JamiiForums
βœ”
23.9K subscribers
40.7K photos
3.6K videos
34.7K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Siku ya Kimataifa ya Haki ya Kupata Taarifa (International Day For Universal Access to Information) ni siku inayotumiwa kutambua na kusisitiza umuhimu wa Haki ya Umma kupata Habari na Taarifa ili kufanya Maamuzi sahihi

Siku hii inaadhimishwa Septemba 28 kila Mwaka na inalenga kuhamasisha Uwazi na Uwajibikaji kwa Serikali na Taasisi za Umma

Soma https://jamii.app/AccessToInfoDay2023

#JamiiForums #InternationalDayForUniversalAccessToInformation #AccessToInfoDay
#Accountabilty
πŸ‘2
Raia wenye Taarifa Sahihi wanaweza kufanya Maamuzi Sahihi hasa wakati wa kupiga kura. Ni pale tu Wananchi wanapojua jinsi wanavyotawaliwa, ndipo wanaweza kuiwajibisha Serikali kwa Maamuzi na Matendo yake

Upatikanaji wa Taarifa kwa wote unamaanisha kila Mtu ana Haki ya kutafuta, kupokea na kusambaza taarifa. Haki hii ni sehemu muhimu ya Haki ya Uhuru wa Kujieleza. Pia, inafungamana na Haki ya Uhuru wa Vyombo vya Habari

Soma https://jamii.app/AccessToInfoDay2023

#JamiiForums #AccessToInfomation #Accountabilty
πŸ‘1
UCHUMI: Serikali ya Tanzania imekubali kukutana na Mabalozi wa Nchi 9 kujadili madai yaliyotolewa na baadhi ya Wawekezaji kuhusu masuala ya Kikodi ikiwemo madai na makadirio ya Kodi kubwa zisizoendana na uhalisia kutoka Mamlaka ya Mapato (TRA)

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Januari Makamba, amesema Kikao hicho kitakuwa na Maafisa wa Serikali kutoka Taasisi husika hivyo Wawekezaji wanaokabiliwa na changamoto zote wawasilishe vielelezo juu ya malalamiko yao

Mabalozi waliowasilisha hitaji la kikao hicho ni wanaowakilisha Mataifa ya Marekani, Uingereza, Uholanzi, Ufaransa, Ubelgiji, Canada, Korea Kusini, Sweden, na Ujerumani

Soma https://jamii.app/ForeignTax

#JamiiForums #Governance #Accountabilty
πŸ‘9
DAR ES SALAAM: Mdau wa JamiiForums.com anatoa wito kwa Mamlaka kuchukua hatua za kuhakikisha ulindaji wa taarifa binafsi katika kituo cha NIDA kilichopo Kawe akidai taarifa za Watu hazilindwi kama inayotakiwa

Anasema Mamlaka husika zitoe Elimu kwa Maofisa hao kuhusu ulindaji wa taarifa binafsi katika kituo hiko

Soma https://jamii.app/NidaKutunzaFaragha

#JFUwajibikaji #JamiiForums #JFHuduma #Accountabilty #DigitalRights #PersonalDataProtection #JFDigitali
πŸ‘4
Mdau wa JamiiForums.com anadai changamoto ya Mabasi kusitisha safari kabla ya kufika Kituoni kutokana na Abiria kutojaa ipigwe Marufuku na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (#LATRA) iwachukulie hatua wahusika

Anasema 'kufaulishwa' pia sio salama kwa kuwa Abiria hawajui ubora wa chombo wanachohamishiwa na kama akipata changamoto anaweza kukosa msaada kwa kuwa tiketi itasoma namba ya basi tofauti

Soma https://jamii.app/KufaulishwaMabasi

#HudumaZaKijamii #JamiiForums #ServiceDelivery #Accountabilty
πŸ‘6
Vipi Mdau, umeshanunua LUKU Mwezi huu wa Julai 2024 na kukutana na Ongezeko la Tozo kwenye Makato kutoka Tsh. 1,500 hadi Tsh. 2,000?

Mjadala zaidi https://jamii.app/NyongezaTozoLUKU

#Uchumi #JamiiForums #Accountabilty #ServiceDelivery #HudumaZaKijamii
πŸ‘4
Mdau wa JamiiForums.com amelalamikia Kero ya Kivuko kimoja tu kufanya Kazi kati ya Kigongo - Busisi licha ya eneo hilo kuwa na Vivuko Vitatu ambapo inadaiwa vingine ni vibovu

Ameomba Serikali ishughulikie kero hiyo kwasababu inaleta Usumbufu kwa Watumiaji pamoja na kusababisha Msongamano mkubwa wa Magari

Soma https://jamii.app/BusisiKivuko1

#JamiiForums #ServiceDelivery #Accountabilty #Uwajibikaji #HudumaZaKijamii
πŸ‘3
Benki ya Dunia (WB) inadaiwa kusimamisha Haki ya #Gabon kupewa Mikopo na Ruzuku kuanzia Julai 2024 kutokana na kushindwa kulipa madeni ya zamani ambapo malipo ya Madeni yaliyopitiliza yalikuwa takriban Dola Milioni 17 (Tsh. Bilioni 44.7) kufikia Juni 30

Kwa mujibu wa #Reuters, Nchi hiyo ya Afrika ya Kati kwa sasa inalipa mikopo angalau 11 ya Benki ya Dunia ambapo #WB ilikubali kukopesha au kutoa ruzuku kwa Gabon zaidi ya Dola Bilioni 1 (Tsh. Trilioni 2.6) tangu Mwaka 2012 na imeshatoa zaidi ya Dola Milioni 700 (Tsh. Trilioni 1.8)

Msemaji wa Benki ya Dunia amesema Kusimamishwa kwa utoaji wa Fedha ni utaratibu ulioainishwa katika makubaliano ya ufadhili na wana imani Mamlaka zitachukua hatua za kurekebisha hali hiyo haraka iwezekanavyo

Soma https://jamii.app/GabonLoansWB

#Accountabilty #JamiiForums #Uchumi #Governance
πŸ‘3
Mdau wa JamiiForums.com aliyejitambulisha kuwa ni Mwanafunzi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (Dar es Salaam University College of Education - DUCE) - amedai Wanafunzi wanaodai malipo ya β€œRefund” wamekuwa wakizungushwa na kutolipwa tangu Julai 2023

JamiiForums imepata mrejesho kutoka Idara ya Naibu Mkuu - Mipango, Fedha na Utawala ya DUCE ambayo imeeleza Wanafunzi ambao bado wanadai ni 11 ambao Hundi yao iliwasilishwa Benki lakini ikakwama kutokana na majina ya akaunti kutofautiana

Taarifa imeeleza β€œIlilazimika kuwatafuta mmoja mmoja ili kupata majina na akaunti sahihi, ilitarajiwa kuwa hadi kufikia Julai 3, 2024 wawe wamepata.”

Soma https://jamii.app/RefundDUCE

#Governance #JamiiForums #Accountabilty #Uwajibikaji #ServiceDelivery
πŸ‘5❀1
Bodi ya Sukari Tanzania (SBT) imesema ilitoa Vibali vya Kuagiza Sukari kwa Wazalishaji wa Ndani (Viwanda) mapema lakini hawakuvichukua kwa wakati na hivyo ikavitoa vibali kwa Wafanyabishara ili kukabiliana na upungufu wa Sukari uliojitokeza

Mkurugenzi wa SBT, Profesa Kenneth Bengesi amezitaja kampuni za Wafanyabishara (Wasiozalisha Sukari) zilizopewa Vibali ili kuziba pengo ni Yasser Provisional Store (Aprili 2, 2024), Zenj General Machandise (Aprili 30, 2024) na Itel East Africa (Januari 30 na Februari 2, 2024)

Soma https://jamii.app/VibaliSugar

#JamiiForums #Governance #JFHuduma #SugarCrisis #ServiceDelivery #Accountabilty #Uwajibikaji
πŸ‘1
HAKI RAIA: Sifa Muhimu za Mwananchi kujiandikisha na kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 ni awe Raia wa Tanzania mwenye Miaka 18 au Zaidi, awe Mkazi wa eneo la Kitongoji au Mtaa husika, asiwe na Ugonjwa wa akili uliothibitishwa na Daktari na awe amejiandikisha kupiga kura

Kwa Dar es Salaam, Uchaguzi utafanyika katika Mitaa yote 564 ikiwa na Mgawanyo wa Wilaya ya #Ilala Mitaa 159, #Kinondoni Mitaa 106, #Temeke Mitaa 142, #Kigamboni Mitaa 67 na #Ubungo Mitaa 90

Hatua zinazoendelea ni pamoja na Maandalizi ya Vifaa vya Uchaguzi, Uhakiki wa Vituo vya kuandikishia Wapiga kura, na Uelimishaji umma juu ya Uchaguzi huo

Soma https://jamii.app/MitaaUchaguziDar

#JamiiForums #Accountabilty #Democracy #CivilRights #Kuelekea2025 #UchaguziSerikaliMitaa
πŸ‘1
Vipi Mdau, Barabara za eneo lako zinafanyiwa Usafi au Lami imegeuka kuwa Barabara ya Vumbi?

Mjadala https://jamii.app/MichangaBarabara

#JamiiForums #Accountabilty #Uwajibikaji #HudumaZaKijamii
πŸ‘1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
MANYARA: Waziri Mwigulu amesema Wananchi wanaofika katika ofisi za umma wanapaswa kuandika majina yao pamoja na maelezo ya changamoto au huduma waliyoifuata, ili kuongeza uwajibikaji na kuboresha utoaji wa huduma.

Mwigulu ametoa kauli hiyo Februari 26, 2026, wakati akizungumza katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi la jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, akisisitiza kuwa utaratibu huo utasaidia kuongeza uwajibikaji.

Zaidi https://jamii.app/OfisiUmmaHuduma

#JamiiForums #Uwajibikaji #Accountabilty