DAR: Mdau wa JamiiForums.com kutoka Tegeta anasema ni muhimu kwa DAWASA kufanya jitihada za kuhakikisha taarifa za Ukosefu wa Maji zinawafikia Wateja wao kwa wakati, ili kuwaepusha na usumbufu wa Ukosefu wa Huduma hiyo Muhimu
Amesema ni vema wakatumia kurasa zao za Mitandao ya Kijamii kusambaza taarifa mara kwa mara, badala ya kutuma kwa namba za Simu ambazo nyingi ni za wenye nyumba hivyo taarifa kutowafikia Wateja ambao ni Wapangaji
Je, ulipata taarifa mapema ya changamoto ya Maji iliyopo maeneo mbalimbali ya Jiji?
Mjadala https://jamii.app/DAWASATaarifa
#JamiiForums #ServiceDelivery #JFHuduma #Governance #Accountability #DigitalWorld #EmbracingTechnology

👍1
TEKNOLOJIA: Taasisi ya Kitaifa ya Afya na Ubora wa Huduma (NICE) ya Uingereza imesema teknolojia ya Akili Mnemba (AI), itasaidia kuongeza Uhakika wa Majibu ya Vipimo vya X-Ray kwakuwa ina uwezo wa kuona Uvunjikaji wa Mifupa zaidi ya inavyoonekana kwenye X-Ray
Kwa mujibu wa NICE, kwa sasa, uwezekano wa X-Ray kutoona Mivunjiko mingine zaidi kwa Mgonjwa huwa ni kati ya asilimia 3 hadi 10 kwenye vipimo vya sasa na hivyo kuongeza muda wa uchunguzi au kutopatikana kwa tiba stahili kwenye majeraha
Imeelezwa kuwa, teknolojia ya AI kwenye Vipimo vya X-Ray itapunguza muda wa kusubiri majibu kutoka kwa wataalamu wa Maabara, pamoja na kuondoa makosa ya kibinadamu yanayojitokeza wakati wa kusoma vipimo
Soma https://jamii.app/AIonXRays
#JamiiForums #TechWorld #DigitalWorld #Innovations #EmbracingTechnology

👍3❤1
MAREKANI: Serikali kupitia Tume ya Biashara imeishtaki Kampuni ya #Meta, ikidai ununuzi wa Mitandao ya Kijamii ya #Instagram na #WhatsApp ulikuwa na nia ya kuondoa Ushindani katika Sekta ya Mitandao ya Kijamii
Kesi hiyo iliyoanza kusikilizwa leo Aprili 14, 2025, Washington DC inatarajiwa kuchukua Wiki kadhaa, huku Mwanzilishi wa Meta, Mark Zuckerberg, pamoja na aliyekuwa Afisa Mkuu wa Uendeshaji, Sheryl Sandberg wakitarajiwa kutoa ushahidi
Imeelezwa, ingawa FTC iliidhinisha manunuzi ya Mitandao hiyo, imeendelea kufuatilia athari zake kwa ushindani wa soko na kama itashinda kesi hiyo, Meta inaweza kulazimika kuuza Instagram na WhatsApp
Meta si Kampuni pekee ya Teknolojia inayochunguzwa kwa tuhuma za ukiritimba. Google pia inakabiliwa na uwezekano wa kulazimishwa kuuza kivinjari (Browser) chake cha #Chrome ili kuvunja utawala wake katika soko la Utafutaji mtandaoni (Online Search)
Soma https://jamii.app/MetaKuuzaIgNaWhatsApp
#JamiiForums #EmbracingTechnology #DigitalWorld