JamiiForums
✔
23.9K subscribers
40.7K photos
3.6K videos
34.7K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MAREKANI: Wanahabari wa #Reuters wamepanga kugoma kupinga ongezeko la Mishahara la 1% ambalo haliendani na Mfumuko wa Bei wa 9%

> Hivi karibuni Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari nchini humo wamelalamika kutotendewa haki na Waajiri wao

Soma https://jamii.app/MgomoReuters
👍4👏1😁1
KENYA: Bunge la Kitaifa limepokea Ombi linalotaka Mtandao wa #TikTok ufungiwe Nchini humo kwa maelezo umekuwa ukitumika kuchapisha Maudhui ya Ngono, Uchochezi na Uchafu Unaodhoofisha Maadili ya Kitamaduni na Kidini

Mlalamikaji ameonya endapo Mtandao huo hautafungiwa, utahatarisha Usalama wa Wananchi hasa katika #AfyaYaAkili kwa Vijana na kushuka kwa Ufaulu wa Masomo

Katika utafiti uliofanywa na #Reuters, #Kenya inaongoza kwa 54% katika matumizi ya kila namna ya TikTok Duniani na 29% ikitumika kwaajili ya kupata Habari ikifuatiwa na #Thailand na Afrika Kusini

Soma https://jamii.app/TiktoKE

#JamiiForums #DigitalRights #InternetSafety #Governance #MentalHealthAwareness #DigitalWorld #JFDigitali
👍11👏1
ISRAEL/GAZA: Watu zaidi ya 1,100 wameripotiwa kupoteza maisha katika mapigano kati ya #Israel na #HAMAS wakiwemo Watoto zaidi ya 100 na majeruhi zaidi 3,000

Kwa mujibu wa #AlJazeera na #Reuters, Watu zaidi ya 123,000 wamelazimika kuyakimbia makazi yao kutokana na mashambulizi hayo

Aidha, takwimu zinaonesha kwa kipindi cha miaka 15 kutoka Mwaka 2008, mapigano kati ya Israel na #Palestina yamegharimu maisha ya Watu zaidi ya 7,500, ambapo kumekuwa na wastani wa siku 100 za mapigano tangu wakati huo

Soma https://jamii.app/GazaDeaths

#JamiiForums #JFMatukio #Diplomacy #HumanRights
😢5👍3
Benki ya Dunia (WB) inadaiwa kusimamisha Haki ya #Gabon kupewa Mikopo na Ruzuku kuanzia Julai 2024 kutokana na kushindwa kulipa madeni ya zamani ambapo malipo ya Madeni yaliyopitiliza yalikuwa takriban Dola Milioni 17 (Tsh. Bilioni 44.7) kufikia Juni 30

Kwa mujibu wa #Reuters, Nchi hiyo ya Afrika ya Kati kwa sasa inalipa mikopo angalau 11 ya Benki ya Dunia ambapo #WB ilikubali kukopesha au kutoa ruzuku kwa Gabon zaidi ya Dola Bilioni 1 (Tsh. Trilioni 2.6) tangu Mwaka 2012 na imeshatoa zaidi ya Dola Milioni 700 (Tsh. Trilioni 1.8)

Msemaji wa Benki ya Dunia amesema Kusimamishwa kwa utoaji wa Fedha ni utaratibu ulioainishwa katika makubaliano ya ufadhili na wana imani Mamlaka zitachukua hatua za kurekebisha hali hiyo haraka iwezekanavyo

Soma https://jamii.app/GabonLoansWB

#Accountabilty #JamiiForums #Uchumi #Governance
👍3
Kampuni ya Novartis kwa kushirikiana na Shirika la Medicines for Malaria Venture (#MMV) imetangaza kupokea kibali kutoka Mamlaka ya Dawa nchini Uswisi kwa dawa ya kwanza Duniani ya kutibu #Malaria kwa watoto wachanga iitwayo 'Coartem Baby' au 'Riamet Baby' kwa baadhi ya nchi, ikilenga watoto wenye uzito kati ya kilo 2 mpaka 5, ambao awali hawakuwa na tiba iliyothibitishwa kutibu Ugonjwa huo

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la #Reuters, Nchi nane za Africa; Tanzania, Kenya, Uganda, Malawi, Msumbiji, Nigeria, Burkina Faso na Ivory Coast, zilishiriki katika tathmini ya dawa hiyo na zinatarajiwa kuidhinisha matumizi yake ndani ya siku 90, huku Ghana ikiwa tayari imeshaidhinisha

Dawa hiyo inatarajiwa kusaidia Kuboresha utoaji wa Huduma za Afya, Kupunguza Vifo vya Watoto na kuchangia katika lengo la muda mrefu la Kutokomeza Malaria Duniani


Zaidi soma https://jamii.app/TibaMalariaWatotoWachanga

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFHuduma #JFAfya #Malaria
❤1