Rais wa Rwanda, #PaulKagame amemshutumu Rais wa #DRC, Fรฉlix Tshisekedi akidai anatoa matamko tofauti na wanayokubaliana juu ya Mgogoro wa Nchi hizo
Asema Tshisekedi amekuwa akitoa matamko ya kuilaumu #Rwanda badala ya kutatua changamoto za Nchi yake
Soma https://jamii.app/Rwanda
#Diplomacy

๐1๐ค1
#DRC: Raia waandamana nje ya Ubalozi wa Ufaransa, kupinga ziara ya Rais Emmanuel Macron inayotarajiwa baadaye wiki hii
Wanaishutumu #France kwa kuegemea upande wa #Rwanda, ambayo inatajwa kuunga mkono waasi wa #M23
Soma https://jamii.app/AntiMacronProtests
#DRCRwandaConflict

๐2
DRC: WANAMGAMBO WA ADF WAUA WATU 17
Mauaji hayo yametokea Kijiji cha #Kirindera, Jimbo la #Kivu Kaskazini. Watu wengine wanne wamejeruhiwa
Siku chache zilizopita, Wanamgambo hao walilipua Watu 40 eneo la Mashariki mwa #DRC ambapo kuna machafuko
Soma https://jamii.app/ADFKillings
#HumanRights

๐3๐1
CAF: YANGA YAWEKA REKODI, YAIPIGA TP MAZEMBE NJE, NDANI
Goli la Farid Mussa limeipa Yanga ushindi wa 1-0 ikiwa Jijini Lubumbashi, #DRC katika mchezo wa Kundi D kwenye Kombe la Shirikisho Afrika
#Yanga imekuwa timu ya kwanza ya #Tanzania kuifunga #TPMazembe mechi mbili za ushindani
Soma https://jamii.app/MazembeYanga
#JFSports #CAFCC

๐11
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Mbunge wa Kisesa, Luhaga Joelson Mpina amehoji hivyo wakati akichangia Azimio la Bunge katika mapendekezo ya kuridhia Itifaki ya Biashara ya Huduma ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika ya Mwaka 2012 (SADC Protocol on Trade in. Services, 2012)
Amehoji โRais #JakayaKikwete alisaini Itifaki hii Mwaka 2012, ina marekebisho gani? Sekta ya Fedha, Dola zimeadimika, Serikali inasema Watalii wameongezeka, Uwekezaji umeongezeka, Dola zimeenda wapi? Serikali ni lazima iwajibike kwa kutotatua uhaba wa Dola Nchini."
Wanachama wa #SADC walisaini Itifaki ya Biashara ya Huduma (Agosti 2012) na ilianza kutumika Januari 13, 2022 baada ya kuridhiwa na theluthi mbili ya Wanachama, #Tanzania ni kati ya Nchi 5 ambazo bado hazijaridhia, nyingine ni #Angola, #DRC, #Madagascar na #Comoro
Soma https://jamii.app/BungeAgosti31
#Governance #Diplomacy #JamiiForums

๐17โค2
#DIPLOMASIA: Takriban Malori 250 kutoka Tanzania yaliyobeba Shaba (Copper) yanashikiliwa Nchini DR-Congo kutokana na mgogoro wa kodi baina ya Serikali ya #DRC na Kampuni za Madini zilizopakia Mzigo huo
Malori hayo na Madereva wake wamekwama kwenye mpaka wa Kasumbalesa ambapo Balozi wa Tanzania Nchini Congo, Said Mshana amesema Ofisi yake inashughulikia Changamoto hiyo ili kubaini Ukweli
Soma https://jamii.app/MaloriDRCKodi
#JamiiForums #Diplomacy #TaxPayments

๐7โค1
#DRC: Shambulio lililofanywa na Wanamgambo wa Allied Democratic Forces (ADF) ambao wanatajwa kuwa na uhusiano na Kundi la IS, eneo la Oicha, Mji wa Beni katika Jimbo la Kivu Kaskazini limesababisha mauaji ya watu zaidi ya 20 wakiwemo Watoto
Hali ya hofu imekuwa kubwa ambapo raia wameandamana na kuteketeza magari ya kusambaza chakula wakidai hawahitaji msaada wa Kibinadamu bali wanahitaji usalama wao
#Uganda na DRC zilizindua operesheni ya pamoja Mwaka 2021 dhidi ya #ADF ili kuwafukuza wapiganaji hao kutoka ngome zao lakini mashambulizi yameendelea
Soma https://jamii.app/MoreThan20Killed
#HumanRights #Governance #Accountability #JamiiForums

๐3โค1
DR CONGO: Kikosi cha Kanda ya Afrika Mashariki kimeanza kuondoka eneo lenye machafuko lililopo Mashariki nchini humo baada ya wenyeji kudai Jeshi hilo halifanyi kazi iliyowapeleka eneo husika kama inavyotakiwa
Wanajeshi hao waliwasili eneo husika Novemba 2022 wakiitikia wito wa maombi ya Serikali ya #DRC kusaidia udhibiti wa kundi la waasi la M23
Ikumbukwe zimesalia siku chache kabla ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Desemba 20, 2023
Soma https://jamii.app/KenyanTroopsExit
#Governance #Democracy #Diplomacy #JamiiForums

BAADA YA WAASI KUDAIWA KUUA WATU 20, BURUNDI YAFUNGA MPAKA WAKE NA RWANDA
Serikali ya Burundi imechukua uamuzi huo baada ya kuishutumu #Rwanda kuwa inafadhili vikundi vya waasi vinavyopambana na Serikali
Rais wa Rwanda, #PaulKagame amekanusha tuhuma hizo lakini Serikali ya Burundi imemtaja kuwa ni โJirani mbayaโ
Desemba 2023 Rais wa Burundi, #EvaristeNdayishimiye aliishutumu Rwanda kuwa inatoa mafunzo kwa Kundi la Waasi la #RedTabara ambalo anadai limehusika na mauaji ya Watu 20 yaliyotokea Mpaka wa Magharibi mwa Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (#DRC)
Soma https://jamii.app/BurundiRwanda
#Diplomacy #Diplomasia #Governance #JamiiForums

๐6
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa (#UN) wa kulinda amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (#DRC) wenye Wanajeshi 13,500, ambao umesaidia vita dhidi ya Waasi kwa zaidi ya miaka 20, unatarajiwa kuondoka Nchini humo ifikapo Disemba 2024
Tangazo limetolewa baada ya Serikali ya DRC kuitaka Tume ya UN kuondoka ikisema imeshindwa kuwalinda raia dhidi ya makundi yenye silaha yakiwemo Allied Democratic Forces (#ADF) na M23 kwenye maeneo yenye machafuko katika Majimbo ya Kivu Kaskazini, Kusini na Ituri
Aidha, Serikali ya DRC imeagiza kikosi cha Kanda ya Afrika Mashariki, kilichotumwa Mwaka 2023 kusaidia kukomesha mapigano, kuondoka nchini humo pia kwa sababu sawa na zile za UN
Soma https://jamii.app/UNInDRC
#Governance #Diplomacy #HumanRights #Accountability #JamiiForums

KENYA: Waziri wa Mambo ya Nje, Musalia Mudavadi amekanusha ripoti za kuwa #Kenya ina uhusiano mbaya na majirani zake, licha ya mizozo kadhaa iliyotokea hivi karibuni ambapo amesisitiza inatatuliwa Kidiplomasia
Kenya inakabiliwa na kesi ya usambazaji wa Mafuta na #Uganda, pia Januari 16, 2024 ilimaliza mzozo wa usafiri wa Anga na #Tanzania. Januari 5, 2024 #Sudan ilimrejesha nyumbani Balozi wake baada ya Kenya kuwa mwenyeji wa Mohamed Dagalo (Kiongozi wa vikosi vya Wanamgambo wanaopigana na Serikali)
Desemba 17, 2023, Jamhuri ya #DRC ilimrejesha nyumbani Balozi wake wa Nchini Kenya baada ya muungano mpya wa Waasi wa Kikongo wakiwemo M23 kuundwa Jijini Nairobi
Soma https://jamii.app/KenyaVsMajirani
#JamiiForums #Diplomacy #Governance

โค1๐1
NIGERIA: Wanafunzi 17 wa Shule 5 katika Jimbo la Yobe wamepoteza maisha kutokana na mlipuko wa Homa ya Uti wa Mgongo (#Meningitis), huku takwimu zikionesha kuna wengine 473 wanasumbuliwa na maradhi hayo
Homa hiyo ni maambukizi ambayo husababisha kuvimba kwa tabaka za nje za Ubongo na Uti wa Mgongo na inaweza kuhatarisha maisha ya Mgonjwa kama haitatambulika mapema na kutibiwa huku Wataalam wa Afya wanaeleza kuwa chanjo ni njia bora ya kuzuia Ugonjwa huo
2021 kulitokea mlipuko wa aina hiyo Nchini #DRC na kuua zaidi ya Watu 129 ambapo Tanzania kupitia Ofisi ya Mganga Mkuu ilitoa tahadhari kwa Wananchi na kueleza Homa hiyo inasababishwa na vimelea aina ya Bakteria (Neisseria Meningitidis) wanaoambukizwa kwa njia ya hewa na inachukua Siku 2 hadi 10 tangu kuambukizwa hadi kuanza kuonesha dalili
Soma https://jamii.app/MeningitisOutbreak
#PublicHealth #JamiiForums

โค2๐2๐คฎ1
MAREKANI: Mahakama ya Rufaa imetupilia mbali kesi iliyodai kwamba Kampuni 5 kubwa za Teknolojia (#Apple, #Microsoft, #Tesla, #DellTechnologies na Kampuni Mama ya #Google, #Alphabet) zilikuwa zimehusika kutumikisha Watoto katika kuchimba Kobalti Nchini DR Congo kwa kuwa ndio Wateja wakubwa wa Kolbati (Colbat)
DRC inazalisha 60% ya Kobalti inayosambazwa Duniani, madini muhimu yanayotumika katika utengenezaji wa vifaa vingi vya Elektroniki, ambapo takriban Watoto 25,000 wanatajwa kufanya kazi katika Migodi hiyo
Kesi hiyo ilifunguliwa Mwaka 2019 na Shirika la International Rights Advocates, lililokuwa linawakilisha Watoto walionusurika au kuumia, pia Familia za Watoto waliopoteza Maisha wakati wakifanya kazi katika Migodi hiyo
Soma https://jamii.app/ChildLabourDRC
#JamiiForums #HumanRights #DRC

๐1
RIPOTI: Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa masuala ya Amani na Usalama (#SIPRI) imesema matumizi ya Kijeshi Duniani yameongezeka kwa asilimia 7 kwa Mwaka 2023 ikiwa ni ongezeko kubwa tangu Mwaka 2009 huku Nchi zilizoongoza zikiwa ni Marekani, #China na Urusi
Katika Mataifa ya Afrika, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (#DRC) iliongeza matumizi yake kwa asilimia 105, ikiwa moja ya Nchi iliyo na matumizi makubwa ya Kijeshi, kutokana na mgogoro unaoendelea kati ya Serikali, na makundi ya Waasi.
Soma https://jamii.app/MilitarySpending2023
#JamiiForums #MilitarySpending #Conflicts #NATO

๐3
Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema takriban watu Milioni 25.4 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanakabiliwa na Mgogoro wa Kiafya na Kibinadamu, kutokana na kuongezeka kwa vurugu za waasi wa #M23 zinazosababisha watu kuyahama Makazi yao, Magonjwa kusambaa kwa Kasi, Ukatili wa Kijinsia na kudorora kwa Afya ya Akili
Afisa Mwandamizi wa dharura wa WHO, Dkt. Adelheid Marschang amesema Mgogoro wa #DRC unabaki kuwa moja ya Migogoro ambayo haipati ufadhili wa kutosha, jambo ambalo linakwamisha uwezo wa watu kupokea vifaa vya msaada na huduma zinazohitajika ili kuwakinga dhidi ya Magonjwa ya kuambukiza, Njaa, na #UkatiliWaKijinsia
Marschang alisema WHO imepokea Dola Milioni 6.3 (takriban Tsh. Bilioni 16.83) pekee kati ya dola Milioni 30 (Tsh. Bilioni 80.16) inazohitaji, huku katika nusu ya mwaka 2024 pekee ikiripoti zaidi ya visa 20,000 vya #Kipindupindu vikiwemo vifo 274, vingi vikiwa katika jimbo la #KivuKaskazini, na visa 65,415 vya #Surua, ikijumuisha vifo 1,523
Zaidi https://jamii.app/MsaadaWaKibinadamuDRC
#JamiiForums #Afya #PublicHealth #SocialJustice #HumanRights #DRCCrisis #WomenRights

๐4โค1
AFYA: Baada ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kutangaza Ugonjwa wa #Mpox kuwa dharura ya Afya Kimataifa Agosti 14, 2024, Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya imetoa tahadhari ya Ugonjwa huo na kuongeza hadi sasa hakuna rekodi ya Maambukizi Nchini
Taarifa imesema Wizara inaandaa miongozo ya tiba na kinga kwa Watumishi, pamoja na kuimarisha uwezo wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii ili kuweza kupima sampuli za ugonjwa wa Mpox.
Aidha, visa vya ugonjwa wa Mpox vimezidi kuongezeka katika nchi za jirani ikiongozwa na #DRC, ambapo hadi sasa watu 29 wanahisiwa kuwa na Maambukizi ya ugonjwa huo Nchini Kenya
Soma https://jamii.app/NoMpoxCaseInTz
#JamiiForums #JFAfya #Accountability

๐5
MICHEZO: Timu ya Taifa ya Tanzania โ#TaifaStarsโ imekwama kupata matokeo mazuri katika mwendelezo wa Michezo ya Kundi H โ Kufuzu Michuano ya Mataifa ya Afrika (#AFCON2025) kwa kupoteza mbele ya DR Congo Goli 1-0
Taifa Stars imepoteza mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Stade des Martyrs Jijini Kinshasa kwa goli la kujifunga la Clement Mzize dakika ya 53, hivyo #DRC imeendelea kuongoza Kundi kwa kuwa na alama 9 wakati Stars imebaki na pointi 4
Mchezo ujao wa #Tanzania ni dhidi ya wapinzani wao haohao unaotarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, Jumanne ijayo Oktoba 15, 2024
Soma https://jamii.app/DRCTZOct10
#JamiiForums #JFSports

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, #SamiaSuluhuHassan, amewataka viongozi wenzake wa Kikanda kuchukua hatua madhubuti kuhusu hali inayoendelea kuzorota katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (#DRC), akionya kwamba historia itawahukumu vikali endapo watafumbia macho mgogoro kati ya Serikali ya DRC na Vikosi vya #M23 ambao unatajwa kusababisha vifo vya takriban raia 700 huko #Goma
Rais Samia ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC, alizungumza hayo akitoa hotuba ya ukaribisho kwa Wakuu wa Nchi waliohudhuria Mkutano wa Pamoja wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (#SADC) uliofanyika katika Ikulu ya Dar es Salaam, Tanzania, ukiwa na lengo la kutafuta mwafaka wa mgogoro huo
Zaidi https://jamii.app/MkutanoKuhusuDRC
#JamiiForums

GAMBIA: Wizara ya Afya imetangaza mlipuko wa ugonjwa wa #Mpox baada ya kugunduliwa kisa kimoja kupitia uchunguzi wa kawaida jana Julai 22, 2025. Hii inafuatia ongezeko la maambukizi katika nchi jirani za Sierra Leone, Liberia na Guinea.
Wizara hiyo imesema kugundulika kwa ugonjwa huo katika nchi ambayo haikuwa na Mpox kunahitaji hatua za haraka, ikiwa ni pamoja na ufuatiliaji wa Wagonjwa na waliokaribiana nao pamoja na kutoa elimu kwa Jamii ili kuzuia maambukizi zaidi.
Ugonjwa wa Mpox uligundulika kwa mara ya kwanza Mwaka 1970 Nchini #DRC, husababisha homa, maumivu ya misuli na vidonda vikubwa vya ngozi vinavyofanana na majipu, na unaweza kusababisha kifo.
Soma https://jamii.app/GambiaMpoxOutbreak
#JamiiAfrica #JamiiForums #JFAfya #PublicHealth

This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Rais Samia Suluhu amesema hayo Februari 7, 2026, baada ya mazungumzo ya faragha na Rais wa #Uganda, Yoweri Museveni, yaliyofanyika Ikulu, akieleza kuwa reli hiyo awali ilipangwa kupita katika nchi mbili ambazo ni #Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (#DRC).
Taarifa zaidi https://jamii.app/SRGUgandaNaTz
#JamiiForums #Diplomasia #Uwajibikaji #JFDiplomacy