JamiiForums
✔
23.9K subscribers
40.7K photos
3.61K videos
34.7K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Mchezo wa #ManchesterCity dhidi ya #Arsenal umekamilika kwa suluhu ya 0-0 kwenye Uwanja wa Etihad, matokeo ambayo yanaiwezesha Liverpool kuongoza Msimamo wa #PremierLeague

Arsenal imefikisha pointi 65 na hivyo kushuka hadi nafasi ya Pili ilifuatiwa na Man. City yenye alama 64

#Liverpool ambayo imeshinda 2-1 dhidi ya Brighton inaongoza msimamo kwa kuwa na pointi 67

Soma https://jamii.app/CityArsenal

#JFSports #JamiiForums
👍12❤2
#MICHEZO: Kocha wa #Liverpool, #JurgenKlopp ametoa kauli hiyo baada ya matokeo ya magoli 2-2 ya timu yake dhidi ya #ManchesterUnited katika #PremierLeague, akielezea sababu za mchezo baina ya timu hizo huwa unakuwa mgumu kwake hata kama United haina kiwango kizuri kwa wakati huu

Rekodi za Liverpool ya Klopp dhidi ya Man United ikiwa chini ya Kocha Erik ten Hag zipo hivi:

FA Cup (Machi 17, 2024)
Man. United 4-3 Liverpool

EPL (Desemba 12, 2023)
Liverpool 0-0 Man. United

EPL (Machi 5, 2023)
Liverpool 7-0 Man. United

EPL (Agosti 22, 2022)
Man. United 2-1 Liverpool

Kirafiki (Julai 12, 2022)
Man. United 4-0 Liverpool

Soma https://jamii.app/ManULiver

#JFSports #JFNukuu #JamiiForums
❤3👍2
TETESI: Wakati msimu wa 2023/24 ukielekea ukingoni inadaiwa #FCBarcelona ina mpango wa kumuuza Mshambuliaji wake, Robert Lewandowski mwishoni mwa msimu huu na nafasi yake kuchukuliwa na Straika wa #Liverpool, Darwin Nunez

Uamuzi huo umekuja baada ya Barcelona kushuhudia wapinzani wao wa jadi, #RealMadrid wakitwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Uhispania (#LaLiga)

Lewandowski (35) amesaliwa na miaka miwili katika mkataba wake lakini Barcelona inataka kumuuza ili kupunguza gharama kubwa za mishahara ambazo klabu hiyo inapambana nazo

Soma https://jamii.app/NunezToBarca

#JFSports #JamiiForums
ENGLAND: #ManchesterCity imefanikiwa kutwaa Ubingwa wa #PremierLeague baada ya kuifunga #WestHamUnited magoli 3-1 na kuweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kubeba taji hilo mara 4 mfululizo
-
Ushindi huo umeifanya City kufikisha pointi 91, ikifuatiwa na #Arsenal yenye alama 89 baada ya kushinda magoli 2-1 dhidi ya #Everton katika michezo ya kukamilisha Msimu wa 2023/24
-
Timu ya #Liverpool ambayo imemuaga kocha wake, Jürgen Klopp imemaliza ikiwa nafasi ya 3 kwa pointi 82, #AstonVilla ni ya 4 kwa kuwa na pointi 68
-
Staa wa #ManCity, #ErlingHaaland ameibuka Mfungaji Bora kwa kufikisha magoli 27. Upande wa pili Timu zilizoshuka Daraja ni Sheffield United, Burnley na Luton Town
-
#JFSport #JamiiForums
👍7🔥4
MAN. UNITED YATWAA FA CUP KWA KUIFUNGA MAN CITY 2-1

#ManchesterUnited imefanikiwa kubeba Ubingwa wa #FACup 2024 kwa kuifunga #ManchesterCity katika Fainali kwa magoli 2-1 kwenye Uwanja wa Wembley Jijini London

Magoli ya Alejandro Garnacho na Kobbie Mainoo yameiwezesha United kubeba kombe hilo kwa mara ya 13, mara ya mwisho kulibeba ilikuwa Mwaka 2016, huku City ambayo iliyopewa nafasi kubwa ya kushinda imepata goli kupitia kwa Jeremy Doku

Kipigo hicho ni kama United imelipa kisasi kwa kuwa msimu uliopita ilifungwa na wapinzani haohao katika Fainali ya FA kwa magoli 2-1

Timu zilizobeba FA Cup mara nyingi ni #Arsenal (14), Man. United (13), #Chelsea (8), #Liverpool (8), #TottenhamHotspur (8), Man. City (7) na #AstonVilla (7)
-
#JFSports #JamiiForums
🔥7👍6❤2🤨1
ENGLAND: Timu ya #ManchesterCity imeukaribisha Msimu wa 2024/25 kwa kushinda Ngao ya Jamii mbele ya Wapinzani wao wa Jadi, #ManchesterUnited kwa ushindi wa penati 7-6

Hadi dakika 90 matokeo yalikuwa 1-1, United iliyopata nafasi nyingi za wazi ikashindwa kutumia vizuri ilitangulia kwa goli la Alejandro Garnacho kisha Bernardo Silva akasawazisha

Ushindi huo umeifanya #ManCity kufikisha Ngao ya 7

Timu zilizoshinda Ngao mara nyingi ni Man. United (21), #Arsenal (17), #Liverpool (16), #Everton (9), Spur (7) na Chelsea (4)

#JFSports #CommunityShield24 #JamiiForums
👍1
ENGLAND: Beki wa Kati na Nahodha wa #Liverpool, Virgil van Dijk (33) amesema licha ya kuwa Mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa Msimu wa 2024/25, hajapata mkataba mpya hali ambayo inaonesha dalili kuwa inawezekana maisha yake yasiwe marefu kikosini hapo

Mbali na Van Dijk, mastaa wengine wa timu hiyo ambao mikataba yao imebakisha Miezi 11 kumalizika ni mshambuliaji #MohamedSalah (32) na Trent Alexander-Arnold (25) ambao wote ni Manahodha Wasaidizi

Wachambuzi wa Soka wanaamini inawezekana Kocha mpya wa Liverpool, Arne Slot ameanza kutengeneza kikosi chake, hivyo wachezaji hao hawamo kwenye mipango ya muda mrefu

Soma https://jamii.app/VanDijk

#JFSports #JamiiForums
👍3❤1👎1
MICHEZO: Klabu za Hispania, #RealMadrid na #FCBarcelona zinaendelea kumfuatilia kwa ukaribu Beki wa Pembeni wa #Liverpool, Trent Alexander-Arnold (25), ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa Msimu wa 2024/25

Inadaiwa, Liverpool ipo tayari kumpa Mkataba mpya utakaomfanya alipwe Pauni 180,000 (Tsh. Milioni 619) kwa Wiki na kama hataridhia hilo, anaweza kuuzwa au kubaki hadi mwisho wa msimu ili aondoke akiwa Mchezaji huru

Taarifa za Watu wa karibu na Beki huyo zinaeleza kuwa anaweza kujiunga na Real Madrid ili aungane na rafiki yake, Jude #Bellingham

Soma https://jamii.app/TrentTransfer

#JFSports #JamiiForums
👍1
MICHEZO: Kiungo Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na #Liverpool, Alex Oxlade-Chamberlain ambaye msimu uliopita aliitumikia Besiktas, inadaiwa yupo mbioni kurejea katika #PremierLeague

Timu ya Brentford inadaiwa ipo katika hatua za mwisho za mazungumzo ya kumsajili

Oxlade-Chamberlain ni mmoja kati ya Wachezaji 9 ambao wamewekwa sokoni na Besiktas ambayo msimu uliopita ilishika nafasi ya 6 katika Ligi Kuu ya Uturuki "Super Lig"

Soma https://jamii.app/Chamberlain

#JFSports #JamiiForums
#PREMIERLEAGUE: Kocha wa #ManUnited, Erik ten Hag ameendelea kukiweka kibarua chake mashakani, baada ya timu yake kukubali kichapo cha Magoli 3-0 kutoka kwa #Liverpool, kwenye Uwanja wa Old Trafford

Huo unakuwa Mchezo wa Pili kupoteza kati ya Mitatu iliyopita tangu kuanza kwa Msimu wa 2024/25, ambapo magoli yamewekwa wavuni na Luis Diaz (Mawili) na Mohamed Salah, ambaye amefunga mfululizo katika mechi 7 zilizopita alizocheza Old Trafford

Licha ya kubeba Kombe la FA msimu uliopita, #ManU chini ya Ten Hag ilikuwa na matokeo mabaya katika michuano mingine ikiwemo Premier League (nafasi ya 8), hivyo matokeo ya leo yanaongeza presha ya ajira yake klabuni hapo

#JFSports #JamiiForums #JFEPL24
👍1
MICHEZO: Ligi Kuu ya England “Premier League” inaendelea leo Jumamosi Oktoba 5, 2024, vigogo kadhaa wapo uwanjani, wakiwemo #Liverpool, #Arsenal na #ManchesterCity

#JFSports #JFEPL24 #JamiiForums
👍2
PREMIER LEAGUE: Liverpool inazidi kutengeneza njia ya kubeba Ubingwa wa #LigiKuu ya England baada ya kuifunga #ManchesterCity Magoli 2-0 kwenye Uwanja wa Anfield, wafungaji wakiwa ni Cody Gakpo na #MohammedSalah

Matokeo hayo yanaifanya City ambayo haijashinda Michezo 7 mfululizo kupoteza Michezo Minne mfululizo ya #EPL, huku ikizidiwa pointi 11 na #Liverpool

Liverpool ina alama 34 ikiwa inaongoza msimamo wa Ligi wakati City, bingwa mtetezi ipo nafasi ya 5 ikiwa na alama 23

#JFSports #JamiiForums #JFEPL24
❤2👍1
Goli lililofungwa na Martin Ødegaard dakika ya 2 lilikuwa na baraka ya kuifanya #Arsenal kushusha mvua ya Magoli 5-1 dhidi ya #ManchesterCity katika Ligi Kuu ya England "#PremierLeague" kwenye Uwanja wa Emirates

Magoli mengine yamewekwa wavuni na Thomas Partey, Lewis Skelly, Kai Havertz na Ethan Nwari, huku City ikipata goli lake kupitia kwa Erling Haaland. Ikumbukwe mchezo uliopita baina ya timu hizo ulimalizika kwa sare ya 2-2

Arsenal imefikisha pointi 50, nyuma ya #Liverpool inayoongoza Ligi, ikiwa na alama 56 huku City imebaki nafasi ya 4 ikiwa na pointi 41

Soma https://jamii.app/ArsenalWin5

#JamiiForums #JFEPL25 #JFSports
ENGLAND: Wachezaji wa #Liverpool, Mohamed Salah na Trent Alexander-Arnold wamerushiana maneno wakati wakiwa mazoezini, hali iliyofanya wenzao kuingilia na kuwatenganisha kwa kuwa walionekana wakisogeleana huku kila mmoja akimrushia maneno mwenzake

Tukio hilo limetokea muda mfupi kuelekea mchezo wa 16 Bora wa UEFA Champions League dhidi ya #PSG, ambapo baada ya muda walitenganishwa. Liverpool haijatoa tamko lolote kuhusu tukio hilo

Mechi dhidi ya PSG ni ya marudio baada ya awali Liverpool kushinda 1-0, michezo mingine ya leo Machi 11, 2025: Barcelona vs Benfica, Bayer Leverkusen vs Bayen Munich, Inter Milan vs Feyernoord

Soma https://jamii.app/SalahArnold

#JFSports #JamiiForums
Miaka ya kusubiri imeisha kwa #NewcastleUnited, baada ya kuifunga Liverpool goli 2-1 katika Uwanja wa Wembley na kufanikiwa kushinda Kombe la EFL kwa mara ya kwanza katika histori ya Kombe hilo

Mwaka 1969, ilikuwa mara ya mwisho kwa Newcastle kushinda Kombe ambapo ilishinda Kombe dogo la Inter-Cities Fairs. Aidha, imepita miaka 70 tangu timu hiyo ishinde Kombe kubwa ambapo mwaka 1955 ilishinda Kombe la FA

#Liverpool imepoteza mechi mfululizo kwa mara ya kwanza katika msimu huu, na hivyo kukosa nafasi ya kuongeza Kombe la 10 la michuano hiyo. Timu hiyo sasa inawania kushinda kombe la Ligi peke yake kwa msimu huu

Zaidi, tembelea https://jamii.app/NewcastleEFL25

#JamiiAfrica #Sports
TANZIA: Nyota wa #Liverpool, #DiogoJota (28) amefariki Dunia kutokana na ajali ya gari iliyotokea Nchini Uhispania ikiwa ni wiki mbili tangu afunge ndoa na Rute Cardoso, ambapo Wanandoa hao wana Watoto watatu

Taarifa zinaeleza ajali hiyo imetokea wakati akisafiri kwa gari akiwa na mdogo wake Andre (26) ambaye naye amepoteza maisha baada gari lao kuacha njia, na kwenda kugonga sehemu na kisha kuwaka moto

Winga huyo raia wa Ureno enzi za uhai wake alipata nafasi ya kucheza katika timu kadhaa; Paços de Ferreira, Atlético Madrid, Porto, Wolverhampton Wanderers kisha akatua Liverpool Mwaka 2020

Soma https://jamii.app/RIPDiogoJota

#JamiiForums #JFSports #RIPDiogoJota
MICHEZO: Ligi Kuu ya England (Premier League - #EPL) inarejea leo Agosti 15, 2025 kuashiria rasmi kuanza kwa msimu wa 2025/2026, ufunguzi unatarajiwa kufanyika kwenye Uwanja wa Anfield kati ya bingwa mtetezi #Liverpool dhidi ya Bournemouth.

Kuna timu tatu ngeni kwenye Ligi ambazo zimepanda daraja msimu huu ambao ni Burnley, Leeds United na Sunderland, hiyo ni baada ya timu za Leicester City, Ipswich Town na Southampton kushuka daraja msimu uliopita.

Zaidi Soma https://jamii.app/LigiKuuUingereza

#JFSports #JamiiForums #JamiiAfrica #JFEPL2025
ENGLAND: Timu ya #ManchesterCity imeendelea kupambana kubaki katika mbio wa ubingwa wa #PremierLeague baada ya kuifunga #Liverpool Magoli 2-1 kwenye Uwanja wa Anfield, hivyo kufikisha pointi 50 ikiwa nafasi ya pili nyuma ya Arsenal yenye alama 56.

Upande wa Liverpool imebaki nafasi ya 6 ikiwa na alama 39, nafasi ya tatu ipo Aston Villa (47), Manchester United ni ya nne kwa kuwa na pointi 44, Chelsea ina alama 43 katika nafasi ya tano.

Zaidi tembelea https://jamii.app/MechiKubwa

#JamiiForums #JFSports #JFEPL2026
❤2
UEFA: Timu ya #FCBarcelona imetupwa nje ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya 2025/2026 licha ya kushinda magoli 2-1 dhidi ya #AtleticoMadrid ambayo imefuzu Nusu Fainali kwa jumla ya magoli 3-2.

Mchezo mwingine Paris Saint-Germain (#PSG) imeingia Nusu Fainali pia kwa kuifunga #Liverpool goli 2-0, ushindi wa jumla ukiwa ni magoli 4-0.

Zaidi
https://jamii.app/LiverBarcaUefa

#JamiiForums #JFSports #JFUEFA2026
ENGLAND: Timu ya #ManchesterUnited imetandika #Liverpool magoli 3-2 katika mchezo wa Premier League, leo Mei 3, 2026 ushindi ambao unaifanya Uniyed kujihakikishia nafasi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao wa 2026/27.

Man United imefikisha pointi 64 ikiendelea kubaki nafasi ya tatu, Liverpool imesalia nafasi ya nne ikiwa na alama 58,  huku kila upande ukiwa umesaliwa na michezo mitatu.

Zaidi https://jamii.app/ManUtdVsLiverpool

#JamiiForums #JFSports #JFEPL2026
❤1