JamiiForums
✔
23.9K subscribers
40.7K photos
3.6K videos
34.7K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
ELON MUSK APINGA KULAZIMISHA WATU KUPATA CHANJO YA #COVID19

Mmiliki wa Kampuni ya #Tesla amesema kulazimisha Watu kupata Chanjo au kuwafukuza kazi si sahihi

Ametoa wito Watu washawishiwe kupata Chanjo badala ya kulazimishwa

Soma - https://jamii.app/ElonMusk

#UVIKO3
MAREKANI: Mkurugenzi Mtendaji wa #Tesla, Elon Musk amenunua 9.2% ya hisa za Twitter na kuwa mbia mkubwa akimiliki karibu mara 4 zaidi ya hisa za Mwanzilishi wake #JackDorsey mwenye 2.25%

> Taarifa hii imefanya hisa za Twitter kupanda kwa 22%

Soma https://jamii.app/AnunuaHisaTwitter
Mhandisi wa Twitter aliyezungumza na BBC kwa sharti la kutotajwa, amesema Mfanyabiashara #ElonMusk anayemiliki Kampuni za #SpaceX, #Tesla, Twitter, #Neuralink na #TheBoring hutembea na Walinzi 2 kila anapoingia #TwitterHQ

Musk ameonesha kuhofia Usalama wake na hana imani na Wafanyakazi wa #Twitter. Aidha, #MarkZuckerberg, Bosi wa #META ametengewa bajeti ya Tsh. Bilioni 32.7 kwa Mwaka 2023 kwaajili ya Ulinzi wake na Familia yake

Soma https://jamii.app/ElonSecurity

#JFMaisha #LifeStyle
👍6
MAREKANI: Mahakama ya Rufaa imetupilia mbali kesi iliyodai kwamba Kampuni 5 kubwa za Teknolojia (#Apple, #Microsoft, #Tesla, #DellTechnologies na Kampuni Mama ya #Google, #Alphabet) zilikuwa zimehusika kutumikisha Watoto katika kuchimba Kobalti Nchini DR Congo kwa kuwa ndio Wateja wakubwa wa Kolbati (Colbat)

DRC inazalisha 60% ya Kobalti inayosambazwa Duniani, madini muhimu yanayotumika katika utengenezaji wa vifaa vingi vya Elektroniki, ambapo takriban Watoto 25,000 wanatajwa kufanya kazi katika Migodi hiyo

Kesi hiyo ilifunguliwa Mwaka 2019 na Shirika la International Rights Advocates, lililokuwa linawakilisha Watoto walionusurika au kuumia, pia Familia za Watoto waliopoteza Maisha wakati wakifanya kazi katika Migodi hiyo

Soma https://jamii.app/ChildLabourDRC

#JamiiForums #HumanRights #DRC
👍1