi, #Arsenal ambayo inatarajiwa kucheza baadaye dhidi ya #Liverpool

Mchezo ujao wa United ni dhidi ya #AstonVilla ambayo imekuwa na matokeo mazuri msimu huu ikishika nafasi ya pili

Soma https://jamii.app/WestHam2ManU0

#JFSports #JamiiForums
πŸ‘5❀1πŸ‘1😁1
ENGLAND: Msimu wa 2023/24 wa Ligi Kuu ya England "#PremierLeague" unaelekea mwishoni huku Timu nyingi zimesaliwa na Michezo 11. Kati ya Timu 20, zipo tatu ambazo zimejitenga katika mbio za kuwania ubingwa ambazo ni #Liverpool yenye pointi 63, #ManchesterCity (62) na #Arsenal (61)

Upepo ulivyo, unadhani Timu gani imesaliwa na ratiba ngumu na ipi ina nafasi kubwa ya kubeba ubingwa?

Soma https://jamii.app/Top3EPL24

#JFSports #JamiiForums #EPL
πŸ‘2
MICHEZO: Mechi moja imesalia kwa kila timu katika Ligi Kuu ya England β€˜Premier League’, mbio za ubingwa zimebaki kwa Timu Mbili tu za juu, #ManchesterCity ambaye ni Bingwa Mtetezi na #Arsenal

Je, Mdau karata yako inaangukia wapi, ni City ya Pep Guardiola kubeba taji kwa mara ya 4 mfululizo au Mikel Arteta kuipa Arsenal ubingwa wa kwanza #EPL baada ya Miaka 20?

Zaidi Soma https://jamii.app/EPLBingwa

#JFSports #JamiiForums
πŸ‘1
CHELSEA BADO INAJITAFUTA, KOCHA POCHETTINO AONDOKA KLABUNI HAPO

Kocha Mauricio Pochettino (52) aliyesaini kandarasi ya kuinoa #Chelsea kwa miaka miwili, anaondoka Klabuni hapo kwa makubaliano ya pande zote ikiwa ni mwaka mmoja tangu aanze kuinoa Klabu hiyo ya Magharibi mwa London

Klabu hiyo yenye Makazi yake katika Dimba la Stamford Bridge inatarajiwa kutafuta mrithi, ambapo Kieran McKenna, Sebastian Hoeness, Michel na Enzo Maresca wanatajwa kuwa miongoni mwa Makocha wanaoangaliwa kwa karibu

#Pochettino anayeiacha Chelsea katika nafasi ya 6 ya Ligi ya #EPL anakuwa Kocha wa tatu kuondoka The Blues chini ya Muunganiko wa Wamiliki unaoongozwa na Todd Boehly alipochukua timu hiyo Mei 2022. Makocha wengine ni Thomas Tuchel na Graham Potter

Zaidi Tembelea https://jamii.app/PochOutChelsea

#JamiiForums #JFSports
πŸ‘11πŸ‘Ž1πŸ”₯1
PREMIER LEAGUE: Liverpool inazidi kutengeneza njia ya kubeba Ubingwa wa #LigiKuu ya England baada ya kuifunga #ManchesterCity Magoli 2-0 kwenye Uwanja wa Anfield, wafungaji wakiwa ni Cody Gakpo na #MohammedSalah

Matokeo hayo yanaifanya City ambayo haijashinda Michezo 7 mfululizo kupoteza Michezo Minne mfululizo ya #EPL, huku ikizidiwa pointi 11 na #Liverpool

Liverpool ina alama 34 ikiwa inaongoza msimamo wa Ligi wakati City, bingwa mtetezi ipo nafasi ya 5 ikiwa na alama 23

#JFSports #JamiiForums #JFEPL24
❀2πŸ‘1
MICHEZO: Ligi Kuu ya England (Premier League - #EPL) inarejea leo Agosti 15, 2025 kuashiria rasmi kuanza kwa msimu wa 2025/2026, ufunguzi unatarajiwa kufanyika kwenye Uwanja wa Anfield kati ya bingwa mtetezi #Liverpool dhidi ya Bournemouth.

Kuna timu tatu ngeni kwenye Ligi ambazo zimepanda daraja msimu huu ambao ni Burnley, Leeds United na Sunderland, hiyo ni baada ya timu za Leicester City, Ipswich Town na Southampton kushuka daraja msimu uliopita.

Zaidi Soma https://jamii.app/LigiKuuUingereza

#JFSports #JamiiForums #JamiiAfrica #JFEPL2025
MICHEZO: Wikiendi hii moto wa soka unawashwa Ulaya na Afrika. Kutakuwa na burudani kutoka Ligi Kuu ya England (#EPL), (#Bundesliga), (#LaLiga) pamoja na Michuano ya CHAN 2024.

Unadhani timu yako itafanya maajabu au itakuwa kama Man United?

Zaidi https://jamii.app/MechiZaMoto

#JFSports #JamiiAfrica #JamiiForums #EPL #Bundesliga #LaLiga #CHAN2024
❀2
MICHEZO: Timu ya #LiverpoolFC imeitandika Arsenal Goli 1-0 katika mwendelezo wa Ligi Kuu ya England (#EPL) kwenye Uwanja wa Anfield, leo Agosti 31, 2025. Goli pekee likifungwa na Dominik Szoboszlai raia wa Hungary katika dakika ya 83.

Hivyo, Liverpool imefikisha alama 9 baada ya kushinda mechi 3 mfululizo iliwemo dhidi ya Bournemouth na Newcastle United huku #Arsenal ikisaliwa na alama 6 baada ya kupata ushindi katika mechi mbili dhidi ya Manchester United na Leeds United ambao ni wageni wa ligi msimu huu.

Zaidi https://jamii.app/AnfieldTasa

#JFSports #JamiiForums #JamiiAfrica #JFEPL2025
❀3
MICHEZO: Wikiendi hii moto wa soka unawaka Ulaya na Afrika, burudani kutoka Ligi Kuu ya England (#EPL), (#Bundesliga), (#LaLiga), na fainali ya AFCON 2025 kati ya Senegal dhidi ya Morocco.

Je, timu yako itafanya maajabu? Weka utabiri wako hapa

Zaidi tembelea https://jamii.app/RatibaYaMechi

#JFSports #JamiiForums #EPL #Bundesliga #LaLiga #AFCON2025
❀1
MICHEZO: Wikiendi hii, mashabiki wa soka wanatarajia burudani ya hali ya juu! #Arsenal inakutana na #ManchesterUnited katika #EPL. Simba SC inapambana kufufua matumaini yao ya kupata angalau pointi kwa mara ya kwanza dhidi ya EspΓ©rance ya Tunisia katika Hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.

Timu yako itatoboa? Weka utabiri wako hapa...

Zaidi tembelea https://jamii.app/MechiKaliLeo

#JFSports #JamiiForums #Bundesliga #LaLiga #CAFCL2026
Je, unategemea nini kutoka kwenye timu yako Wikiendi hii?😎

Ligi mbalimbali Duniani zitaendelea, katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, #YangaSC na #SimbaSC zitakuwa kibaruani katika ardhi ya nyumbani.

Upande wa #EPL, vigogo #ManchesterUnited na #Arsenal nao watakuwa kazini, wakisaka alama muhimu kwenye mbio za msimamo wa ligi.

Zaidi https://jamii.app/MechiKaliWikiendi

#JFSports #JamiiForums #Bundesliga #LaLiga #CAFCL2026
❀1
ENGLAND: Arsenal, vinara wa Ligi Kuu England (#EPL), wamepoteza mchezo huo kwa mabao 2-1 dhidi ya Bournemouth katika dimba la Emirates. Arsenal inabaki na alama 70 baada ya michezo 32, huku wapinzani wao wa karibu, Manchester City, wakiwa na alama 61 na michezo 30.

Kupoteza huko kumeongeza presha katika mbio za ubingwa, hasa wakati tofauti ya alama ikiendelea kupungua kadri ligi inavyoelekea ukingoni.

Mchezo ujao wa Arsenal itaivaa Manchester City katika mwendelezo wa ligi hiyo.

Fuatilia mjadala huu https://jamii.app/ArsenalWashikwaBega

#JamiiForums #JFSports #JFEPL2026
🀣2
ENGLAND: Mechi nyingine za Ligi Kuu (#EPL) leo Aprili 12, 2026

Crystal Palace Vs Newcastle Utd
πŸ“ Dimba la Selhurst Park - Saa 10 Jioni

Nottingham Forest Vs Aston Villa
πŸ“ Uwanja wa The City Ground - Saa 10 Jioni

Sunderland Vs Tottenham Hotspur
πŸ“ Uwanja wa Uwanja wa Light - Saa 10 Jioni

Bofya kushiriki mjadalaπŸ‘‰πŸΎ https://jamii.app/ChelseaVsManCityEPL

#JamiiForums #JFSports #JFEPL2026