JamiiForums
βœ”
23.9K subscribers
40.7K photos
3.6K videos
34.7K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Kama umetumiwa SMS ya kitapeli, tuma ujumbe uliotumiwa kwenda 15040 kisha ingiza namba ya simu iliyokutumia na kama umepigiwa simu ya kitapeli tuma neno UTAPELI kwenda 15040 kisha ingiza namba ya simu iliyokupigia

Mjadala zaidi https://jamii.app/KuripotiNambaUtapeli

#JamiiForums #UtapeliMtandaoni #BewareOfScams #CyberSecurity #DigitalSafety #KataaUtapeliMtandaoni #KuwaMachoNaUtapeli
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
SONGWE: Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprisca Mahundi, amesema kuwa Serikali inakusudia kuanza kuwataja watu wanaojihusisha na uhalifu mtandaoni, ikiwemo wale wanaosambaza ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu za mkononi wakitaka watumiwe fedha kupitia namba zao.

Amesema hatua hiyo inalenga kudhibiti uhalifu wa mtandaoni ambao umekuwa ukiongezeka, hasa katika sekta ya mawasiliano

Ameyasema hayo leo Machi 2025 wakati akikagua hali ya mawasiliano katika mpaka wa Tanzania na Zambia, Mjini Tunduma

Soma https://jamii.app/MatapeliMtandaoniKutajwa

#JamiiForums #KuwaMachoNaUtapeli #DigitalSafety #DigitalWorld #Governance
πŸ‘1
Mdau, huwa unazingatia vitu gani kabla ya kununua bidhaa au huduma Mtandaoni ili kuepuka kutapeliwa?

Mjadala zaidi https://jamii.app/BiasharaUtapeliMtandaoni

#JamiiForums #UtapeliMtandaoni #BewareOfScams #CyberSecurity #DigitalSafety #KataaUtapeliMtandaoni #KuwaMachoNaUtapeli
Mdau wa Jukwaa la 'Tech, Gadgets & Science' ameelezea mbinu mbalimbali za kuepuka kutapeliwa Mtandaoni

Mdau, unazingatia nini ili kujiadhari na Matapeli wa mtandaoni?

Mjadala zaidi https://jamii.app/KuepukaKutapeliwaMtandaoni

#JamiiForums #UtapeliMtandaoni #BewareOfScams #CyberSecurity #DigitalSafety #KataaUtapeliMtandaoni #KuwaMachoNaUtapeli
Endapo utapokea ujumbe kama huu usiuzingatie, pia usifuate maelekezo kutoka kwa mtu anayejitambulisha kama mtoa huduma wa Mtandao wako wa simu, kwani Watoa Huduma wa Mitandao ya simu Nchini huwasiliana na wateja kwa namba 100 pekee

Mjadala zaidi https://jamii.app/ZuiaUtapeliMtandaoni

#JamiiForums #UtapeliMtandaoni #BewareOfScams #CyberSecurity #DigitalSafety #KataaUtapeliMtandaoni #KuwaMachoNaUtapeli
Mdau wa Jukwaa la Habari na Hoja Mchanganyiko ndani ya JamiiForums.com ameelezea kisa chake cha kutapeliwa Mtandaoni baada ya kununua kifurushi cha Intaneti Mtandaoni kwa Mtu asiyemfahamu

Mdau umewahi kukutana na tukio kama hili?

Mjadala zaidi https://jamii.app/NimetapeliwaTena

#JamiiForums #UtapeliMtandaoni #BewareOfScams #CyberSecurity #DigitalSafety #KataaUtapeliMtandaoni #KuwaMachoNaUtapeli
πŸ‘1
Mdau wa Jukwaa la Habari na Hoja Mchanganyiko ndani ya JamiiForums.com ameshauri badala ya kupiga namba *106# ili kuangalia namba zilizosajiliwa kwa namba ya NIDA, mhusika wa namba atumiwe ujumbe wa SMS kila namba mpya inaposajiliwa ili kupunguza tatizo la Utapeli Mtandaoni.

Unakubaliana na Mdau huyu?

Mjadala zaidi https://jamii.app/UjumbeBadalaya106

#JamiiForums #UtapeliMtandaoni #BewareOfScams #CyberSecurity #DigitalSafety #KataaUtapeliMtandaoni #KuwaMachoNaUtapeli
❀1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
MOROGORO: Oparesheni Maalum ya Jeshi la Polisi Mkoa iliyofanyika Julai 2 hadi 11, 2025 imebaini Mtandao wa uhalifu wa kimtandao unaojulikana kama β€œHalo Halo”, na kufanikisha kukamatwa kwa Watu 21 wanaodaiwa kuhusika na utapeli.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Alex Mkama amesema Watuhumiwa hao walikamatwa katika maeneo mbalimbali, wakitumia mbinu tofauti, ikiwemo kusajili laini nyingi za simu kwa kutumia majina ya Watu wengine kupitia Mawakala wa kujitegemea.

Kamishna Alex aliongeza kwa kusema baadhi ya Watuhumiwa hao walikuwa wakijitambulisha kama Maafisa wa Makampuni ya simu, Waganga wa Kienyeji au Wafanyabiashara wa Pembejeo za Kilimo na Chakula cha Mifugo

Soma zaidi: https://jamii.app/MatapeliMtandaoniWakamatwa

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFDigitali #DigitalSafety #Accountability


Video: Azam TV
❀1
Mara nyingi vitu vya bure si salama, vinaweza kuja na gharama kubwa zinazoweza kukuathiri.

Kuwa makini unapojiunga na Wi-Fi ya bure. Ni muhimu kuchukua tahadhari ili kulinda taarifa zako zilizo kwenye vifaa kama simu au 'laptop'.

Kupitia Wi-Fi ya bure, mdukuzi anaweza kuiba taarifa zako binafsi, nywila (password) zako na hata kudukua mawasiliano yako.

Mdau, huwa unazingatia nini unapotaka kujiunga na Wi-Fi za bure?

Zaidi soma https://jamii.app/UsipendeWiFiZaBure

#JamiiAfrica #JamiiForums #DataPrivacy #DataProtection #DigitalSafety
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
MBEYA: Kamanda wa Polisi Mkoa, Benjamin Kuzaga amesema wanawashikilia Watu Tisa kwa tuhuma za kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kupitia Mitandao ya Kijamii ikiwemo Facebook na WhatsApp, ambapo Watuhumiwa hao walikamatwa Agosti 18, 2025 katika maeneo ya Nsalala na Mapelele, Mbalizi.

Kamanda Kuzaga ameeleza kuwa Watuhumiwa hao walitumia mbinu mbalimbali ikiwemo kutangaza nafasi feki za ajira, kuwatapeli Watu kwa kutumia simu na mitandao kwa mtindo wa β€œTuma kwenye namba hii,” na kuwarubuni wengine wachangie fedha kujiunga na Kampuni ya Q NET yenye asili ya Malaysia.

Amewataja waliokamatwa ni Nemia Njonga (23), Ombeni Ambilikile (22), Jacob Peter (23), Baraka Mgala (22), Lusajo Jeremiah (45), Adili Mbeyale (19), Shaban Yasin (23), Ester Kimaro (28) na Abdi Awadhi (21).

Zaidi soma https://jamii.app/WakamatwaUtapeli

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFDigitali #DigitalSafety #Accountability
❀1
Mdau huwa unachukua hatua gani unapopeleka simu yako kwa fundi kwa ajili ya matengenezo?

Mjadala zaidi https://jamii.app/HatariYaFundiSimu

#JamiiAfrica #JamiiForums #DataPrivacy #DataProtection #JFDigitali #DigitalSafety
❀1
Kampuni ya Meta yashtakiwa Mahakamani kwa madai ya kusoma mazungumzo ya WhatsApp na kuvunja faragha za Watumiaji wa Mtandao huo, upande wa Meta umesema kesi hiyo haina msingi na watawachukulia hatua za Kisheria dhidi ya mawakili wa walalamikaji.

Aidha, Malalamiko hayo pia yanataja kuwepo kwa whistleblowers (watoa taarifa wa ndani) waliosaidia kufichua taarifa hizi, ingawa hayafafanui ni akina nani.

Mjadala zaidi https://jamii.app/WhatsAppKusomaMessageWateja

#JamiiForums #DigitalSafety #TaarifaZakoNiZako #DataPrivacy #DigitalWorld
Kabla ya kubonyeza 'Kukubali' (Accept), hakikisha unasoma na kuelewa Sera ya Faragha (Privacy Policy) ili ujue jinsi taarifa zako binafsi zinavyokusanywa, kuchakatwa na kutumika.

Soma https://jamii.app/FaraghaYaTaarifa

#JamiiForums #DigitalSafety #TaarifaZakoNiZako #DataPrivacy
Bodi ya Ulinzi wa Taarifa Barani Ulaya (DPAs) imesema inaipa kipaumbele agenda ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi za Watoto, ikieleza rika hilo lipo katika hatari zaidi Mtandaoni kuliko Watu Wazima.

Zaidi Soma https://jamii.app/DataPrivacy2026

#JamiiForums #DigitalSafety #TaarifaZakoNiZako #DataPrivacy #ChildRights
Mshiriki wa Shindano la Stories of Change Msimu wa Pili (2022) alishauri kuwe na Sera na Utaratibu Maalum wa Ufungaji wa Kamera za 'CCTV' ili kudhibiti ukusanyaji wa Taarifa Binafsi.

Alidai Kupost Taarifa Binafsi kama namba ya Simu, anwani ya Makazi, Picha na Video za Faragha kunakuweka hatarini kufanyiwa Vitendo vya Ukatili Mtandaoni.

Kusoma andiko lote https://jamii.app/DhibitiUfungajiHolelaCCCTV

#JamiiForums #DigitalSafety #TaarifaZakoNiZako #DataPrivacy #StoriesOfChangeS2
❀1
Mshiriki wa Stories Of Change Mwaka 2023 alisema kutokana na wimbi la matukio ya Watu kutapeliwa na taarifa zao binafsi kutumika kuwadhalilisha na Taasisi/Vikundi vya kukopesha, ni muhimu Serikali kutoa elimu kwa Wananchi namna ya kujiepusha.

Kusoma andiko lote https://jamii.app/KukopeshaPesa

#JamiiForums #DigitalSafety #TaarifaZakoNiZako #DataPrivacy
CHINA: Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) limebaini uwepo wa takribani kamera 180 za siri ndani ya vyumba vya hoteli mbalimbali ambazo hutumika kurekodi wageni bila wao kufahamu na kisha kuuza video hizo kupitia mtandao wa Telegram.

Mdau, una tabia ya kukagua chumba cha hoteli au gesti unayofikia kabla ya kupumzika?

Zaidi: https://jamii.app/KameraZaSiri

#JamiiForums #DigitalSafety #TaarifaZakoNiZako #DataPrivacy
❀1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Meneja wa Huduma kwa Wateja na Watumiaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (#TCRA), Kadaya Baluhye amewataka waathirika wa unyanyasaji mitandaoni, ikiwemo uvujaji wa picha za utupu, kutoa taarifa Jeshi la Polisi ili waweze kupata msaada unaostahili bila kuona aibu. Amesema hayo Februari 10, 2026, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Usalama Mtandaoni kwenye Ukumbi wa Auditorium, Chuo Kikuu cha Dodoma (#UDOM).

Zaidi https://jamii.app/ZikivujaTaarifu

#JamiiForums #DigitalSafety #TaarifaZakoNiZako #DataPrivacy