#MICHEZO: Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC) imetoa adhabu kwa Bondia Hassan Mwakinyo kutojihusisha na Mchezo wa Ngumi nje na ndani ya #Tanzania kwa muda wa mwaka mmoja pamoja na Faini ya Tsh. Milioni 1
Mwakinyo amekutwa na hatia ya kutoa kauli chafu dhidi ya Uongozi wa #TPBRC pamoja na kugomea pambano dhidi ya Bondia Julius Indongo kutoka #Namibia lililopangwa kufanyika Septemba 29, 2023, Dar es Salaam
Siku moja kabla ya uamuzi huo, Mwakinyo aliandika, "Nilielewa mapema sana huu mchezo mchafu, nia ovu pamoja na dhamira zenu na hatma iliyotengenezwa kwa thamani ya pesa, nafikiri sasa bila kupepesa macho tunalazimika kuweka vitu wazi wazi hadharani kwenye hili, ili inapotokea tena ishu kama hii kuwe na adabu ya maamuzi hususani kwenye mchezo wetu, ni kweli pesa inaweza nunua haki na utu wa mtu lakini hio ni kwa mtu 'boya' asiyejuwa thamani na haki zake za msingi, see you soon."
Soma https://jamii.app/MwakinyoBan
#JamiiForums #JFSports #Boxing

👍6
MICHEZO: Serikali imeufuta Uongozi wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (#TPBRC) baada ya kukumbwa na tuhuma mbalimbali ambapo uchunguzi umebaini ulikuwa na mapungufu ya kiutendaji ikiwemo Matumizi mabaya ya Madaraka, matumizi mabaya ya Fedha na ukiukwaji wa Utawala Bora
Taarifa ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi, imeeleza Mei 8, 2024, Waziri aliunda Kamati Maalum ya Uchunguzi ambayo imejidhihirisha juu ya tuhuma hizo chini ya Rais wa Kamisheni hiyo, Chaurembo Palasa
Waziri ameelekeza hatua zaidi za kisheria zichukuliwe dhidi ya Viongozi walioondolewa Madarakani, ili kuweka fundisho kwa Viongozi wengine wa Vyama na mashirikisho na Michezo Nchini.
Soma https://jamii.app/TPBRC
#JFSports #JamiiForums #Accountability