JamiiForums
✔
23.9K subscribers
40.7K photos
3.6K videos
34.7K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Kwa mujibu wa Ripoti ya #AccessNow, kuzimwa Intaneti kulirekodiwa kwa angalau mara 187 katika Nchi 35 mwaka 2022. Ni mwaka wenye idadi kubwa zaidi ya Nchi ambapo kuzimwa kwa intaneti kulitokea

Kuzima Intaneti kunaathiri #UhuruWaKujieleza, Haki ya Wananchi Kupata Taarifa, na kunaleta athari katika Maendeleo ya Nchi

Zaidi, soma https://jamii.app/UhuruDigitali

#KeepItOn #DigitalRights #JFDigitali
👍5🔥1
SUDAN: Mtandao wa #NetBlocks umesema Vita ya pande mbili za Majeshi zinazopigana imesababisha upatikanaji wa Huduma ya Mawasiliano ya Intaneti kushuka hadi kufikia 2%

Mapigano hayo yaliyoanza Aprili 15 kati ya vikosi vinavyomtii Mkuu wa Jeshi na vya Makamu wake aliyegeuka mpinzani, Mohamed Hamdan Daglo yamesababisha Vifo zaidi ya 400 na Majeruhi zaidi ya 3500

Soma https://jamii.app/NetDownSudan

#JamiiForums #HumanRights #DigitalRights #AccessNow #Governance
👍5
JamiiForums as a partner to host - #CIPESAUG and co-host, the Government of #Tanzania is excited for the Forum on Internet Freedom in Africa (#FIFA2023) making its debut in Tanzania

Save the date: Thursday, 28th Sept. 2023, at 11:30am where we will be leading a session on Data Governance and Privacy Standards in Africa alongside #AccessNow and #Altadvisory. Discover the vast Opportunities and confront the ever-evolving Challenges in preserving Digital Privacy across the African continent

#JamiiForums #DataGovernance #DigitalPrivacy #InternetFreedomAfrica
👍2🤯1
Are you passionate about Data Privacy and Governance in Africa? So are we!

Join our session at #FIFAfrica23 on Sept. 28th, alongside #AccessNow and #Altadvisory and let's explore Challenges and Opportunities.

Together we can shape a more secure digital future

#JamiiForums #DigitalRights #DigitalPrivacy #DataGovernance #DataProtection #InternetFreedomAfrica
#MAWASILIANO: Mkurugenzi wa Jukwaa la Katiba Tanzania (#JUKATA), Bob Wangwe amesema tangazo la Mamlaka ya Mawasiliano (#TCRA) kuzuia matumizi ya VPN linatafsiri Serikali bado inaendelea kubana Haki ya Wananchi kupata Habari huku akitolea mfano Uchaguzi Mkuu wa 2020 ambapo Mitandao ilizimwa na kuwanyima fursa hiyo Wananchi

Amesema matumizi ya #VPN kwenye mataifa mengine hayapigwi marufuku isipokuwa kwa nchi zenye dalili za Udikteta ndio mambo hayo hutokea kwa lengo la kuwachagulia Wananchi aina ya habari ya wanazotakiwa kupata

Ameongeza kuwa badala ya kupambana na wanaotumia VPN, Serikali ihangaike kudhibiti maudhui yasiyofaa na wanaoyazalisha kwasababu wanafahamika pamoja na mitandao yao na sio kuingilia faragha za Wananchi

Soma https://jamii.app/VPNTZA

#JamiiForums #Governance #DigitalRights #AccessToInformation #AccessNow #SayNoToCensorship #FreeVPN
👍10
Mitandao ya #Netblocks na #CloudflareRadar inayohusika na ufuatiliaji wa Huduma za Intaneti na Usalama Mtandaoni imesema baadhi ya Nchi Barani Afrika zimepatwa na tatizo la kukatika kwa Huduma za Intaneti, sababu ikidaiwa ni kukatika kwa nyaya katika Mkongo wa Mawasiliano wa Baharini

Baadhi ya Nchi zilizoripoti kupata shida kwenye mawasiliano ni Tanzania, #IvoryCoast ambayo imeripoti kushuka kwa ubora kwa Intaneti hadi 4%, #Benin 14% na #Ghana kwa 25% huku nchi nyingine zilizopata shida zikiwa ni Afrika Kusini, #Nigeria, #Liberia, na #BurkinaFaso

Nchini #Tanzania, Mtandao wa #Vodacom umekiri kutokea kwa tatizo kwenye huduma za intaneti huku wakisema huduma za M-PESA, Kupiga na Kupokea Simu zinapatikana. Pia, Serikali za Nigeria na Liberia zimesema zimebaini uwepo wa tatizo la Intaneti

Vipi Mdau, umepata changamoto za Mawasiliano ya Simu au Intaneti wiki hii?

Soma https://jamii.app/ComsDisrupt

#JamiiForums #DigitalRights #AccessNow #InternetDisruption #ServiceDelivery
👍8👎1
MAWASILIANO: Wadau mbalimbali kutoka JamiiForums.com wamehoji ukimya wa Watoa Huduma za Intaneti nchini huku wakidai kumekuwa na tatizo la Kukatika kwa huduma hiyo mara kwa mara kwa zaidi ya Wiki 2

Baadhi wanadai walipojaribu kupata maelezo kwa Watoa Huduma (Mitandao ya Mawasiliano ya Simu na Kampuni zinazosambaza huduma) hawapati majibu ya kueleweka huku tatizo likiendelea kujirudia

Wanaomba Mamlaka zinazosimamia Haki za Wateja zichukue hatua kwasababu Wateja wengi wananunua Vifurushi ambavyo vinatolewa kwa muda maalumu na vinaisha bila kulipwa fidia

Soma https://jamii.app/InternetMbovu

#JamiiForums #DigitalRights #JFDigitali #Governance #SocialJustice #AccessNow
👍1