JamiiForums
✔
23.9K subscribers
40.7K photos
3.61K videos
34.7K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DIGITALI: Iwapo utakutana na taarifa zako zisizo sahihi au usizotaka ziwepo Mtandaoni wasiliana na Tovuti husika ili ziondolewe

Kumbuka, taarifa zako zinaweza kutumika vibaya kama kuiba utambulisho na kupunguza faragha na siri zako. Aidha, Walaghai wa Mtandaoni wanaweza kutumia taarifa hizo kukufanyia ulaghai na kukuibia

Soma https://jamii.app/TaarifaZakoMitandaoni

#DigitalSafety #DigitalSecurity #CyberSecurityAwarenessMonth #SecureOurWorld
👍2
DIGITALI: Kufuatilia uwekwaji na uchapishaji wa taarifa zako Mtandaoni kupitia ‘Google Alerts’ ni njia mojawapo ya kuboresha usalama na kujilinda mtandaoni

‘Google Alerts’ zinaweza kukusaidia kugundua matumizi mabaya ya taarifa zako au kugundua unapotajwa katika Tovuti hatari

Kupitia ‘Google Alerts’ unaweza kuripoti matumizi mabaya ya taarifa zako na pia kuchukua hatua ya kulinda taarifa zako

Soma https://jamii.app/GoogleAlertsDigitalSecurity

#JamiiForums #DigitalSafety #DigitalSecurity #CyberAwarenessMonth #SecureOurWorld
👍1
DIGITALI: Mdau kumbuka kuzima kifaa chako kama Kompyuta na Simu ili kulinda taarifa zako binafsi dhidi ya Wadukuzi.

Iwapo hutazima kifaa chako taarifa zako binafsi zinaweza kuangukia katika mikono isiyo salama na zikatumika kufanya vitendo vya kihalifu kama kuiba utambulisho na kupunguza faragha yako

Soma https://jamii.app/ZimaKifaaChako

#JamiiForums #DigitalSafety #DigitalSecurity #CyberAwarenessMonth #SecureOurWorld
DIGITALI: Kuruhusu Programu kupata taarifa binafsi kama vile Eneo, Kamera na Namba za Simu kunaweza kuwa na madhara, kwani Programu hizo zinaweza kukusanya na kutumia taarifa zako binafsi

Pia, inaweza kuongeza matumizi ya data na kupelekea chaji ya simu kuisha haraka, kwani Programu inapata ruhusa za kutumia vipengele vingi zaidi kuliko vinavyohitajika

Aidha, kuna Programu ambazo haziwezi kufanya kazi bila kuwa na ruhusa za baadhi ya taarifa zako, kwa mfano Google Maps inashauriwa kuchagua "Ruhusu wakati tu wa kutumia Programu" (Allow only while using the app) ili uweze kutumia programu hiyo

Soma https://jamii.app/IdhinishaRuhusaProgramu

#JamiiForums #DigitalSafety #DigitalSecurity #CyberAwarenessMonth #SecureOurWorld
❤1👍1
DIGITALI: Taarifa unazoweka mitandaoni haziwezi kusahaulika, hata kama umeamua kuzifuta, hivyo, ni muhimu kuwa makini na jinsi unavyotumia mitandao ya kijamii

Kumbuka kuwa taarifa unazochapisha zinaweza kutumiwa kuiba utambulisho wako, kufanya ulaghai, au hata kudukuliwa

Pia, ni muhimu kuwa makini na kile unachochapisha, kwani waajiri wanaweza kukufuatilia mitandaoni. Taarifa zisizofaa zinaweza kukupotezea nafasi ya ajira

Soma https://jamii.app/MatumiziMakiniMitandao

#JamiiForums #DigitalSafety #DigitalSecurity #CyberSecurityAwarenessMonth #SecureOurWorld
❤2👍1
DIGITALI: Sera ya Faragha (Privacy Policy) ni maelezo ya kina kuhusu jinsi taarifa binafsi zinavyokusanywa, zinavyochakatwa, kutumika na kulindwa katika Programu ya Simu au Tovuti husika

Wakati mwingine Sera za Faragha hutumika kupata Taarifa zako Binafsi ili kufanya Ulaghai Mtandaoni, Uwizi wa Utambulisho na Vitendo vingine vya Kihalifu Mtandaoni

Soma https://jamii.app/KuelewaSeraZaFaragha

#JamiiForums #DigitalSafety #DigitalSecurity #CyberSecurityAwarenessMonth #SecureOurWorld
👍1
DIGITALI: Ni muhimu kufuta au kufunga programu ambazo huzitumii au zilizopitwa na wakati kwani zinaweza kuendelea kukusanya taarifa zako

Programu ambazo hazijatumika kwa muda mrefu zina hatari kubwa zaidi ya kushambuliwa na wadukuzi au kuvujisha taarifa binafsi

Aidha, kifaa chako kitaenda kwa kasi zaidi endapo programu na faili zisizotumika zitafutwa

Soma https://jamii.app/DeleteUnusedApps

#JamiiForums #DigitalSafety #DigitalSecurity #CyberSecurityAwarenessMonth #SecureOurWorld
DIGITALI: Watoa Huduma huruhusu kujiandikisha kwenye Biashara zao kwa kutumia akaunti zako za Mtandaoni kama vile Google

Kwa kufanya hivi baadhi ya taarifa zako na shughuli zako Mtandaoni zinaweza kufikiwa na kuwa katika hatari ya kudukuliwa

Soma https://jamii.app/AvoidLinkingAccounts

#JamiiForums #DigitalSafety #DigitalSecurity #CyberSecurityAwarenessMonth #SecureOurWorld
#DIGITALI: Ulinzi na Usalama wa Mtandaoni si kwa Watu binafsi tu—pia ni muhimu kwa wenye Biashara na Kampuni sababu Mashambulizi ya kimtandao kwa Biashara au Taasisi yanaweza kuwa na madhara makubwa, ikiwa ni pamoja na wizi wa data, athari za kisheria na uharibifu wa muda mrefu wa sifa

Kampuni zinapaswa Kuwekeza katika kutoa Mafunzo kwa Wafanyakazi kwasababu Mashambulizi mengi ya kimtandao huanza na makosa ya kibinadamu

Kwa kuelimisha Wafanyakazi jinsi ya kutambua ulaghai wa Kimtandao, usimamizi mzuri wa nywila na kushughulikia data kwa usalama, biashara zinaweza kupunguza hatari ya mashambulizi kufanikiwa

Soma zaidi https://jamii.app/CSAMonth

#CybersecurityAwarenessMonth #JamiiForums #DigitalSecurity #DigitalSafety #SecureOurWorld #JFDigitali
👍3
#DIGITALI: Watengenezaji wa Programu Tumizi (Application) hugundua Madhaifu ya kimfumo mara kwa mara na kutoa masasisho ili kufanya Mifumo hii ya Kidigitali kuwa salama zaidi

Moja ya sababu muhimu za kusasisha programu za Kidigitali ni kuziba mianya ya Kiusalama. Kadri muda unavyosonga, Wadukuzi hugundua njia mpya za kutumia hivyo usipofanya Usasishaji (Updates) mara kwa mara unajiweka kwenye hatari ya kupata mashambulizi ya Kimtandao

Soma zaidi https://jamii.app/DeviceUpdates

#CybersecurityAwarenessMonth #JamiiForums #DigitalSecurity #DigitalSafety #SecureOurWorld #JFDigitali #CyberCrime #StaySafeOnline
Jifunze na ufahamu kuhusu hatari za mashambulio ya Mtandaoni na jinsi ya kujikinga nayo ikiwemo yanayoweza kufanywa kwa kutumia mbinu za 'phishing' na 'malware'

Kabla ya kutumia Huduma mpya ya Mtandaoni, hakikisha unaangalia Sera zao za faragha ili ujue jinsi wanavyokusanya, kutumia, na kulinda taarifa zako.

Soma zaidi https://jamii.app/OnlineSafety

#CybersecurityAwarenessMonth #JamiiForums #DigitalSecurity #DigitalSafety #SecureOurWorld #JFDigitali #CyberCrime #StaySafeOnline