JamiiForums
✔
23.9K subscribers
40.7K photos
3.61K videos
34.7K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MAREKANI: Taarifa kutoka The Associated Press (AP) kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Marekani zinaonesha Rais wa zamani, #DonaldTrump anaongoza kwa idadi ya Kura ambazo hutumika kuamua mshindi wa Urais (Electoral Votes)

Takwimu za awali zinaonesha Trump ana 'Electoral Votes' 247 huku Makamu wa Rais, Kamala Harris akiwa na 210, ambapo yeyote kati yao ili awe Mshindi atahitaji kupata Kura 270

Aidha, Kura za Wananchi hadi kufikia Saa 3 Asubuhi (EAT), zinaonesha Kamala amepata Kura 61,291,377 (47.4%) huku Trump akiongoza kwa Kura 66,074,641 (51.1%)

Soma https://jamii.app/USDecides

#JamiiForums #Democracy #Governance #CivilRights #USElection2024 #USDecides
👍4❤1
Aliyekuwa Rais wa 45 wa Marekani, #DonaldTrump ametangaza kushinda tena Urais wa Taifa hilo kwa takriban 51.2% ya kura dhidi ya 47.4 % za Kamala Harris na hivyo kuwa Rais wa 47 akitarajia kurejea Ikulu ya #WhiteHouse

Hadi sasa Trump amefikisha Kura za Wajumbe (Electoral Votes) 267 kati ya 270 zinazotakiwa, huku Kamala akiwa na Kura 224. Kwa upande wa Kura za Wananchi Trump ana 68,654,143 na Kamala ana 63,558,470

Soma https://jamii.app/TrumpWins

#JamiiForums #Democracy #Governance #CivilRights #USElection2024 #USDecides
👍3❤1
Aliyekuwa Rais wa 45 wa Marekani (2017-2021), Mfanyabiashara Donald #Trump ameshinda nafasi ya Urais wa taifa hilo kwa takriban Kura 71,837,960 dhidi ya Kura 66,779,589 za Kamala Harris

Ushindi wa Trump ambaye ni Mwanachama wa Republican, unakuja ikiwa ni Miaka Minne tangu aliposhindwa Urais dhidi ya Joe Biden katika Uchaguzi wa mwaka 2020

Aidha, katika Uchaguzi huu Chama cha Republican kimefanikiwa kupata Viti 52 vya Bunge la Seneti, Viti 198 vya Bunge la Congress na Viti 27 vya Magavana wa Majimbo

Soma https://jamii.app/TrumpWins

#JamiiForums #Democracy #Governance #CivilRights #USElection2024 #USDecides
👍3
DEMOKRASIA: Wananchi wa Marekani wamechagua Viongozi watakaoongoza taifa hilo kwa Miaka 4 kuanzia nafasi ya Urais, ambapo Donald Trump amerejea madarakani baada ya kupoteza nafasi hiyo mwaka 2020

Aidha, takwimu zilizoripotiwa na vyombo mbalimbali zimeonesha Kamala Harris ameangushwa katika Kura za Wananchi pamoja na Kura za Wajumbe wa Majimbo (Electoral Votes)

Soma https://jamii.app/TrumpWins

#JamiiForums #Democracy #Governance #CivilRights #USElection2024 #USDecides
🫡3
MAREKANI: Muda mfupi baada ya kushinda Urais katika Uchaguzi uliofanyika Novemba 5, 2024, Rais Mteule, Donald Trump ameripotiwa kuanza mipango ya namna atakavyotekeleza Sera zake baada ya kuapishwa

Kwa mujibu wa Mtandao wa Associated Press (AP), baadhi ya Sera hizo ni Kujenga Ukuta wa kuzuia Wahamiaji kutoka Mexico, Kushusha viwango vya Kodi za Makampuni na Kuweka Sheria za udhibiti wa Masuala ya uhusiano wa Jinsia ya Moja

Sera nyingine ni pamoja na kupunguza ushiriki wa taifa hilo katika masuala ya Kijeshi kwenye mataifa mengine

Soma https://jamii.app/DT100Days

#JamiiForums #Democracy #Governance #CivilRights #USElection2024 #USDecides
👍2❤1