JamiiForums
✔
23.9K subscribers
40.7K photos
3.6K videos
34.7K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
#JFDATA: Mtandao wa Kijamii wa #Facebook umeongoza kwa kutumia kiasi kikubwa cha Intaneti Nchini hadi kufikia 'Gigabytes' (GB) Milioni 48.99 ambapo watumiaji wake waliangalia zaidi Video kupitia mtandao huo

Ripoti ya robo mwaka kutoka Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) imeonesha #YouTube unafuatia kwa Utiririshaji wa Video na Sauti, #WhatsApp nafasi ya 3, #TikTok 4 na #Instagram 5

Je, gharama za Bando za Intaneti zinakupa uhuru wa kufurahia huduma hizi Mtandaoni?

#JamiiForums #DigitalRights #JFHuduma #TCRAQ3Report
❤4👍2👎2
MAREKANI: META YASHUTUMIWA KUWAWEKA WATOTO HATARINI

Mdhibiti Mkuu wa Taarifa Binafsi na Faragha Nchini Marekani ameishutumu Kampuni hiyo inayomiliki Mitandao ya #Facebook na #Instagram kuwa haiweki udhibiti mzuri kwa ajili ya kuwalinda Watoto wanaotumia mitandao yao

Meta imejibu kuwa maelezo hayo ya Mamlaka ni ya Kisiasa, hivyo imewalaumu kwa kutoa kauli bila kushirikisha Watuhumiwa

Soma https://jamii.app/MetaUS

#DataPrivacy #DigitalRights #DigitalWorld
👍1
IRELAND: Kamisheni ya Umoja wa Ulaya (EU) inayosimamia Ulinzi wa Taarifa Binafsi (DPC) imeipiga faini kampuni ya #META baada ya kuendelea kuhamisha #Data za watumiaji wa #Facebook kwenda #Marekani, licha ya zuio la Mahakama

DPC ilitoa miezi 5 kwa #META kusitisha uhamishaji wa Taarifa Binafsi za Watumiaji wake ikiwa ni utekelezaji wa zuio la Mahakama ya EU lililotolewa mwaka 2020 dhidi ya kampuni zinazochakata na kuhifadhi #TaarifaBinafsi

Soma https://jamii.app/MetaFines

#JamiiForums #DigitalRights #DataProtection #DataPrivacy #Accountability
👍3
AFRIKA KUSINI: POLISI YAPELELEZA KIFO CHA MPELELEZI WA KESI YA THABO BESTER

Jeshi la Polisi la Afrika Kusini limesema linapeleleza kifo cha Brigedia Jackson Mkhaulesi (59) aliyekuwa akipeleleza kesi ya #ThaboBester

Muda mfupi kabla ya kukutwa kwenye gari lake, Mkhaulesi alihudhuria Mahakamani ambapo madai ya Mpenzi wa Bester, Dkt. Nandipha Magudumana kuwa alikamatwa #Tanzania kinyume cha Sheria yalikataliwa

Bester ambaye pia anajulikana kama 'Mbakaji wa #Facebook' akiwa gerezani alitengeneza uongo ionekane amefariki Mwaka 2022. Alikamatwa Aprili 2023 Nchini Tanzania akiwa na Mpenzi wake anayedaiwa kumsaidia kutoroka

Soma https://jamii.app/ThaboBesterUpdates

#Governance
👍3
MAREKANI: Kampuni #META inayomiliki Mitandao ya Kijamii ya #Facebook, #Instagram na #WhatsApp, imezundua 'App' nyingine ya Kijamii inayoelezwa kuwa itakuwa mshindani wa #Twitter

Mkurugenzi Mkuu wa META, #MarkZuckerberg amesema kuna kitu Twitter walipaswa kufanya na hawajakifanya hivyo 'Threads' inakuja kwaajili hiyo, japo itachukua muda kuifikia Twitter lakini Mtandao huo unalenga kuhudumia zaidi ya Watu Bilioni 1

Hata hivyo, Watumiaji wameonesha wasiwasi wao kuhusu kiwango cha 'TaarifaBinafsi zinazokusanywa na 'Threads' zikiwemo Taarifa za Afya, Fedha na aina ya Kivinjari (Browser), vyote vikiwa na uhusiano na Utambulisho wa Watumiaji.

Soma https://jamii.app/Threads

#JamiiForums #DigitalRights #Innovation #JFDigitali #DigitalWorld
👍9
ETHIOPIA: Mamlaka zimerejesha huduma za Kimtandao baada ya kufungia Mitandao ya #Facebook, #Telegram, #TikTok na #YouTube tokea Februari 9, 2023 kufuatia mvutano kati ya Serikali na Kanisa la #Orthodox

Kwa Miezi 5 wale tu waliokuwa wanatumia VPN ndio walioweza kuingia kwenye majukwaa ya Mitandao ya Kijamii, hivyo kuzidisha matumizi ya vifurushi vya #Internet

Soma https://jamii.app/MitandaoEthiopia

#JamiiForums #DigitalRights #InternetAccess #HakiZaKidigitali #Governance #JFDigitali
👍2❤1🤔1
Ili Wakazi wa #UmojaWaUlaya (EU) waweze kufurahia Haki zao za Msingi za Faragha (ad-free service) chini ya Sheria ya Umoja wa Ulaya pindi wanapotumia #Facebook na #Instagram, watatakiwa kulipia Tsh. 35,138 kwa Mwezi, au 421,667 kwa Mwaka ili kupata Faragha hiyo

Kampuni ya #Meta inayomiliki Mitandao hiyo ya Kijamii imekuja na pendekezo hili kama jaribio la kutii Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya EU inayotishia kuzuia uwekaji wa Matangazo kwa watumiaji bila idhini yao

Soma https://jamii.app/MetaPayForYourRights

#JamiiForums #DataProtection #DataPrivacy #JFDigitali #DigitalRights
👍3❤1
MAREKANI: Majimbo 41 na D.C. yamefungua mashtaka dhidi ya Meta yakidai Kampuni hiyo inadhuru Watoto kwa kuunda vipengele kwenye Mitandao ya #Instagram na #Facebook ambavyo vinawafanya kuwa na uraibu

Uamuzi huo umetokana na uchunguzi wa Mwaka 2021 kuhusu madai kuwa #Meta inachangia changamoto ya Afya ya Akili kwa Vijana wengi

Inadaiwa Meta ilijihusisha kuwanyonya watumiaji Vijana kwa faida, kuwapotosha kuhusu vipengele vya Usalama na kuenea kwa Maudhui hatari, Kukusanya taarifa zao na kukiuka Sheria kuhusu #Faragha ya Watoto

Soma https://jamii.app/MetaIGFC

#DataPrivacy #DataProtection #JFDigitali #DigitalRights #PersonalDataProtection #JamiiForums #MentalHealth
😐4👍3
#BIASHARA: Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema kitendo cha Serikali kupitisha Kodi ya Matangazo Madogo ya Mitandaoni kitawarudisha nyuma Wafanyabiashara wanaotarajia kufungua Maduka siku za mbele

Kauli ya Mbowe inakuja baada ya Kampuni ya #META inayomiliki Mitandao ya #Facebook, #Instagram, #WhatsApp na #Thread kutangaza kuwa Wafanyabiashara wanaotangaza Bidhaa zao kupitia Mitandao wataanza kukatwa 18% ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kuanzia Desemba 1, 2023

Amesema "Serikali inayotoa msamaha wa kodi kwa Kampuni zenye mitaji ya Mabilioni, imegoma kuwapatia Wananchi wake ahueni. Serikali inaendelea kujaza kodi kila sehemu huku ikishindwa kudhibiti wizi wa kodi ambazo Watanzania wamelipa"

Soma https://jamii.app/MboweVAT

#JamiiForums #Governance #DigitalRights #Accountability #FreeSpeech #Democracy
👍12❤4
#DIGITALI: Tume ya Udhibiti wa Maudhui Mitandaoni ya Umoja wa Ulaya (EU) imeitaka META, kampuni inayoendesha Mitandao ya Kijamii ya #Instagram, #Facebook, #Thread na #WhatsApp kujieleza namna inavyodhibiti maudhui ya Unyanyasaji wa Kingono dhidi ya Watoto

Wito wa kwanza ulitumwa META Novemba 2023 ukitaka maelezo ya Usalama wa Watoto Mtandaoni. #EU imesema mwisho wa wito ni Desemba 22, 2023, kinyume na hapo #META itachunguzwa kwa Mujibu wa Sheria za Umoja wa Ulaya

Sheria mpya ya Huduma za Dijitali ya Umoja wa Ulaya (DSA) inazitaka kampuni za #Teknolojia zinazojihusisha na Uchakataji wa Maudhui Mitandaoni kuhakikisha zinaondoa maudhui yasiyofaa na hatari kwenye mifumo yao.

Soma https://jamii.app/METAEU

#JamiiForums #DigitalRights #InternetSafety #CyberSafety #ChildRights #Accountability #JFDigitali
👍3
KENYA: Rais #WilliamRuto amesema Serikali yake imekamilisha makubaliano na Kampuni ya META na hivi karibuni itaanza kuwalipa Wabunifu na Wazalishaji Maudhui wanaochapisha kazi kupitia Mitandao ya #Facebook na #Instagram

Ruto amesema "Utawala huu umechukua hatua za makusudi kuwekeza katika tasnia ya ubunifu. Nina habari njema kwa wabunifu wetu na wale wanaofikiria kutoa maudhui kupitia #Facebook na #Instagram. Juzi tu, META imeridhia kutenga Pesa kwaajili ya Waandaji Maudhui"

Oktoba 2023, META ilithibitisha kuwa inafikiria namna ambayo Wakenya wataanza kulipwa kutokana na uzalishaji Maudhui huku ikianza na wanaochapisha Video kwa jukwaa la 'Reels' kupitia Instagram. Pia, Watumiaji Facebook wenye wachangiaji wengi watakuwa wanufaika

Soma https://jamii.app/METAPay

#JamiiForums #Economy #DigitalRights #Governance #SocialJustice #JFDigitali #JFSC
🔥3👍2❤1
KENYA: Tovuti ya #CitizenDigital imeendesha kura ya maoni Katika Mitandao ya Kijamii kuhusu tangazo la Rais #WilliamRuto la Nchi hiyo kuwa 'Visa Free' kuanzia 2024 ambapo kulingana matokeo ya kura za #FaceBook, #X, na #Instagram, takriban 72.8% walipinga uamuzi huo huku 27.2% wakiunga mkono

Wanaopinga wamedai utaleta vitisho vya Usalama wa Nchi kwa kuwa Watu wengi watakuwa wakimiminika na wahalifu wanaweza kuona kama mwanya, huku waliounga mkono walisema itaimarisha uhusiano wa Kidiplomasia na Mataifa mengine ambayo yataongeza Mapato ya Nchi kutokana na Wawekezaji

Soma https://jamii.app/WakenyaWapingaVisaFree

#JamiiForums #Diplomacy #Diplomasia #Governance #VisaFreeCountries #KenyaVisaFree
👍5❤3
MAREKANI: Akihojiwa wakati wa kikao cha Bunge la Seneti, Mkurugenzi Mtendaji wa #Meta, #MarkZuckerberg ameomba msamaha kwa Familia zinazodai Watoto wao waliathiriwa au kujidhuru kutokana na maudhui ya Mitandao ya Kijamii

Zuckerberg anayemiliki #WhatsApp #Instagram na #Facebook amesema hayo katika kikao ambacho pia kilihusisha Viongozi wa TikTok, Snapchat, X (Twitter) na Discord ambapo wote kwa pamoja walihojiwa kwa Saa Nne

Pia, Shou Zi Chew kutoka TikTok aliulizwa kama kampuni yake inatoa 'data' za watumiaji wa Marekani katika mtandao wao na kuipa Serikali ya China, alikanusha jambo hilo

Soma https://jamii.app/MitandaoKwaWatoto

#DigitalWorld #DigitalRights #ChildRights #Technology #JFDigitali #JamiiForums
👍4
NIGERIA: Kampuni ya #Meta imefuta akaunti 63,000 za #Facebook za Raia wa #Nigeria, kama hatua ya kudhibiti Utapeli wa Mtandaoni, akaunti 2,500 kati ya hizo zilikuwa zikifanya Utapeli wa Kingono

Imeelezwa kuwa, akaunti hizo zilitumika kulaghai pesa raia wa Marekani hususan Wazee na Watoto, kwa tishio la kuvujisha picha za utupu ambazo nyingine ni 'feki'

Pia, wamefungia akaunti za Matapeli wanaojifanya wawekezaji kwa kuahidi kiasi kikubwa cha fedha, huku wengine wakijifanya wawekezaji kwa kuahidi faida kubwa maarufu kama “#YahooBoys”

Soma https://jamii.app/FacebookKuvutaAkauntiUtapeli

#JamiiForums #DigitalSecurity #Uwajibikaji #CyberSecurity #DigitalWorld #CyberThreats
👍4
MAREKANI: Kampuni ya #META imewafukuza Wafanyakazi zaidi ya 24 ambao walibainika kutumia Fedha ziliwekwa kwenye Kuponi za Chakula wakiwa kazini na kununua Mahitaji mengine zikiwemo Sabuni za Kufulia na Dawa za Meno

META imesema imechukua uamuzi huo kwa Wafanyakazi wa #WhatsApp, #Instagram na #Facebook ambao wamekuwa wakitumia kinyume na makubaliano marupurupu, pia imewahamisha vitengo wengine

Kampuni hiyo imekuwa ikitoa Chakula bure kwa Wafanyakazi katika Migahawa ya Ofisi za Silicon Valley, na walio nje ya ofisi hupewa Dola 70 (takriban Tsh. 190,750) kila siku kwaajili ya Huduma hiyo kila siku.

Soma https://jamii.app/LayoffMeta

#JamiiForums #Governance #Accountability #SocialJustice
👍2
Mdau wa JamiiForums.com anadai Siku hizi Mtu akisema hatumii Mitandao ya Kijamii kama #Instagram na #Facebook ni jambo la kushangaza

Ameuliza kwa Vijana waliopo kwenye Mitandao ya Kijamii wanaitumia vipi nguvu ya Mitandao katika kujenga au kujiharibia Maisha yao?

Mjadala zaidi https://jamii.app/MatumiziVijanaMtandao

#JamiiForums #DigitalLiteracy #DigitalEmpowerment
#MatumiziYaMtandao #MtandaoSalama
Mdau wa Jukwaa la Mahusiano, Mapenzi na Urafiki anadai walijuana na mpenzi wake Mwaka 2023 kupitia #Facebook, lakini sasa anachanganyikiwa na ndoto za kimapenzi ambazo mpenzi wake amekuwa akiota mara kwa mara kuhusu mpenzi wake wa zamani.

Je, unamshauri nini Mdau apeleke mahari au aache?

Kusoma kisa hiki https://jamii.app/MpenziKuota

#JamiiForums #JamiiAfrica #Lifestyle #JFChitChats
😁1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Mwanasiasa na Balozi Humphrey Polepole akizungumza kupitia ukurasa wake wa #Facebook amesema "Huu Mchakato wa kupata Wagombea (ndani ya Chama Cha Mapinduzi - #CCM) umekosewa, wakati mwingine inatakiwa kubomoa ili tujenge, nimeongea na mzee mmoja amekiri kuwa pale walichemka."

Soma https://jamii.app/PolepoleWagombea

#Democracy #JamiiForums #JamiiAfrica #FreedomOfExpression
👍1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Mwanasiasa na Balozi Humphrey Polepole akizungumza kupitia ukurasa wake wa #Facebook amesema "Kwenye #CCM hakuna kuvuana nguo, wala wasisingizie kuwa tunakosoana kwenye vikao, sisi tusiokuwa na vikao tunakosoana hadharani."

Amesema hayo leo Julai 18, 2025 na kuongeza, "Hata walipokuwa wanafanya vibaya kwenye CCM, Mwalimu Julius Nyerere alitoka hadharani zaidi ya mara moja na kuwaambia waliokuwa wanakosea."

Soma https://jamii.app/WaojifanyaWanaCCM

#Democracy #JamiiForums #JamiiAfrica #FreedomOfExpression
❤1
IVORY COAST: Mahakama imemhukumu Tokpa Flan Japhet kifungo cha Miaka Mitatu jela na kumtoza faini ya Dola 8,500 (Tsh. Milioni 22.1) kwa kutoa maoni kwenye #Facebook akisema "Kama Mama wa Rais Alassane Ouattara angefanya 'utoaji mimba' angekuwa ameokoa Afrika." Kauli iliyotafsiriwa kama lugha ya kumdhihaki Rais.

Ofisi ya Mwendesha Mashtaka imesema adhabu hiyo ni sehemu ya juhudi za kudhibiti vitendo visivyofaa vinavyoongezeka kwenye Mitandao ya Kijamii.

Hukumu hiyo imetolewa miezi michache kabla ya uchaguzi wa Rais unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025, ambapo chama cha #RHDP kimemteua Rais Ouattara kuwania kwa mara ya nne.

Soma https://jamii.app/IvoryCoastRais

#JamiiAfrica #JamiiForums #FreedomOfExpression #UhuruWaKujieleza #Governance
❤1