JamiiForums
✔
23.9K subscribers
40.7K photos
3.6K videos
34.7K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
#JFTECHNOLOGY: Mtandao wa Kijamii wa Twitter ambao una kikomo cha herufi 280 umeamua kufanya idadi kuwa 2,500 ikidaiwa ni katika kuboresha huduma kwa Wateja wake

> Mwaka 2017, #Twitter iliongeza idadi ya herufi kutoka 140 na kufikia 280

Soma - https://jamii.app/TwitterNewFeature
👍14👏2
Ndani ya Dunia ya sasa ya #Kidigitali, Simu Janja zimekuwa nyenzo muhimu katika Maisha ya kila siku, iwe kazini, nyumbani, kibiashara na Kijamii. Uwepo wa programu (#Applications) mbalimbali umesaidia katika kurahisisha shughuli mbalimbali kwa ufanisi zaidi.

Ukiwa ni Mdau wa #Teknolojia, ni programu gani unazozitumia ambazo ungeshauri wengine pia kuwa nazo? Kwa sababu gani?

Soma zaidi https://jamii.app/ProgramuSimu

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFTechnology #JFDigital #DigitalRights #DigitalWorld
Mdau wa JamiiForums.com anasema kawaida huwa anabadilisha simu baada ya Miaka miwili hadi Mitatu, Je, wewe unabadilisha baada ya muda gani na unazingatia nini zaidi?

Zaidi tembelea https://jamii.app/SimuMuda

#JamiiForums #JFTechnology #JFDigital
NIGERIA: Mkandarasi kutokea China, China Great Wall Industry Corporation ametoa siku 30 kwa Serikali ya Nigeria kulipa deni la Dola Milioni 11.44 (takriban Tsh. Bilioni 30) za huduma za uendeshaji wa satelaiti la sivyo itafunga huduma za mawasiliano zinazotegemea satelaiti nchini humo.

Deni hilo linahusiana na huduma za Telemetry, Tracking na Command kwa satelaiti ya mawasiliano NigComSat-1R, ambazo zimekuwa zikitolewa kutoka kituo cha udhibiti cha Kashi nchini China, ambapo huduma hiyo ikizimwa inaweza kuathiri matangazo ya televisheni, huduma za intaneti na mawasiliano ya kiusalama nchini humo.

Maafisa wa Nigeria Communications Satellite Limited wamesema wanapitia taarifa hiyo na watatoa majibu rasmi, huku satelaiti hiyo iliyozinduliwa Mwaka 2011 ikitarajiwa kufikia mwisho wa maisha yake ya kazi mwishoni mwa Mwaka 2026.

Soma https://jamii.app/ChinaNigeriaSatellite

#JamiiForums #Diplomacy #JFTechnology
❤1
Fainali za mashindano hayo zimefanyika Aprili 11, 2026, katika Ukumbi wa CRDB, Dar es Salaam.

Katika dunia ya leo ambapo kila mmoja wetu ana maisha mtandaoni, unadhani ni kitu gani kimoja ambacho unapaswa kukifahamu zaidi ili kulinda usalama wa akaunti yako?

Shiriki kwenye mjadala huu👉🏾 https://jamii.app/UdomCyberCompetition

#JamiiForums #JFElimu #JFTechnology #JFSports
Mdau, una utaratibu gani kuhusu matumizi ya simu wakati wa chakula?

Shiriki kwenye mjadala huu👉🏾 https://jamii.app/SimuChakula

#JamiiForums #JFTechnology #Maisha
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche ameyasema hayo Aprili 15, 2026 wakati akizungumzia kuondolewa kwa zuio la shughuli za chama na Mahakama ya Rufaa.

Shiriki mjadala kupitia https://jamii.app/HecheTeknolojia

#JamiiForums #JFTechnology #JFMatukio
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Jaji Chande ameyasema hayo wakati akiwasilisha Ripoti ya Tume ya Rais ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani Yaliyotokea Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2025, tarehe 23 Aprili, 2026, Dar es Salaam

Zaidi https://jamii.app/ChandePichaAI

#JamiiForums #Uwajibikaji #Utawala #JFTechnology
🤬2🤮1🕊1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo akizungumza Bungeni, Aprili 30, 2026, ameishauri Serikali kupitia Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA CCC) kuwasaidia Wananchi akieleza kuwa wana manung'uniko kuhusu gharama za 'bando' za simu.

Kauli hiyo imeungwa mkono na Spika wa Bunge, Mussa Azan Zungu ambaye ameeleza kuwa Nchi nyingi bando likibaki linapelekwa kifurushi kipya, hivyo amesisitiza bando lihamishiwe kifurushi kipya, lisikatwe.

Zaidi https://jamii.app/BandoKukatwa

#JamiiForums #DigitalWorld #DigitalRights #JFHuduma #JFTechnology