JamiiForums
✔
23.9K subscribers
40.7K photos
3.61K videos
34.7K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
TWITTER YATISHIA KUWASHTAKI META KWA KUIGA MIPANGILIO YAO KWENYE THREADS

#Twitter imetishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Meta, ikiishutumu kwa ujangili wa Wafanyakazi wa zamani na kutumia vibaya siri za Biashara na miliki

Twitter wamedai Meta imeajiri Wafanyakazi kadhaa wa zamani wa Twitter Mwaka jana, wakiongeza kuwa Kampuni hiyo "iliwapa kazi kimakusudi" kufanya kazi kwenye #Threads "kwa nia mahususi kwamba watumie siri za Biashara za Twitter na mali nyingine za kiakili ili kuharakisha Maendeleo ya programu shindani ya Meta."

Soma https://jamii.app/TwitterVsThreads

#JamiiForums #JFDigitali #DigitalRights
👍7❤1😁1
Uchunguzi uliofanywa na Taasisi ya #SensorTower inayohusika na masuala ya utafiti wa Masoko ya Kimtandao, umeonesha Matumizi ya Mtandao wa #Threads yameporomoka hadi 75% ambapo imebainika Watumiaji wamekuwa wakiacha kuutumia siku chache tu baada ya kuupakua

Threads ambayo ilifanikiwa kupakuliwa na watumiaji zaidi Milioni 100 ndani ya Siku 5, na hadi sasa imepita watumiaji Milioni 184 imedaiwa kutokuwa na utofauti mkubwa na mshindani wake ambaye ni #Twitter

Ikumbukwe, Threads haipatikani katika Nchi za Umoja wa #Ulaya (EU) kutokana na Sheria kali za Ulinzi wa #TaarifaBinafsi.

Soma https://jamii.app/ThreadsFlops

#JamiiForums #DigitalRights #DataPrivacy #DataProtection #JFDigitali
👍6❤1