Umoja wa Ulaya (EU) umeonya unaweza kuiwekea vikwazo #Twitter kwa kutoheshimu Uhuru wa Vyombo ya Habari
Ni baada ya Twitter kufungia akaunti za Wanahabari wa #NewYorkTimes, #CNN na #WashingtonPost
Soma https://jamii.app/EUVsTwitter
#PressFreedom #DigitalRights #DataPrivacy

👍4
WATUMIAJI WA #TWITTER MILIONI 10 WATAKA #ELONMUSK AJIUZULU UTENDAJI MKUU
Jumla ya Kura 17,502,391 zimepigwa ndani ya Saa 12 ambapo Kura 10,063,874 (57.5%) zimependekeza Musk ajiuzulu huku Kura 7,438,516 (42.5%) zikimtaka aendelee
Soma https://jamii.app/TwitterVotes
#DigitalRights

👍12😁6
Seneta Gloria Orwoba wa Nchini #Kenya amesema anafikiria kuachana na #Twitter. Ameeleza, "Hili suala la kuwa na ngozi ngumu HAPANA! Sisi ni Binadamu"
Kwa Mtazamo wako, unadhani Uonevu ni sababu mojawapo inayopelekea baadhi ya Viongozi kuepuka Mitandao?
Soma https://jamii.app/SenatorKE
#JFDigitali #Cyberbullying #Governance

👍2😱1
Kupitia #Twitter na #Instagram, Msanii Wizkid kutoka Nigeria ameandika "Kwasababu ya hali zisizotarajiwa, More Love, Less Ego Tour imeahirishwa hadi mwishoni mwa 2023, Tiketi zote zilizonunuliwa zitapewa kipaumbele katika tarehe mpya"
#Wizkid alitarajiwa kuanza ziara hiyo Nchini Marekani Machi 3, 2023. Hata hivyo, atashiriki katika Tamasha la uzinduzi la #AfroNation huko Miami, Mei 28, 2023 akimfuatia #BurnaBoy atakayeanza Mei 27
Soma https://jamii.app/WizkidTour
#JFEntertainment

👍1
Mhandisi wa Twitter aliyezungumza na BBC kwa sharti la kutotajwa, amesema Mfanyabiashara #ElonMusk anayemiliki Kampuni za #SpaceX, #Tesla, Twitter, #Neuralink na #TheBoring hutembea na Walinzi 2 kila anapoingia #TwitterHQ
Musk ameonesha kuhofia Usalama wake na hana imani na Wafanyakazi wa #Twitter. Aidha, #MarkZuckerberg, Bosi wa #META ametengewa bajeti ya Tsh. Bilioni 32.7 kwa Mwaka 2023 kwaajili ya Ulinzi wake na Familia yake
Soma https://jamii.app/ElonSecurity
#JFMaisha #LifeStyle

👍6
UGANDA: MTOTO WA MUSEVENI ATANGAZA NIA YA URAIS
Jenerali Muhoozi Kainerugaba kupitia ukurasa wake wa #Twitter amethibitisha kugombea kiti cha Urais wa nchi hiyo ifikapo 2026
Mnamo Januari 2023, #Muhoozi alidai kuwa ana uhakika wa kumrithi baba yake, #YoweriMuseveni ambaye ametawala nchi hiyo tokea mwaka 1986
Soma https://jamii.app/PresidencyUG
#Democracy

👍8🤯2❤1
KENYA: Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai imeomba radhi kwa kuchapisha picha za zamani katika taarifa yake ya msako, ikiwataka washukiwa wanaodaiwa kuhusika na vitendo vya ghasia wakati wa #Maandamano kujisalimisha katika Vituo vya Polisi
Ni baada ya kukosolewa vikali kwa kueneza habari potofu Mtandaoni, baada ya kubainika kuwa baadhi ya picha zilizochapishwa kwenye ukurasa wao wa #Twitter zilipigwa tarehe za nyuma, nyingine takriban Miaka 10 iliyopita, huku nyingine zikiwa zimepigwa nje ya Mipaka ya #Kenya
Soma https://jamii.app/MsamahaDCI
#KenyaProtests #DCIKenya

❤4👍4
Mmiliki wa Mtandao #Twitter, #ElonMusk amesema licha ya kuwa hatumii #TikTok lakini hakubaliani na mipango ya kuufungia Mtandao huo Nchini Marekani kwasababu zinazodaiwa kuwa ni za Usalama licha ya kuwa uamuzi huo utakuwa na faida kwake kwa Watu wengi kuhamia Twitter
Soma https://jamii.app/TwitterTikTok
#DigitalWorld #DigitalRights
Soma https://jamii.app/TwitterTikTok
#DigitalWorld #DigitalRights
❤6😁4👍1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
#BUNGENI: Katika hatua za kupambana na wanaotangaza Mapenzi ya jinsia moja, Waziri wa Habari, #NapeNnauye amesema Tovuti 334, akaunti 361 za #Facebook, #Instagram 198, #Twitter 12, na Vikoa zaidi ya 2,456 vimefungwa
Kifungu cha 154 cha Sheria ya Kanuni za Adhabu Sura ya 16 kinabainisha kufanya mapenzi kinyume na maumbile ni kosa la jinai na adhabu yake ni kifungo cha Maisha jela au kisichopungua Miaka 30 jela.
Soma https://jamii.app/BungeniApril17
#Governance

👍21👏5👎1
Taarifa iliyotolewa Wiki hii kutoka kwa Mmiliki wa Twitter, Bilionea #ElonMusk, mtandao huo utaanza kuzifuta akaunti zote za watumiaji ambao hawajaingia kwa zaidi ya siku 30
Baadhi ya watumiaji wamehoji endapo ufutaji huo utamgusa Rais wa zamani wa Marekani, #DonaldTrump ambaye hajaitumia akaunti yake kwa siku 174 tangu aliporejeshwa baada ya kufungiwa Januari 2021
Awali, Sera ya #Twitter ilieleza kuwa ili uendelee kumiliki akaunti yako inatakiwa usivuke miezi 6 bila kuingia, lakini kwa mujibu wa Musk, hautakiwi kuingia tu, angalau uchapishe ujumbe
Soma https://jamii.app/TwitterPurge
#JamiiForums #DigitalRights

👍6🤡2
Mtandao wa #Twitter umetangaza kuweka kiwango cha idadi ya 'Tweets' utakazoona kuanzia Julai 1, 2023. Waliolipia '#Twitter Blue' watasoma Tweets 10,000, Wasiolipia 1,000 na Watumiaji Wapya watasoma 500
#ElonMusk ambaye anamiliki Mtandao huo amesema hatua hiyo imechukuliwa ili kudhibiti kiwango cha matumizi mabaya ya 'Data' na Mifumo ya Twitter kwa muda ikiwemo kuwataka Watu kujiunga na Huduma ya kulipia.
Hivyo kama unakutana na changamoto ya kutumia Twitter, taarifa hii ikufikie.
Soma https://jamii.app/TwitterBluePay
#JamiiForums #DigitalRights #JFDigitali #SocialJustice

😁7👍3👎1🤔1🥱1
MAREKANI: Kampuni #META inayomiliki Mitandao ya Kijamii ya #Facebook, #Instagram na #WhatsApp, imezundua 'App' nyingine ya Kijamii inayoelezwa kuwa itakuwa mshindani wa #Twitter
Mkurugenzi Mkuu wa META, #MarkZuckerberg amesema kuna kitu Twitter walipaswa kufanya na hawajakifanya hivyo 'Threads' inakuja kwaajili hiyo, japo itachukua muda kuifikia Twitter lakini Mtandao huo unalenga kuhudumia zaidi ya Watu Bilioni 1
Hata hivyo, Watumiaji wameonesha wasiwasi wao kuhusu kiwango cha 'TaarifaBinafsi zinazokusanywa na 'Threads' zikiwemo Taarifa za Afya, Fedha na aina ya Kivinjari (Browser), vyote vikiwa na uhusiano na Utambulisho wa Watumiaji.
Soma https://jamii.app/Threads
#JamiiForums #DigitalRights #Innovation #JFDigitali #DigitalWorld

👍9
TWITTER YATISHIA KUWASHTAKI META KWA KUIGA MIPANGILIO YAO KWENYE THREADS
#Twitter imetishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Meta, ikiishutumu kwa ujangili wa Wafanyakazi wa zamani na kutumia vibaya siri za Biashara na miliki
Twitter wamedai Meta imeajiri Wafanyakazi kadhaa wa zamani wa Twitter Mwaka jana, wakiongeza kuwa Kampuni hiyo "iliwapa kazi kimakusudi" kufanya kazi kwenye #Threads "kwa nia mahususi kwamba watumie siri za Biashara za Twitter na mali nyingine za kiakili ili kuharakisha Maendeleo ya programu shindani ya Meta."
Soma https://jamii.app/TwitterVsThreads
#JamiiForums #JFDigitali #DigitalRights

👍7❤1😁1
Kitendo cha Viongozi wa #NATO kudai #Ukraine inapaswa kujiunga na Muungano wa Kijeshi wa Umoja huo siku zijazo pindi masharti yatakapotimizwa bila kuyataja wala kutaja muda, kimemfanya Rais #VolodymyrZelenskyy kukosoa mchakato huo dhidi ya Taifa lake
Kupitia #Twitter, Rais Zelenskyy amekosoa uamuzi huo kwa kuandika "Ni jambo lisilo la kawaida na la kipuuzi kutoweka muda wa mwaliko au uanachama wa #Ukraine."
Soma https://jamii.app/ZelenskyyNATO
#Diplomacy #Governance #RussiaUkraineWar #JamiiForums

👍10
Waziri wa Afya, #UmmyMwalimu ametoa maelekezo kwa Mganga Mkuu wa Serikali kufuatia tukio la Mwanaume anaedaiwa kuwa na changamoto ya Afya ya Akili kukata uume wake, na Taarifa zake Binafsi kuwekwa hadharani na Wahudumu wa Afya
Akimjibu Mdau kwenye Mtandao wa #Twitter aliyelalamika kusambaa kwa taarifa hizo, Ummy ameandika “Upo sawa. Hii ni kinyume na Maadili ya Kitabibu. Namuelekeza Mganga Mkuu wa Serikali kulifuatilia na kunipatia Taarifa.”
Wadau mbalimbali wamelalamikia kitendo cha Taarifa Binafsi za Mgonjwa huyo kuanikwa Mtandaoni kinyume na Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (Kifungu cha 25) ambayo imeanza kutumika tangu Mei 1, 2023
Soma https://jamii.app/MaelekezoYaWaziri
#DataProtection #DataPrivacy #Accountability #JFDigitali #JFUwajibikaji23 #JamiiForums

👍7
Uchunguzi uliofanywa na Taasisi ya #SensorTower inayohusika na masuala ya utafiti wa Masoko ya Kimtandao, umeonesha Matumizi ya Mtandao wa #Threads yameporomoka hadi 75% ambapo imebainika Watumiaji wamekuwa wakiacha kuutumia siku chache tu baada ya kuupakua
Threads ambayo ilifanikiwa kupakuliwa na watumiaji zaidi Milioni 100 ndani ya Siku 5, na hadi sasa imepita watumiaji Milioni 184 imedaiwa kutokuwa na utofauti mkubwa na mshindani wake ambaye ni #Twitter
Ikumbukwe, Threads haipatikani katika Nchi za Umoja wa #Ulaya (EU) kutokana na Sheria kali za Ulinzi wa #TaarifaBinafsi.
Soma https://jamii.app/ThreadsFlops
#JamiiForums #DigitalRights #DataPrivacy #DataProtection #JFDigitali

👍6❤1
Bosi wa Mtandao wa Kijamii wa Twitter, Bilionea #ElonMusk amesema kuanzia sasa #Twitter itabadilika na kuitwa "X" pia, 'Logo' ya Ndege wa Blue itaondolewa rasmi na kuanza kutumika logo ya 'X'
Aidha, mwonekano wote wa Mtandao huo utakuwa umebadilika kufikia Julai 24, 2023, na hiyo ni endapo Elon Musk ataridhishwa na mwonekano wa mabadiliko hayo mapya
Soma zaidi > https://jamii.app/TwitterX
#DigitalRights #JFDigitali #Teknolojia #Innovation

👍12🔥3❤2💯1
Makamu wa Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya (EU) inayohusika na uchunguzi wa Maudhui Mitandaoni, #VeraJourova ameagiza Mitandao ya TikTok na X (zamani Twitter) kuongeza kasi ya kuondoa Maudhui ya Upotoshaji, Unyanyasaji Watoto na Chuki kuhusu Mgogoro wa #Israel na #Palestina
#TikTok imesema Wasimamizi wake wa Maudhui zaidi ya 6,000 na Akili Bandia (AI) wameondoa Mamilioni ya Taarifa Potofu huku #X (Zamani #Twitter) ikitakiwa kuchukua hatua zaidi baada ya kubainika kuwa na maudhui mengi lakini ina idadi ndogo ya Wasimamizi wa Maudhui
Sheria ya Huduma za Kidijitali ya #EU, iliyoanza kutumika mwaka 2022, inayataka Majukwaa ya Taarifa, Teknolojia na 'Injini Tafuti' (Search Engine) kuhakiki na kuondoa haraka maudhui hatari Mitandaoni
Soma https://jamii.app/XTOK
#JamiiForums #DigitalRights #InternetSafety #Accountability #Governance #JFDigitali

👍2👎1
#JanuariMakamba aliandika Nukuu hiyo Desemba 28, 2017 kupitia Mtandao wa #Twitter (Kwa sasa X) wakati akiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais akishughulikia masuala ya Muungano na Mazingira
Miezi 19 baadaye, Hayati Rais John Magufuli alimuondoa katika Baraza lake la Mawaziri. Septemba 12, 2021 aliteuliwa kuwa Waziri wa Nishati na Agosti 30, 2023 alihamishiwa Wizara ya Mambo ya Nje.
#JamiiForums #Governance #GoodMorning #JFQuotes

👍2
Mdau wa JamiiCheck.com alihitaji kufahamu Uhalisia wa chapisho linalosambaa mtandaoni linalodaiwa kuwa la #TheChanzo likionesha kuwa Mwenyekiti wa #CHADEMA, Freeman Mbowe amemshukuru Rais Samia kwa kuungana na CHADEMA kuomboleza kifo cha Mzee Ali Kibao
Ufuatiliaji wa #JamiiCheck kwa kutumia #GoogleReverseImage umebaini kuwa Taarifa hiyo Si ya Kweli na haijachapishwa katika kurasa rasmi za Mitandao ya Kijamii ya The Chanzo. Pia, kupitia kurasa zake, The Chanzo imekanusha kuhusika na Taarifa hiyo
Aidha, JamiiCheck imebaini uwepo wa utofauti wa Nembo inayotambulisha mtandao wa X ambapo chapisho hilo limetumia nembo ya zamani ya alama ya Ndege wakati mtandao huo ukijulikana kama #Twitter tofauti na The Chanzo ambao hutumia nembo yenye herufi X
Soma https://jamii.app/MboweAmshukuruSamia
#JamiiCheck #HakikiTaarifa #FactsCheck #FactsChecking #VisitJamiiCheck #MisDis04

👍3👏1