MAREKANI: Wagombea wa Nafasi ya Urais, #KamalaHarris wa Democratic na #DonaldTrump wa Republican wamekutana katika mdahalo kwa mara ya kwanza ikiwa ni wiki 8 kabla ya Uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Novemba 5, 2024 ambapo kila upande umetamba kuwa umefanya vizuri kuliko mwingine
Trump anasema “Harris ameahidi kufanya mambo mengi mazuri, kwanini hajafanya sasa? Wamekuwa katika uongozi kwa Miaka mitatu na nusu, wamekuwa na muda wa kufanya yote hayo aliyoahidi ikiwemo ajira lakini hawajafanya. Binafsi ulikuwa Mdahalo wangu bora.”
Harris amesema "Nitakuwa Rais ambaye nitalinda Haki za Msingi na Uhuru, ikiwemo Haki ya Mwanamke kufanya maamuzi yake na mwili wake na sio kuwa suala la Serikali kumwambia nini cha kufanya.”
Soma https://jamii.app/KamalaTrump
#JamiiForums #TrumpVsKamala #Democracy #USElections #USPresidentialDebate #JFDemokrasia

👍4
MAREKANI: Taarifa kutoka The Associated Press (AP) kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Marekani zinaonesha Rais wa zamani, #DonaldTrump anaongoza kwa idadi ya Kura ambazo hutumika kuamua mshindi wa Urais (Electoral Votes)
Takwimu za awali zinaonesha Trump ana 'Electoral Votes' 247 huku Makamu wa Rais, Kamala Harris akiwa na 210, ambapo yeyote kati yao ili awe Mshindi atahitaji kupata Kura 270
Aidha, Kura za Wananchi hadi kufikia Saa 3 Asubuhi (EAT), zinaonesha Kamala amepata Kura 61,291,377 (47.4%) huku Trump akiongoza kwa Kura 66,074,641 (51.1%)
Soma https://jamii.app/USDecides
#JamiiForums #Democracy #Governance #CivilRights #USElection2024 #USDecides

👍4❤1
Aliyekuwa Rais wa 45 wa Marekani, #DonaldTrump ametangaza kushinda tena Urais wa Taifa hilo kwa takriban 51.2% ya kura dhidi ya 47.4 % za Kamala Harris na hivyo kuwa Rais wa 47 akitarajia kurejea Ikulu ya #WhiteHouse
Hadi sasa Trump amefikisha Kura za Wajumbe (Electoral Votes) 267 kati ya 270 zinazotakiwa, huku Kamala akiwa na Kura 224. Kwa upande wa Kura za Wananchi Trump ana 68,654,143 na Kamala ana 63,558,470
Soma https://jamii.app/TrumpWins
#JamiiForums #Democracy #Governance #CivilRights #USElection2024 #USDecides
Hadi sasa Trump amefikisha Kura za Wajumbe (Electoral Votes) 267 kati ya 270 zinazotakiwa, huku Kamala akiwa na Kura 224. Kwa upande wa Kura za Wananchi Trump ana 68,654,143 na Kamala ana 63,558,470
Soma https://jamii.app/TrumpWins
#JamiiForums #Democracy #Governance #CivilRights #USElection2024 #USDecides
👍3❤1
DIGITALI: Taarifa ya Mmiliki wa #META, Mark Zuckerberg imesema majaribio ya utaratibu wa kutumia Madokezo ya Kijamii (Community Notes) kuhakiki Maudhui utaanza kwa Watumiaji waliopo Marekani na baadaye utaendelea kwa watumiaji Duniani kote
Awali, META ilikuwa ikitumia timu maalumu ya Uhakiki wa Maudhui na Mifumo ya Kiotomatiki, utaratibu ambao ulikuwa ukilalamikiwa kuwa unabana Uhuru wa Kujieleza
Inadaiwa kuwa hatua hiyo ni mkakati wa META kujenga uhusiano na Utawala mpya wa Rais #DonaldTrump atakayeingia Ikulu Januari 20, 2025.
Soma https://jamii.app/FactCheckers
#DigitalRights #FreeSpeech #FreedomOfExpression #JFDigitali #JamiiForums

🔥1
MAREKANI: Rais #DonaldTrump amesaini takriban amri 200 za Kiutendaji, baada ya kuapishwa kama Rais wa 47 wa Nchi hiyo, zikihusisha mabadiliko makubwa kwenye Uhamiaji, Uchumi, Afya, Mazingira, na Masuala ya Jinsia
Miongoni mwa amri inayozungumziwa zaidi ni kukomesha Uraia wa Kuzaliwa. Trump amesema hatua hiyo inalenga kukomesha Utalii wa Uzazi, (Birth Tourism) ambapo Watu huenda Marekani kwa makusudi ya kujifungua ili Watoto wao wapate uraia
Aidha, Trump amefuta amri 78 za mtangulizi wake, #JoeBiden, ambazo zilihusisha kupunguza utoaji wa Gesi chafu, kulinda Ardhi ya Serikali, na kupunguza gharama za Dawa
Soma https://jamii.app/TrumpsExcutiveOrders
#JamiiForums #TrumpExcutiveOrders #Governance #Democracy #Demokrasia #Diplomacy

❤2
MAREKANI: Moja ya masharti waliyowekewa Watu Januari 20, 2025, kabla ya kuingia katika ukumbi wa Capital One Arena, Jijini Washington DC ilikuwa ni kuacha mabegi na mikoba nje ili waweze kushuhudia uapisho wa Rais #DonaldTrump
Soma https://jamii.app/CapitalOneAreaInstructions
#JamiiForums #Democracy

Kupitia chapisho lake katika Mitandao ya Kijamii, Rais #DonaldTrump amesema mtangulizi wake #JoeBiden ndiye alianzisha utaratibu huo Mwaka 2021 alipoagiza Idara za Ujasusi (IC) kumnyima Rais wa 45 wa Marekani (Trump) ufikiaji wa taarifa za Usalama wa Taifa, haki ambayo kawaida hutolewa kwa Marais wa zamani
Aidha, katika chapisho hilo, Trump amesema "Ripoti ya Hur imefichua kuwa Biden ana matatizo ya kumbukumbu na hata alipokuwa kwenye kilele cha uwezo wake, hakuweza kuaminiwa kwa taarifa nyeti. Mimi daima nitalinda usalama wa taifa letu."
Robert Hur ni Mwanasheria Maalum aliyekuwa na jukumu la kuongoza uchunguzi juu ya jinsi Rais Joe Biden alivyoshughulikia nyaraka za siri alipokuwa Makamu wa Rais (2009-2017) zilizopatikana katika maeneo yasiyo rasmi, ikiwa ni pamoja na ofisi yake ya zamani iliyopo Washington, D.C., na nyumbani kwake, Delaware
Soma https://jamii.app/TrumpVsBidenFeb
#JamiiForums #Governance #Accountability #Demokrasia

This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Akihojiwa na Azam TV kuhusu maamuzi yanayofanywa na Rais wa Marekani, #DonaldTrump, ikiwemo Sera za kusitisha baadhi ya misaada kwa Nchi za Afrika, Mkurugenzi wa Kituo cha Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC), David Kafulila, amesema hiyo ni inaweza kuwa fursa kwa Afrika
Kafulila amesema moja ya njia ya kujiweka sawa ni kupunguza matumizi ya kodi na mikopo katika maeneo yanayoweza kufanywa na Sekta Binafsi, moja ya sehemu ambayo ilikuwa na sapoti ya Marekani ili kunufaisha sekta mbalimbali kama Elimu, Afya au Maji ambazo zilikuwa zinapata msaada wa Marekani au Benki ya Dunia
Soma https://jamii.app/KafulilaTrump
#Uchumi #JFEconomy #Accountability #Governance

👍2
MAREKANI: Rais #DonaldTrump ametoa "onyo la mwisho" kwa Hamas kuwaachia mateka walioko Gaza pamoja na miili ya Watu waliofariki na kusisitiza kuwa Marekani itampa msaada Israel wa kuwamaliza kama hawatafuata agizo hilo
Ameyasema hayo kupitia Ukurasa wake wa Mtandao wa Instagram leo Machi 6, 2025 muda mfupi baada ya Serikali ya Marekani kuthibitisha kuwa wanafanya mazungumzo
Taarifa hiyo imetoa onyo kuwa Viongozi wa #Hamas wasipofanya hivyo ikiwa ni pamoja na kuondoka #Gaza kutakuwa na madhara makubwa. Marekani iliitaja Hamas kama Shirika la Kigaidi mnamo 1997
Soma https://jamii.app/TrumpAionyaHamas
#JamiiForums #JFDiplomacy #HumanRights

MAREKANI: Zaidi ya Wafanyakazi 1,300 wa Kituo cha Habari cha Voice of America (VoA) wametakiwa kupumzika, ikiwa ni muda mfupi baada ya Serikali ya Rais #DonaldTrump kusitisha ufadhili kwa Vyombo kadhaa vya Habari ambavyo vinafadhiliwa na Serikali hiyo
Mkurugenzi wa VoA, Michael Abramowitz, amesema ana masikitiko kutoa taarifa ya Wafanyakazi wake hao wakiwemo Waandishi, Watayarishaji vipindi na Wasaidizi kulazimika kwenda Likizo ya Kiutawala, hali ambayo imeathiri matangazo ya Shirika hilo linalotangaza katika Lugha 50
Aidha, mbali na VoA ambayo bajeti yake kwa Mwaka ni Wastani wa Dola Milioni 270 (takribani Tsh. Bilioni 717), ikiwa na takribani Wafanyakazi 2,000 na wasikilizaji takribani Milioni 361, pia Shirika la Vyombo vya Habari la Kimataifa (Global Media) linalofadhili Radio Free Europe/Radio Liberty na Radio Free Asia nalo limeathirika
Soma https://jamii.app/VoAOnLeave
#JamiiForums #PressFreedom #Governance

MAREKANI: Rais #DonaldTrump, siku ya Jumatano Aprili 9, 2025 alisitisha ghafla ushuru wa Forodha kwa Nchi nyingi kwa kipindi cha Siku 90, na kuongeza zaidi kiwango cha ushuru kwa Bidhaa kutoka China hadi kufikia 125%
Hatua hiyo imeonekana kuwa jaribio la kupunguza Mvutano wa Vita ya Kibiashara ambayo haijawahi kushuhudiwa kati ya Marekani na Mataifa mengi Duniani, na kulenga zaidi mzozo kati ya Marekani na China
Wakati Hisa na Dhamana za Serikali zikiuzwa kwa wingi, Wananchi wanashuhudia Akiba zao za kustaafu zikipungua, huku Biashara zikiashiria mauzo duni kuliko matarajio na kupanda kwa bei.
Soma https://jamii.app/TrumpTariffs90Days
#JamiiForums #Governance #TariffWar #TrumpTarrifs

MAREKANI: Serikali ya Rais #DonaldTrump imekizuia Chuo Kikuu cha Harvard kuandikisha Wanafunzi wa Kigeni ambapo inaelezwa imechukua hatua hiyo kwa kuwa #Harvard inaiunga Mkono Palestina pamoja na kushirikiana na Chama cha Kikomunisti cha China
Barua iliyoelekezwa kwa Uongozi wa Chuo hicho inaeleza kuwa Cheti cha Usajili cha Mpango wa Kubadilishana Wageni (Student Exchange Visitor Program – SEVP) cha Chuo hicho kimefutwa rasmi
Chuo cha Harvard kina jumla ya Watu 9,970 katika kundi lake la Taaluma ya Kimataifa na takwimu zinaonesha Wanafunzi wa Kimataifa 6,793 wanachangia 27.2% ya Usajili wake kwa Mwaka wa Masomo wa 2024–2025
Soma https://jamii.app/HarvardBannedOutsiders
#JamiiForums #Governance #Diplomacy #JamiiAfrica

👍1👎1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
#DIPLOMASIA: #Israel imefanya mashambulizi Nchini #Iran katika Mji wa #Tehran ikiwa ni sehemu ya Oparesheni kwa kile ambacho Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amesema walilenga kudhoofisha Miundombinu ya Nyuklia ya Iran na Viwanda vya Makombora ya masafa marefu
Pamoja na hivyo, Israel imetangaza hali ya hatari, ikisema inatarajia mashambulizi ya kulipiza kisasi kutoka kwa Iran, wakati ambapo Iran imesema mashambulizi hayo yameathiri Makazi ya raia na kuua Watu kadhaa wakiwemo Watoto
Wakati huohuo, Rais wa Marekani, #DonaldTrump amekiambia Kituo cha #FoxNews kuwa alikuwa na taarifa kuhusu mashambulizi hayo kabla lakini Nchi yake haikuhusika kwa namna yoyote
Soma https://jamii.app/IsraelAgainstIran
#Diplomacy #Governance #HumanRights #JamiiForums #JamiiAfrica

❤1
DIPLOMASIA: Siku kadhaa baada ya Rais wa Marekani, #DonaldTrump kuwaonya raia wa #Iran waliopo Mji wa Tehran kuhama, kwa kile alichoeleza kutakuwa na mashambulizi yanayoweza kufanyika katika eneo hilo, amedai Marekani ina udhibiti wa anga la Iran
Kupitia Mtandao wa Truth Social, Trump ameandika “Marekani sasa inadhibiti kikamilifu anga la Iran. Iran ilikuwa na vifaa vizuri vya kufuatilia anga na ulinzi wa kutosha na vingi lakini haviwezi kulinganishwa na ‘vitu’ vilivyotengenezwa na Wamarekani. Hakuna anayefanya vizuri zaidi ya Marekani.“
Ameongeza “Tunajua kwa uhakika kabisa alipojificha huyo anayeitwa ‘Kiongozi Mkuu’ (akimaanisha Ayatollah Ali Khamenei). Ni mlengwa rahisi, lakini yuko salama pale alipo hatutamwondoa (kumuua!), angalau si kwa sasa. Hatutakubali makombora yaelekezwe kwa raia au kwa Wanajeshi wa Marekani. Subira yetu inaanza kuisha. Asanteni kwa kulipa hili uzito!”
Soma https://jamii.app/MarekaniKumilikiAngaIran
#JamiiAfrica #JamiiForums #JFMatukio

MAREKANI: Rais #DonaldTrump amemtuhumu Rais wa zamani #BarackObama kwa uhaini, akidai aliongoza njama na kushirikiana na Urusi ili kuhujumu kampeni zake za Uchaguzi Mwaka 2016, ingawa hakutoa ushahidi.
Trump ametoa tuhuma hizo wakati akiwa bado anakabiliwa na shinikizo kutoka kwa Wanahabari la kutakiwa kutoa taarifa zaidi kuhusu mhalifu wa ngono Jeffrey Epstein, aliyefariki kwa kujinyonga gerezani Mwaka 2019 wakati akisubiri kesi.
Msemaji wa Obama, Patrick Rodenbush amesema: “Ofisi yetu kwa kawaida haijibu upuuzi na upotoshaji unaotoka Ikulu hii lakini haya ni madai ya kushtua kiasi cha kustahili majibu.”
Soma zaidi https://jamii.app/TrumpNaObama
#JamiiAfrica #JamiiForums #Governance #Democracy #JFDiplomacy

Serikali ya Uganda imethibitisha kuwa imeingia makubaliano na Marekani yatakayohusisha Wahamiaji kutoka Marekani kupokelewa nchini humo, ikiwa ni sehemu ya mpango wa #DonaldTrump unaolenga kuwarudisha maelfu ya Wahamiaji walioko katika hifadhi za Marekani.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Uganda imesema wapo tayari kupokea Wahamiaji hao na kudokeza kuwa itawapa kipaumbele zaidi wale ambao wana asili ya Kiafrika na ambao hawana rekodi yoyote ya Uhalifu.
Kando na Uganda nchi nyingine kutoka Afrika ambazo zimekubali kupokea wahamiaji kutokea Marekani ni Eswatini, Rwanda pamoja na Sudan ya Kusini.
Zaidi Soma: https://jamii.app/WahamiajiUganda
#JamiiAfrica #JamiiForums #HakiZaBinadamu #Utawala

❤3
MAREKANI: Majaji 6 kati ya 9 wa Mahakama Kuu wamefuta ushuru uliowekwa na Rais #DonaldTrump kwa mataifa mbalimbali, yakiwemo China, Canada na Mexico wakieleza kuwa Trump alivuka mipaka ya mamlaka yake kwani kwa mujibu wa Katiba, ni Bunge pekee lenye mamlaka ya kuweka ushuru dhidi ya mataifa mengine.
Akizungumza na Wanahabari muda mfupi baada ya tamko la Mahakama, Rais Trump alisema kuwa hajaridhishwa na uamuzi huo ambapo alidai kuwa mahakama na majaji waliotoa hukumu hiyo wana maslahi au wameshawishiwa na mataifa ya kigeni.
Zaidi https://jamii.app/TrumpUshuru
#JamiiForums #Diplomacy #JFDiplomacy #Governance

Wakati Zimbabwe ikikataa msaada huo, baadhi ya mataifa 16 ya Afrika yamesaini mikataba hiyo chini ya mkakati wa “America First Global Health Strategy” wa Rais #DonaldTrump, unaohusisha takribani Dola Bilioni 18.3 kwa ajili ya kupambana na magonjwa ya kuambukiza barani Afrika ukichukua nafasi ya programu zilizokuwa zinatekelezwa kupitia USAID.
Kwa taarifa zaidi tembelea https://jamii.app/ZimbabweMsaada
#JamiiForums #Diplomasia #JFDiplomacy
Kwa taarifa zaidi tembelea https://jamii.app/ZimbabweMsaada
#JamiiForums #Diplomasia #JFDiplomacy
❤1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Akizungumza muda mfupi baada ya Israel na Marekani kushambulia Mji Mkuu wa Iran, Tehran, Rais wa Marekani, #DonaldTrump amesema kwa muda mrefu Wananchi wa Iran walikuwa wakiomba msaada wa Marekani ili kuondoa Serikali iliyopo madarakani, na kuongeza kuwa Marekani imejibu ombi hilo.
Amesema pia baada ya shambulizi hilo, Wananchi wa #Iran watapata nafasi ya kurudisha Serikali iwe chini ya udhibiti wao.
Zaidi https://jamii.app/MarekaniNaIran
#JamiiForums #Diplomasia #Governance #JFDiplomacy

Kauli ya Rais #DonaldTrump inakuja siku moja baada ya Papa Leo XIV wakati wa ibada Aprili 11, 2026 katika Kanisa la Mtakatifu Petro mjini Vatican, kukosoa vita inayoendelea kati ya Marekani, Israel na Iran, akisema Viongozi wanaolewa sifa za madaraka na nguvu za kijeshi ndiyo wanaochochea vita hiyo.
Shiriki mjadala https://jamii.app/TrumpPapaMarekani
#JamiiForums #JFDiplomacy #Governance