JamiiForums
βœ”
23.9K subscribers
40.7K photos
3.61K videos
34.7K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
#GOOGLE YAPATA SHAMBULIO LA MTANDAO

> Kampuni hiyo imepata shambulio la mtandao lililodumu kwa dakika 45

> Huduma zake mbalimbali kama Gmail na YouTube zilishindwa kupatikana kwa baadhi ya nchi ikiwemo Marekani, Canada, India na Uingereza

Soma https://jamii.app/GoogleIsDown
#GOOGLE NA FACEBOOK ZAITAKA AUSTRALIA KUBADILI SHERIA YA MAUDHUI

- Muswada uliwasilishwa Bungeni 2020 ili kulazimisha Google na #Facebook kuvilipa Vyombo vya Habari vya #Australia kwa kuchapisha maudhui yao au walipe mamilioni ya fedha kama faini

Soma - https://jamii.app/GoogleVsAustralia
URUSI YATISHIA KUPUNGUZA KASI YA GOOGLE

Urusi itafanya hivyo ikiwa #Google itashindwa kufuta kile ambacho Taifa hilo linaita ni maudhui yanayovunja Sheria

Mamlaka imetoa saa 24 kwa video zinazohusiana na Dawa za Kulevya na vurugu kuondolewa

Soma https://jamii.app/RussiaGoogle
ZOOM KULIPA DOLA MILIONI 86 KUMALIZA MADAI YA FARAGHA

Ilidaiwa kuingilia Faragha ya mamilioni ya watumiaji kwa kutoa Taarifa zao Binafsi kwa Facebook, #Google na LinkedIn

Pia, ilishutumiwa kushindwa kuzuia wadukuzi kuingilia Vikao

Soma https://jamii.app/ZoomLawsuit

#DataProtection
YOUTUBE YAONDOA VIDEO MILIONI MOJA ZINAZOPOTOSHA KUHUSU #COVID19

Taarifa ya #YouTube inayomilikiwa na Kampuni ya #Google inajiri wakati mitandao ya kijamii ikishutumiwa kushindwa kudhibiti usambazaji wa habari potofu kuhusu #CoronaVirus

Soma - https://jamii.app/TubeDeleteVideo
#UVIKO3
UCHAGUZI URUSI: #GOOGLE NA APPLE ZAONDOA 'APP' YA NAVALNY

Mamlaka zilitishia kutoza faini Kampuni hizo ikiwa zitakataa kuondoa 'Smart Voting App' ya Kiongozi wa Upinzani, Alexei Navalny

Uchaguzi wa Bunge unafanyika kwa siku tatu kuanzia leo

Soma https://jamii.app/NavalnyApp
Takwimu kutoka tovuti ya Global Stats Counter zinaonesha kivinjari (Browser) cha Chrome kinachomilikiwa na Kampuni ya #Google kinatumiwa na watu wengi zaidi

Kinatumiwa na zaidi ya 64% ya watumiaji wote wa intaneti duniani, ikifuatiwa na kivinjari cha Safari

#JamiiForums
URUSI: GOOGLE YAPIGWA FAINI YA TSH. BILIONI 225.7

Kampuni ya #Google inatuhumiwa kushindwa kuondoa maudhui ambayo Urusi inasema yanaenda kinyume na Sheria

> Kampuni za Meta na #Twitter pia zimewahi kupigwa faini kwa kosa kama hilo

Soma https://jamii.app/FainiGoogleUrusi

#DigitalRights
TEKNOLOJIA: GOOGLE KUFUNGUA KITUO CHA BIDHAA NAIROBI

Kituo hicho kinalenga kukuza Bidhaa na Huduma za "mabadiliko" kwa soko la Afrika na dunia nzima

#Google inalenga kuwekeza Dola Bilioni 1 Barani Afrika katika miaka mitano ijayo

Soma - https://jamii.app/GoogleKE

#Technology
#DATAPRIVACY: Shirika la Ulinzi wa Taarifa la Ufaransa linaituhumu Kampuni ya #Google kwa kuwatumia matangazo Watumiaji wa Gmail bila idhini yao

> Hii ni kinyume na Sera ya Faragha na maamuzi ya Mahakama ya Haki ya Umoja wa Ulaya

Zaidi - https://jamii.app/MalalamikoGoogle

#JamiiForums
πŸ‘10
MAREKANI: Kampuni mama ya #Google (Alphabet) imetangaza kupunguza Wafanyakazi 12,000 kutokana na Mdororo na Ukuaji Mdogo wa #Uchumi usioendana na Mapato ya Kampuni kwa Miaka 2 mfululizo

Watalipwa Mishahara ya Miezi 2, Bonasi za Mwaka 2022, Posho za Likizo, Fidia ya Kuachishwa Kazi kwa Wiki 16 na Wiki 2 za ziada, Miezi 6 ya Huduma za Afya na Msaada wa Huduma za Ajira na Uhamiaji

Soma https://jamii.app/GoogleLayoff

#DigitalWorld #EconomyCrisis #JFDigitali
πŸ‘7πŸ€”2
KENYA: Rais #WilliamRuto ameiagiza Wizara ya #TEHAMA na Uchumi wa Dijitali kuandaa Sheria itakayovutia Uwekezaji wenye Ushindani katika Masuala ya Kidijitali huku akieleza kuwa Serikali yake imeweka nia ya kutengeneza mazingira yatakayovutia Kampuni za Teknolojia kuwekeza zaidi Nchini humo

Kauli ya Ruto inakuja siku chache tangu aanze ziara ya siku 10 katika Mataifa ya #Marekani na #Uingereza ambako amefanya mazungumzo na baadhi ya Kampuni za Kiteknolojia zikiwemo #Starlink, #Apple, #Intel, #Google, na #Microsoft

Kupitia ziara hiyo, Bosi wa Apple, #TimCook aliahidi kuwa kampuni hiyo itaanza maandalizi ya kuwekeza katika Chuo cha Wanasidi Programu (Developers) huku Bosi wa Microsoft, #BradSmith akiielezea #Kenya kuwa kivutio cha Uwekezaji mkubwa wa Kampuni za Kimarekani

Soma https://jamii.app/RutoOnICT

#JamiiForums #DigitalRights #Innovations #Technology #TechWorld #Accountability #Governance
πŸ‘8πŸ”₯1πŸ‘1
Benki ya Dunia (WB) imeitaka Kenya kufanya mabadiliko ya Sheria inayoweka ulazima kwa Kampuni Nchini humo kutunza #TaarifaBinafsi kwenye 'Server' zilizopo ndani ya Nchi ikilenga kurahisisha Uwekezaji wa Huduma za Kidijitali kutoka Mataifa mengine

Kwa mujibu wa WB, Sheria hiyo inaweka vikwazo vya Kibiashara kwa Huduma za Dijitali hasa wakati ambao Kampuni kubwa Duniani ikiwemo #Google, #Meta, #TikTok, #Netflix, #Oracle, #Apple na #Microsoft zikizidi kufungua fursa za Uwekezaji Nchini humo na kuwa chanzo muhimu cha Ajira na Mapato ya Kodi

Soma https://jamii.app/ServerKenya

#JamiiForums #Governance #PersonalDataProtection #DataPrivacy #Accountability
πŸ‘4
Andrew Karamagi (Uganda), akiwa kwenye Maadhimisho ya Wiki ya AZAKI, ametambulisha dhana inaitwa 'Techno-Feudalism' yaani Ukabaila wa Kiteknolojia

Anasema Duniani kuna Kampuni kubwa Tano (5) za #Teknolojia yaani Alphabet (inamiliki #Google), #Meta (inamiliki Facebook, #Instagram, #WhatsApp), Amazon, #Apple na Microsoft

Kampuni hizi zinamilikiwa na Watu wachache na tunawapa taarifa nyingi mno ikiwemo alama za vidole, sura zetu n.k. Hatujui zinaenda wapi na Kampuni hizi zina pesa sana kiasi kwamba Bajeti ya kununua vifaa vya Ofisi tu vya #Google ni zaidi ya pato la Taifa la Nchi zetu.

Je, nchi zetu zikitaka kutengeneza #Sheria za kusimamia Kampuni hizi zitaweza?

Kila mara unapoenda Mtandaoni kununua kitu unaamini unanunua bidhaa, ila ukweli mchungu ni kuwa wewe ndio bidhaa. #Taarifa zako zinauzwa kwa Kampuni mbalimbali na zina thamani kweli kweli

#JamiiForums #DigitalWorld #TechnoFeudalism #TechGiants #CSOWeek2023 #WikiYaAZAKI2023 #Technology
πŸ‘2
#MAREKANI: Kampuni ya #Apple imekiri kutoa taarifa za itikio la haraka (push notification) kwa siri kwa Serikali mbalimbali ambazo zimekuwa zikifuatilia shughuli za Programu za Watumiaji wa Simu za Apple na #Google na kuwezesha Upelelezi wa Serikali hizo

#PushNotifications ni sehemu ya Programu ya Simu ambayo humjulisha Mtumiaji kuhusu Ujumbe mpya wa Maandishi, Barua Pepe, Maoni kwenye Mitandao ya Kijamii, Habari mpya, na shughuli yoyote ya programu ambayo haijafunguliwa.

Soma https://jamii.app/AppleDataBreach

#DataPrivacy #PersonalDataProtection #JFDigitali #Accountability #JamiiForums #JFSC
πŸ‘7❀1
MAREKANI: Mahakama ya Rufaa imetupilia mbali kesi iliyodai kwamba Kampuni 5 kubwa za Teknolojia (#Apple, #Microsoft, #Tesla, #DellTechnologies na Kampuni Mama ya #Google, #Alphabet) zilikuwa zimehusika kutumikisha Watoto katika kuchimba Kobalti Nchini DR Congo kwa kuwa ndio Wateja wakubwa wa Kolbati (Colbat)

DRC inazalisha 60% ya Kobalti inayosambazwa Duniani, madini muhimu yanayotumika katika utengenezaji wa vifaa vingi vya Elektroniki, ambapo takriban Watoto 25,000 wanatajwa kufanya kazi katika Migodi hiyo

Kesi hiyo ilifunguliwa Mwaka 2019 na Shirika la International Rights Advocates, lililokuwa linawakilisha Watoto walionusurika au kuumia, pia Familia za Watoto waliopoteza Maisha wakati wakifanya kazi katika Migodi hiyo

Soma https://jamii.app/ChildLabourDRC

#JamiiForums #HumanRights #DRC
πŸ‘1
Akishiriki Mjadala wa Athari za Taarifa Potoshi kwa Mpiga Kura, Mkufunzi kutoka Nukta Africa, Daniel Mwingira amesema Maswali ya kujiuliza ya muhimu kabla ya kusambaza taarifa ni, Je, picha imetumwa au kupostiwa na nani na katika muda gani? Huku akitoa mifano ya nyenzo za kutumia katika uhakiki wa taarifa

Amesema "'Tools' za kugundua taarifa potoshi zipo za aina mbalimbali, mfano ipo ya kutambua picha au video. Kuna β€˜tools’ za Mtandaoni, Mfano unaweza kutumia #Google ili kutambua picha au video husika"

Soma https://jamii.app/XspaceSept30

#JamiiForums #JFDemokrasia #JFSpaces #FakeNewsAwareness #Disinformation #TaarifaPotoshi #MisinformationAwareness