JamiiForums
✔
23.9K subscribers
40.7K photos
3.61K videos
34.7K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Samaki na Dagaa wana wingi wa Madini ya #Calcium ambayo huhifadhiwa kwenye Mifupa na meno ya binadamu kwa zaidi ya 99%. Madini haya hufanya kazi ya kuimarisha meno na mifupa

Tafiti za Kisayansi za Virutubisho vilivyomo kwenye Vyakula zimebainisha kuwa, Mlaji wa Dagaa hupata kiasi kikubwa zaidi cha Madini hayo yanayopatikana kwa wingi katika mifupa yake ambayo hutafunwa moja kwa moja, tofauti na ilivyo kwa aina nyingi za Samaki walio na mifupa mikubwa isiyotafunika kirahisi

Fahamu zaidi https://jamii.app/FaidaZaDagaa

#JamiiCheck #FactCheck
👍6
Kabla ya kugunduliwa kwa #Intaneti na Mitandao ya Kijamii, watu walikuwa wakitumia njia mbalimbali kusambaza #HabariPotofu kwa lengo la kufikia Malengo yao, iwe ni Kisiasa, Kiuchumi au Kijamii

Hata hivyo, Ugunduzi wa Intaneti na Mitandao ya Kijamii vimeongeza urahisi wa usambazaji wa Habari Potofu kwa kufanya zifikie Watu wengi ndani ya Muda mfupi

Katika kipindi chote cha Historia, Suala la Elimu, Uhuru wa kujieleza na Ukweli wa Habari vimekuwa nyenzo muhimu katika kukabiliana na Changamoto hii

Soma https://jamii.app/IntanetiNaHabari

#JamiiForums #JamiiCheck #HakikiHabari #Misinformation #Disinformation #FactsChecking #FactCheck
👍5
Jukwaa la JamiiCheck.com limefuatilia madai yanayosambaa kwenye Mitandao ya Kijamii kuwa Ugonjwa wa Macho Mekundu (#RedEyes)unaweza kuambukizwa kwa kutazamana na Mgonjwa na kubaini kuwa ni Uzushi

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya #Tanzania, Ugonjwa huu huambukizwa kwa kugusa Tongotongo au Machozi ya Mtu mwenye Maambukizi ambapo hili linaweza kuwa ni kwa kugusa sehemu ambazo mtu mwenye maambukizi amezigusa

Aidha, hakuna Tiba Maalumu ya ugonjwa huu ambao kwa baadhi ya Watu huweza kudumu hadi wiki mbili

Soma https://jamii.app/UzushiRedEyes

#JamiiForums #VisitJamiiCheck #HakikiTaarifa #Misinformation #Disinformation #FactsChecking #FactCheck
👍1
Kuketi muda mrefu sehemu moja si salama kwa afya, huongeza hatari ya kupata magonjwa ambayo hufanya kushindwa kutekeleza majukumu, kuongezeka uzito, kisukari, kuziba mishipa ya damu na hata kusababisha kifo.

Wataalamu wa afya wanashauri mtu atembee kidogo kila baada ya dakika 30 ili kujiepusha na hatari ya magonjwa yanayoweza kusababishwa na kukaa muda mrefu.

Soma https://jamii.app/Kukaasehemumoja

#JamiiForums #VisitJamiiCheck #HakikiTaarifa #Misinformation #Disinformation #FactsChecking #FactCheck
❤3👍3🥱2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Tembelea Jukwaa la JamiiCheck.com uweze kushiriki mchakato wa Kuhakiki Taarifa zinazopatikana ndani na Nje ya Mtandao

#JamiiCheck #Misinformation #Disinformation #FactCheck #VisitJamiiCheck
Mdau, nini kifanyike kupunguza unyanyasaji wa kijinsia Mitandaoni?

Kushiriki Mjadala Bofya https://jamii.app/UonevuMtandaoni

#JamiiCheck #FactCheck #FactChecking #VerifyBeforeYouShare #HakikiTaarifa