JamiiForums
✔
23.9K subscribers
40.7K photos
3.6K videos
34.7K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
#MAWASILIANO: Mkurugenzi wa Jukwaa la Katiba Tanzania (#JUKATA), Bob Wangwe amesema tangazo la Mamlaka ya Mawasiliano (#TCRA) kuzuia matumizi ya VPN linatafsiri Serikali bado inaendelea kubana Haki ya Wananchi kupata Habari huku akitolea mfano Uchaguzi Mkuu wa 2020 ambapo Mitandao ilizimwa na kuwanyima fursa hiyo Wananchi

Amesema matumizi ya #VPN kwenye mataifa mengine hayapigwi marufuku isipokuwa kwa nchi zenye dalili za Udikteta ndio mambo hayo hutokea kwa lengo la kuwachagulia Wananchi aina ya habari ya wanazotakiwa kupata

Ameongeza kuwa badala ya kupambana na wanaotumia VPN, Serikali ihangaike kudhibiti maudhui yasiyofaa na wanaoyazalisha kwasababu wanafahamika pamoja na mitandao yao na sio kuingilia faragha za Wananchi

Soma https://jamii.app/VPNTZA

#JamiiForums #Governance #DigitalRights #AccessToInformation #AccessNow #SayNoToCensorship #FreeVPN
👍10